Neno la Mungu

image

NENO LA MUNGU…
Kuna tofauti kati ya Neno la Mungu na maelekezo ya Mganga wa kienyeji… Ila Wakristo wengi wanajaribu kulitumia kama MAGIC…Wanataka wakiwa kwenye shida walitumie na litoe matunda kwao…wanajitahidi hata ku-memorize baadhi ya mistari ya Biblia, kama hadithi za alfurela ulela…halitafanya kazi kwa style hiyo…Neno la Mungu linafanya kazi na kuwa halisi pale tu unapoamua kufanya kila kitu kwa neno au kwa tendo sawasawa na kile Neno la Mungu kisemacho…Pale Neno la Mungu linapokuwa sehemu ya maisha yako, kila utakaloliomba mbele za Mungu litakuwa lako…hautakuwa na ombi lisilojibiwa, maana Yesu anasema, “Ninyi mkikaa ndani yangu na MANENO YANGU NDANI YENU, OMBENI LOLOTE NANYI MTAPEWA/MTATENDEWA” (Yohana 15:7)
Kama ukiomba chochote mbele za Mungu, kwa mtaji wa Neno la Mungu lililojaa moyoni mwako kwanza, kabla ya kulitamka mdomoni, Mungu hatakunyima chochote…”Na huu ndio ujasiri sisi tulionao kwake, ya kuwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake [Neno lake] Yeye atusikia, na kama atusikia, TAYARI TUNAYO YOTE TULIYOOMBA” (1 Yohana 5:13-14)
Neno la Mungu linabeba kilichoko Moyoni mwa Mungu, linabeba Mawazo ya Mungu…kwanini? Ni kwa sababu NENO LA MUNGU NI MUNGU MWENYEWE (Yohana 1:1-3)
Neno la Mungu lina akili na ufahamu, “…LAWEZA KUYATAMBUA MAWAZO YA MOYO” (Waebrania 4:12)
Usiwe msikiaji au msomaji tu wa NENO LA MUNGU…” …maana yeye asikiaye/ asomaye Neno lakini asilitende ni sawa na mtu anayejiangalia kwenye kioo lakini baada ya muda anaisahau sura yake ikoje…” (Yakobo 1:22-24)
Nalipenda NENO LA MUNGU maana, “Neno la Mungu ni ROHO na ni UZIMA” (yOHANA 6:63)

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: