Thamani ya yesu

https://i2.wp.com/www.atotheword.com/wp-content/uploads/2010/04/first-fruit.jpg

Mungu akiangalia hapa duniani, anaona vituko, anawaona wanae (tulionunuliwa kwa damu ya thamani ya Yesu) tunaishi maisha chini ya kiwango. Anashangaa kwanini hatuna tofauti na watu wengine wa kawaida wasiomjua. Anashangaa kwanini sisi ni masikini ilhali Yesu alishafanyika masikini ili sisi tuwe matajiri kwa Yeye. Anashangaa kwanini miili yetu imekuwa masikani ya magonjwa, maradhi na madhaifu ya kila namna badala ya masikani ya Roho wake mtakatifu. Anashangaa kwanini tuna tabia kama za binadamu wa kawaida ilhali Roho wake mtakatifu yumo ndani yetu na anayo MATUNDA YA ROHO KWA AJILI YETU. Anashangaa kwanini tuna mawazo ya ubinafsi wakati Yesu alishaonesha kielelezo kwamba lazima tuishi kama SADAKA kwa ajili ya wengine. Anashangaa kwanini tunakimbilia miujiza wakati sisi wenyewe ni miujiza, ni wanadamu pekee wenye kuishi katika dunia iliyochafuka na bado hatutendi dhambi. Anashangaa kwanini tumekazana kutafuta umaarufu na majina hapa duniani ilhali hapa ni mahali pa muda tu na kuna siku tutang’ara kama jua (si zaidi ya miaka 100 toka sasa). Anashangaa kwanini tunayaamua mambo yetu kwa kutegemea milango 5 ya fahamu badala ya NENO LAKE. Anashangaa kwanini tunaenenda kama mataifa wasio na akili ilhali sisi wa dunia hii kama Kristo Yesu asivyo wa dunia hii. Anashangaa kwanini tunawekeza muda wetu na nguvu zetu katika vitu visivyo na thamani ya milele. Ebu amua kuwa wa tofauti, ishi sawa na Neno la Mungu, kipimo chako cha ubora kisiwe mtu fulani bali Neno la uzima. ** MUNGU ANASHANGAA- Na Mwl. Dickson**

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: