HUITAJI KUJIPIGIA DEBE

si kwa mapenzi yetu bali kwa neema

Mara zote na siku zote, Yesu ndiye kielelezo na mfano wa namna gani tunapaswa kuishi na kuyaendesha maisha. Yeye anasema, “JITIENI NIRA YANGU, MKAJIFUNZE KWANGU…” (Mathayo 11:29). Tunajifunza nini kwa Yesu? Yesu alipokuwa hapa duniani, hakuwa na CAMPAIGN MANAGER, hakuwa na gazeti la kumpigia chapuo au kumtafutia umaarufu. Lakini bado aliwavuta watu maelfu maelfu kila alikokwenda. Si unakumbuka alipowalisha Wanaume 5000, wanawake wengi zaidi na watoto? Hakupiga mbiu kuwakusanya. Hakupiga debe kwa namna yoyote. Bali watu wenyewe walikusanyana wakisema, “Njoo twende, nimekutana na yule aliyesemwa na manabii, Yesu Mnazareti “(Yoh 1:41,45). Kilichowavuta watu kwa Yesu si Miujiza. Kilichowavuta kwa Yesu ni kile walichokiona, “NASI TUKAUONA UTUKUFU, UTUKUFU KAMA WA MWANA PEKEE ATOKAYE KWA BABA, AMEJAA NEEMA NA KWELI”(Yoh 1:14). Kila walipomwona Yesu, waliona UTUKUFU WA MUNGU. Waliona NEEMA YA MUNGU. Waliona KWELI YA MUNGU. Ndio maana walikuwa radhi kukaa siku 3 mfululizo wakimsikiliza, wakiwa na njaa tumboni lakini shibe na utoshelevu ndani yao. Wakiwa na uchovu na usingizi miilini mwao lakini wakiwa na nguvu tele mioyoni mwao na utukufu wa Mungu ukiwaatamia. Ukiwa na vitu hivi muhimu maishani mwako, hauhitaji KUPIGA DEBE, Marafiki watakuja, watu sahihi watakuja, utafanikiwa na kustawi, utamtumikia Mungu wako na Kuthibitika. Kumbuka, “HAUHITAJI KUPIGA DEBE”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: