Naipenda sana Dunia yangu

NAIPENDA SANA DUNIA YANGU IITWAYO IMANI…

imani

Hii ni dunia halisi isiyoendeshwa kwa kile ambacho macho yanaona au masikio yasikia…Wenyeji wa dunia hii tunaishi kwa kile kinachotoka kwenye kinywa cha Mungu [NENO LA MUNGU].
Tunatembea hata kama dunia inasema simama, ilimradi kinywa cha Mungu kimesema tembea…Tunastawi sana na kuchanua hata kama dunia inasema, “Haiwezekani, uchumi umeporomoka, hali ni mbaya” …Tunakuwa na afya na uzima muda wote hata kama dunia inalia kwa kila namna ya ugonjwa na maradhi, kwa sababu Mungu mwenyewe ni “MUNGU ATUPONYAYE”…Tunafanya yale ambayo dunia inasema hayawezekani kwa vile Mungu amesema, “KWA MSAADA WANGU MTATENDA MAKUU”…Tunapita kwenye changamoto na ugumu kama wengine walio hapa duniani lakini hatuko katika msiba wao kwa sababu Mungu ametuhakikishia, “UJAPOPITA KATIKA MAJI MENGI HAYATAKUGHARIKISHA WALA KATIKA MOTO HAUTAKUUNGUZA” …Wakati dunia inasema ili ufanikiwe sera yetu ni WHOM YOU KNOW, Mungu anatwambia sisi, “MSIWE NA SHAKA, MNANIJUA MIMI, INATOSHA, MTAKUWA NA AMANI, NA MEMA YATAWAJIA”…Dunia inaposema unajua Mnajinyima raha na mnapitwa na wakati, Mungu anatunong’oneza, “MSIWE NA SHAKA, YOTE YATAPITA LAKINI NENO LANGU HALITAPITA KAMWE…NINALIANGALIA NENO LANGU ILI NIPATE KULITIMIZA…MIMI SI MTU NISEME UONGO WALA SI MWANADAMU NIJUTE…LIAMINI NENO LANGU HALITAWAANGUSHA”…Dunia inaposema Ni ngumu kuwa mtakatifu, mmevaa mwili, Mungu anatusemesha mioyoni mwetu kwa Furaha, “MSIWE NA SHAKA, SIHITAJI JUHUDI YENU ILI NIWAKUBALI KUWA NINYI NI WATAKATIFU WANGU MPENDWAO…NILISHAMFANYA YESU ASIYEIJUA DHAMBI KUWA DHAMBI ILI NINYI MFANYIKE HAKI YANGU…HAKUNA WA KUWAHUKUMU, MIMI MWENYEWE NDIYE NINAYEWAHESABIA HAKI…”
Hii ni Dunia yangu bora ninayokaa ndani yake, huwezi kunitoa hapo, huwezi kunibadilisha, huwezi kwa neno lako lolote au kwa tendo lako lolote…HUU NI MFUMO WANGU WA MAISHA, UKO KWENYE ROHO YANGU NAFSI NA MWILI WANGU…NI SEHEMU YA DAMU YANGU…NI UZIMA WA MUNGU [ZOE] NDANI YANGU

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: