Mambo yanayosababisha waliokoka…

image

MAMBO YANAYOSABABISHAWATU WALIOOKOKA WASIWE NA NGUVU ZA MUNGU NA UWEPO WAKE WAKATI WOTE…

1.Kukosa nidhamu katika MAMBO YANAYOINGIA MASIKIONI MWAO (UNAYARUHUSU MASIKIO YAKO YASIKIE NINI?)
Yesu alisema, “ANGALIENI JINSI MNAVYOSIKIA…”
Watu wengi waliookoka na Wakristo wengi, wana utapiamlo wa Nguvu na Uwepo wa Mungu kwa sababu wanatega masikio yao kusikiliza mambo yanayobomoa, na yanayokula Uwepo wa Mungu, kama vile Miziki ya kidunia, Michezo ya Luninga au Redio iliyojaa mizaha na Utani wa kipuuzi (Baraza la Wenye Mizaha: Zaburi 1:1-3)…Unaongea na kusikiliza maneno na mazungumzo ya aina gani ukiwa na marafiki zako? Ukiwa kazini? Ukiwa kwenye mikusanyiko isiyokuwa ibada? Kinachoingia Ndani yako kupitia masikio yako, kinaweza kukujenga au kukubomoa…Kama Unaamua kuwa Hekalu la Mungu na chombo chake cha kutunza Nguvu na Uwepo wake, lazima uyalinde masikio yako!

2.Kukosa Nidhamu katika MAMBO YANAYOANGALIWA NA KUTAZAMWA NA MACHO YAO (UNAYALISHA NINI MACHO YAKO?)
Kinachotazamwa au kuangaliwa na macho yako, kinajenga fikra na mawazo ndani yako. Na mawazo au fikra hizo zinaweza kuwa sawa na Neno la Mungu zikakujenga na kukuboresha kuwa chanzo cha Nguvu na Uwepo wa Mungu…Vitu kama Video CD za mahubiri, Mafundisho, Matendo ya Miujiza kwa Jina la Yesu na Kwaya(kidogo) vinasaidia kujenga Imani na mtazamo chanya wa Imani ambayo mwisho wa siku inakusaidia kuwa mtakatifu na kutunza Nguvu na Uwepo wa Mungu.
Wakristo wengi wamenaswa kwenye MAGAZETI YA UDAKU ambayo yamejaa mambo yaliyooza (corrupted) ambayo yanakula uwepo wa Mungu, na kudidimiza kiroho chao…(MIMI BINAFSI NI MUHANGA WA HILI…KWA MIAKA 7 TANGU NILIPOOKOKA, NILIKUWA NAPATA SHIDA SANA NA HAYA MAGAZETI NA VIJARIDA…LAKINI NILIPOAMUA KUHESABU GHARAMA NA KUJITOA KIKAMILIFU KWA YESU, NIMEKUWA HIVI NILIVYO SASA…Najua maisha yangu yanajieleza, sihitaji kukushawishi)…Pia wengine wamenaswa kwenye PICHA/VIDEO ZA UCHI NA NGONO (PORNOGRAPHS) ambazo ni chanzo kikubwa cha uharibifu katika Roho, Nafsi na Miili yetu ambayo ni hekalu la Mungu (1Kor 6:13-18)…Unapoangalia picha na video hizi, zinakujengea mawazo[imagination] ya hicho ukionacho, na mwisho wa siku utakuwa tayari umezini, maana Yesu alisema, “ANAYETAMANI, TAYARI AMEZINI MOYONI MWAKE” …Na kibaya zaidi, Dhambi hii mbaya inakufanya ukose ujasiri wa kumkabili shetani…ile inakuwa hukumu na kizingiti mbele zako, kila ukitaka kufanya kitu cha rohoni, shetani anakuletea ile picha au tukio chafu uliloangalia au ulilowahi kuangalia…Na pia ni chanzo kikubwa cha kuvamiwa na mapepo na nguvu za giza hasa Spiritual husbands and wives (wanaume na wanawake wa kipepo) ambao wanakuwa wanafanya mapenzi na wewe kwenye ndoto, wanavunja mahusiano yako unayoyaanzisha na mtu mwingine ili kuoana naye…wanawezakukufanya uwe na ndoa yenye mateso na kutoelewana hata kama utaolewa au kuoa, kama ni mwanamke unakuwa umekaa kiume ume (unapenda kutawala na kutoa amri), unakosa affection kwa mmeo/mkeo nk…Na hii inaondoka tu kama utaamua kuwa mkweli, ukaleta hoja zako kwa Watumishi wa Mungu wenye Nguvu(si kila mtumishi wa Mungu ana upako huu) na kisha kuvunja nao mikataba, na kumpa Yesu maisha yako kikamilifu, na ukifanya hivyo Yesu atakufungua na utafurahia maisha (Kama una tatizo katika eneo hili, mimi niko tayari kusaidia katika hili, maana huo upako wa kumnyanganya shetani mateka ninao…naye anajua hilo).
Movie si nzuri pia, zinaweza kukujenga kidogo lakini zina uharibifu mkubwa sana pia…Kama unataka usalama, achana nazo…badala yake angalia mafundisho ya Neno la Mungu kama burudani mbadala!

Kukaa na Mungu na Nguvu zake, Uwepo wake na Upako wake kila sekunde, na kumweka shetani chini ya miguu yako ni gharama sana…lazima uamue, na maamuzi yako yatakufanikishaau kukuangusha…AMUA VEMA, Linda masikio yako, Linda macho yako…kaa na Mungu!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “Mambo yanayosababisha waliokoka…
  1. Lucas Kombe says:

    Ninaota ndoto zinazonikwaza mara kwa mara. Nashiriki tendo la ndoa ktk ndoto na wanaume wenzangu, marafiki na hata ndugu zangu wa damu pia wanyama kama nguruwe na hata wanyama nisio watambua! Je utanisaidiaje ktk hizi ndoto!?

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: