Kutana na roho mtakatifu

image

roho,mtakatifu

KUTANA NA ROHO MTAKATIFU…
Imeandikwa katika 2Kor 2:12, ” Hatukupokea roho ya dunia bali Roho atokaye kwa Mungu MAKUSUDI tupate kuyajua yale tuliyokirimiwa[tuliyopewa bure] na Mungu”
Kusudi mojawapo la Mungu kumpa Mwamini kipawa cha Roho Mtakatifu pale anapoamua kumpokea na kumwamini Yesu ni ili Roho Mtakatifu afumbue macho ya Mwamini huyo ili apate kuyajua yale ambayo Mungu tayari ametupatia sisi Waamini bure, kwa ukarimu kama zawadi iambatanayo na wokovu!
Hautaweza kujua haki zako ndani ya Kristo Yesu endapo Roho Mtakatifu hatafanya kazi yake ya kuyafungua macho ya roho yako ili ugundue na kujua yale ambayo Mungu amekupa…na kama hautajua haki zako kama Mkristo mbele za Mungu, hautaweza kuwa na maisha ya ustawi na mafanikio…maana kama haujui kuwa una kitu fulani, hautaweza kukitumia na kukifurahia maishani!
Yesu anasema yafuatayo kuhusu Roho Mtakatifu, “Atakapokuja huyo Msaidizi, Roho wa Kweli atokaye kwa Baba, hatanena kwa shauri lake mwenyewe, atachukua katika YALIYO YANGU na kuwapasheni…YOTE ALIYONAYO BABA YANGU NI YANGU” (Yohana 16:13,15).
Yote aliyonayo Mungu amempatia BWANA YESU, “Nimekabidhiwa yote na Baba yangu” (Mathayo 11:27)…atakayekujulisha yale yote aliyonayo Yesu ni Roho Mtakatifu…KAANAYE VIZURI…LINDA USHIRIKA WAKO NA YEYE…NA KAMA HAUJAWA NA UHUSIANO THABITI ANZA LEO..!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: