KILA KITU HUTOKEA KWA KUSUDI

Jumanne iliyopita nilikuwa kwenye boti ya spidi kubwa toka Pemba kuja Unguja. Na ilikuwa safari ya masaa 3 na dk 20 hivi. Siku hiyo bahari ilichafuka sana na boti ilikuwa ikikita kwenye wimbi kama inagonga ukuta. Abiria tuliokuwa nao wengi walikuwa Wazenji, na hali ilikuwa tete sana. Wale abiria wa kizenji walianza kuomba dua ili ‘mungu wao’ awanusuru na wengi walikuwa wakitapika ovyo na wenye BP walikuwa wakizimia. Macho yangu yalipoiona hali hiyo, shetani alipata fursa ya kuniletea wazo la hofu, mashaka na woga wa kifo. Kwa wasiwasi mkubwa nikaanza kumwita Yesu ili atunusuru na kisha nikaiamuru bahari itulie, badala yake hali ikawa mbaya zaidi. Halafu ghafla Roho Mtakatifu akaanza kunisemesha, ” Hivi unadhani nahodha wa hii boti haoni hali hii ? Unadhani ni kwanini hapunguzi mwendo?…Nikamjibu sijui ni kwanini. Akaniambia, “Huyu nahodha hapunguzi mwendo kwa sababu hana MASHAKA, ANA IMANI, HANA HOFU KAMA WEWE, NA HAJAOKOKA NA WALA MIMI SIKAI NDANI YAKE”…Unajua nini kilitokea? Nilisikia aibu na fedheha sana, kwamba Imani yangu imepitwa na Imani ya mtenda dhambi. Nikamwambia Roho mtakatifu, “Nisamehe mpendwa wangu, nimekuhuzunisha, nimekuaibisha, nirehemu” Na hapo hapo hofu ikaisha na nikaanza kuwatia moyo abiria wenzangu, “Msiogope, hatutazama, hatutakufa, Yesu yumo ktk chombo hiki, tulieni, tutafika salama, hatuko kwenye orodha ya watakaokufa” …Kila nikikumbuka hili tukio, naelewa ya kuwa Mungu aliliruhusu ili nijifunze Imani kwa nahodha yule asiye na Yesu. **EVERYTHING HAPPENS FOR REASON AND FOR YOUR GOOD**

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “KILA KITU HUTOKEA KWA KUSUDI
  1. Nzuri sana mambo ya ajabu.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: