Siku ukigundua ulichoumbwa kufanya

image

SIKU UKIGUNDUA ULICHOUMBWA KUFANYA DUNIANI, UTAKUWA MTU HATARI KWA WATU NA HATA KWA SHETANI…
Yesu alipokuwa hapa duniani, alikaa kama mtu wa kawaida kwa muda wa miaka 29…Alipofikisha umri wa miaka 30, majira na muda sahihi ambao Mungu alimkusudia kuanza rasmi kazi ya kulitumikia kusudi la maisha yake, na Yeye Yesu alipodaka ndoto (Vision) ya Mungu maishani mwake na kisha akatangaza rasmi kule Kapernaumu, “ROHO WA BWANA YU JUU YANGU, MAANA AMENITIA MAFUTA KUWAHUBIRIA MASIKINI HABARI NJEMA, KUWATANGAZIA UHURU WALIOFUNGWA, KUWAFUNGUA WALIOSETWA, NA KUTANGAZA MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIKA…” (Luka 4:18-19).
Siku zote ukigundua KUSUDI LA UWEPO WAKO DUNIANI, UKAIONA PICHA YA NDANI YA WEWE HALISI, NA ROHO WA MUNGU AKAKUPA AMANI NA UHAKIKA…UNASHINDWA KUKAA KIMYA, UNAJIKUTA UNAAMINI HICHO HATA KAMA WOTE WALIOKUZUNGUKA HAWAELEWI USEMACHO AU WANAONA KAMA UMECHANGANYIKIWA…Yesu alipodaka ndoto ya Mungu juu ya maisha yake na kuidhibitisha, alishindwa kukaa nalo moyoni…aliamua kwenda hekaluni na kulitangaza mbele za wale watu kwa Ujasiri…Wengiwalimwona kama amechanganyikiwa…wengine walimkasirikia na kumkamata na kutaka kumuua…Unapodaka ndoto (Vision) ya Mungu…Marafiki hawatakuelewa, Ndugu zako hawatakuelewa, Wazazi wako hawatakuelewa…Kama ilivyokuwa kwa YUSUFU au kwa DAUDI…Ndoto ya Mungu (Vision) ni kubwa mno, haiwezi kuingia ndani ya mawazo ya mtu, haieleweki kwa Yeyote isipokuwa wewe uliyeibeba…Baadhi ya watu wataanza kupata picha pale unapoweka SKELETON/BLUE PRINT mezani NA HAO NI WACHACHE SANA…Lakini wengi wataelewa pale yatakapokuwa halisi…Ndio wanazinduka usingizini kwa mshangao, watasema, “KUMBE HUYU FULANI ALIKUWA AMEBEBA HAYA YOTE NDANI YAKE? KUMBE HAKUWA MTU WA KAWAIDA? DAH JAMANI…”
Bill Gates alikuwa kijana wa kawaida tu…ila alipogundua njozi ya Mungu maishani mwake…
Henry Ford alikuwa mtu wa kawaida sana, tena hakuwa na elimu kubwa kama baadhi yetu tulizonazo, lakini alipogundua Njozi ya Mungu maishani mwake…
Benny Carson alikuwa kijana wa familia masikini ya Wamarekani weusi, alipogundua Njozi ya Mungu kwake…
Steve Jobs, Abraham Lincoln, Smith Wigglesworth, Kathreen Kuhluman, Benny Hinn, Bill Graham, na wengine wengi hata wale ambao ni ROLE MODELS wako, Waligundua Njozi ya Mungu kwao ndio maana Dunia na Mazingira hayawezi kuwaficha!
UKIGUNDUA NDOTO YA MUNGU KWAKO, UNAKUWA MTU HATARI SANA…HAIJALISHI UMRI WAKO…ELIMU YAKO…HISTORIAYAKO nk

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
3 comments on “Siku ukigundua ulichoumbwa kufanya
  1. nasra david says:

    nampenda yesu, naitaj kumjua zaid na awe ndan yang

  2. leopdius matembe says:

    jaman bwana awatie nguvu kwa ili mungu awabarik

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: