MAMLAKA NA NGUVU…

Ili Mkristo awe na ufanisi na ubora ambao Mungu amekusudia, ni lazima awe na ufahamu wa kutosha kuhusu Mamlaka na Nguvu ya Mungu maishani mwake!
Tunajua ya kuwa Mungu wa rehema atamseta Ibilisi chini ya miguu yetu [sisi tulio mali ya Kristo na Warithi pamoja naye: Rumi 8:16-17]…(Rumi 16:20). Na ni vema ujue ya kuwa Mungu amemweka shetani chini ya Miguu yetu wakati huu tuliomo humu duniani, tukifika mbinguni hakuna haja ya kumseta shetani chini ya miguu yetu maana huko Mbinguni shetani alishafukuzwa na hana mahali pake tena…”MAHALI PAKE YEYE NA MALAIKA ZAKE[MAPEPO] HAPAKUONEKANA TENA BAADA YA KUTUPWA CHINI [DUNIANI] ” (Ufunuo 12:7-10)
Kwa hiyo ni muhimu sana ujue ya kuwa, Mamlaka na Nguvu ya Mungu inayotenda kazi maishani mwetu, inayomweka shetani chini ya miguu yetu INAFANYA KAZI WAKATI HUU TUKIWA KATIKA MWILI…Tukiondoka duniani, tunakwenda kuwa na Bwana milele, Uweponi mwake, ambako chochote kiovu na kinyonge [kama shetani] hakiwezi na hakitakuwepo!
Ni muhimu ujue ya kuwa, MAMLAKA BILA NGUVU HAINA FAIDA NA HAIFANYI KAZI…Unawakumbuka wale wanafunzi wa Yesu katika Mathayo 17? Walikuwa na Mamlaka ya Mungu, na walijaribu kumtoa yule pepo kifafa kwa yule kijana na wakashindwa. Na Yesu alipokuja, kutoka mlimani kuomba, alipoletewa yule kijana ili asaidie, alifanya kwa urahisi sana, na mara moja yule pepo alimtoka yule kijana. Wanafunzi wake walimuuliza BWANA, “Kwanini sisi tumeshindwa kumtoa?” Yesu aliwajibu, “JINSI HII HAIWEZEKANI ILA KWA KUFUNGA NA KUOMBA” Hapa Yesu alikuwa anazungumza siri ya kuwa na NGUVU ZA MUNGU MUDA WOTE…Alijua mamlaka wanayo, tena aliwapa mwenyewe katika Luka 10:19 na Luka 9:1, lakini alijua wanakosa NGUVU ZA MUNGU…Akawadokeza kuhusu KUFUNGA NA KUOMBA kama chanzo kimojawapo cha kuzipata NGUVU ZA MUNGU!
Kwa lugha nyepesi, Yesu alikuwa akiwaeleza kuhusu Zaburi 105:4 isemayo, “MTAKENI BWANA NA NGUVU ZAKE, UTAFUTENI USO WAKE SIKU ZOTE”
Alipowambia wawe WANAFUNGA NA KUOMBA, hakumaanisha kuwa Nguvu ziko kwenye kitendo hicho, la hasha! ila alimaanisha kuwa, KWA KUFUNGA NA KUOMBA, WATAUBANA NA KUUDHIBITI MWILI, NA KUIPA NAFASI ROHO KUKAA UWEPONI MWA BWANA, NA KUZIVAA NGUVU ZAKE NA ASILI YAKE, AMBAVYO VIKIWA NDANI YAO VITAMFANYA SHETANI ASIWEZE KUSTAHIMILI ILA KUTII AMRI NA MAMLAKA YAO.
ANGALIZO: Tunapofunga, hatufungi ili kutafuta nguvu zetu bali tunakuwa mbele za Mungu kwa utiifu na unyenyekevu, tukimlingana na kuupata uzoefu wa asili yake na nguvu zake. Tukitoka kule tayari tunakuwa ni HODARI KATIKA BWANA NA KATIKA UWEZA WA NGUVU ZAKE (Waefeso 6:10)
Unapofunga, unajizoeza kumkaribia Mungu, na kutokana na hilo, unajikuta tayari UPENDO wako na UTIIFU WAKO kwa Mungu vinapanda…Na Utiifu wako kwa Mungu ukipanda, Shetani na majeshi yake yote yanaanza kukutii wewe pia…”BASI MTIINI MUNGU.MPINGENI SHETANI NAYE ATAWAKIMBIA” (Yakobo 4:7).
UTII WAKO KWA MUNGU, UNAMFANYA SHETANI NA KAMBI YAKO KUKUTII WEWE [Hii ni kanuni ya Ufalme wa Mungu]!
Mamlaka inafnya kazi pamoja na Nguvu…Yesu mwenyewe alifanya yote aliyofanya kwa sababu ya mambo makuu 3 yafuatayo:
1.ROHO MTAKATIFU
2.NGUVU
3.MUNGU ALIKUWA PAMOJA NAYE AKITENDA KAZI ZOTE
Tunaupata ushahidi huu wa muhimu kutoka katika Matendo ya Mitume 10:38 isemayo, “HABARI ZA YESU KRISTO WA NAZARETH, JINSI MUNGU ALIVYOMPAKA MAFUTA KWA ROHO MTAKATIFU NA KWA NGUVU, AKAZUNGUKA HUKU NA HUKO AKITENDA MEMA, NA KUWAPONYA WOTE WALIOONEWA NA IBILISI KWA KUWA MUNGU ALIKUWA PAMOJA NAYE”
Tuyaangalie haya mambo 3 Muhimu;
ROHO MTAKATIFU
Yesu alipomaliza tu kubatizwa na Yohana pale Yordani, mbingu zilifunguka na sauti ya Mungu Baba ikasikika, “Huyu ni mwanamgu mpendwa ninayependezwa naye, msikilizeni” halafu Roho Mtakatifu akaja juu yake kama hua/njiwa (Mathayo 3:16)
Yesu mwenyewe alisema wazi wazi ya kuwa alikuwa na Roho Mtakatifu, “ROHO WA BWANA YU JUU YANGU, MAANA AMENITIA MAFUTA KUWAHUBIRIA MASIKINI HABARI NJEMA, KUWAWEKA HURU WAFUNGWA, KUWAFUNGUA WALIOSETWA…” (Luka 4:18)
Na hata alipowajibu wale Mafarisayo ya kuwa anatoa Pepo kwa Mamlaka gani? Yeye aliwajibu kwa uwazi, “NINATOA PEPO KWA ROHO MTAKATIFU”
Muhimu: Wakristo wanaangaika na mapepo kwa sababu wanadhani ya kuwa Pepo atatoka tu kwa kumwamuru kwa Jina la Yesu, bila kuwa na ufahamu na uelewa kuhusu Utendaji wa Roho Mtakatifu katika kulitukuza Jina la Yesu walilotumia. Na ndio maana wana mahusiano mabovu na Roho Mtakatifu na wanakemea pepo mpaka sauti zinakauka, kwa masaa mengi sana…inakera kweli!

NGUVU
Yesu alisema, “HAKUNA AWEZAYE KUMTOA MTU KWENYE NYUMBA YAKE NA KUMFUNGA ISIPOKUWA ANA NGUVU KULIKO YEYE”
Kwa lugha nyepesi, hautamtoa Pepo au kuufukuza Ugonjwa katika mwili wa mtu kama hauna nguvu ya Mungu ya kutosha…utajaribu na utachemka, Biblia inasema UTAZIMIA…”AZIMIAYE SIKU YA TAABU[VITA] NGUVU ZAKE NI CHACHE”

MUNGU ALIKUWA PAMOJA NAYE AKITENDA KAZI ZOTE
Ni vema uisome Injili ya Yohana sura ya 14, mstari wa 1 hadi ule wa 10. Yesu anasema, “MIMI NI NDANI YA BABA NA BABA NI NDANI YANGU…ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA…MIMI SITENDI JAMBO LOLOTE WALA SISEMI NENO LOLOTE…BALI BABA HUZITENDA KAZI ZOTE NDANI YANGU”
Sehemu nyingine wanafunzi wake walitaka kurudi nyuma na kumuacha, akasema, “NANYI MWATAKA KUNIACHA PEKE YANGU? SIKO PEKE YANGU, BALI BABA YU PAMOJA NAMI”
Ni muhimu uwe na uhakika ya kuwa Mungu yuko upande wako muda wote…usifanyechochote kwa mazoea au ujuzi wako, bali hakikisha ya kuwa Mungu yuko nawe!
MUNGU AKIWA UPANDE WETU, NI NANI ALIYE JUU YETU? (Warumi 8:31)
Daudi alishinda kila vita aliyokwenda kupigana wakati wa ujana wake na wakati akiwa Mfalme wa taifa la Israel, lakini alijua siri hii ya umuhimu wa Mungu kuwa Upande wake. Kabla ya kwenda vitani alimuuliza Mungu, “JE NIWAPANDIE UMEWATIA MIKONONI MWANGU? JE UTAKUWA NAMI?”
Na mara zote alipotoka vitani alisema kwa uhakika, “KAMA SI MUNGU ALIYEKUWA UPANDE WETU, ISRAEL NA ASEME SASA…”
Usipoteze ushirika wako na Mungu kila sekunde, Tunza utakatifu na ishi kwa utiifu kwa Neno la Mungu na sauti ya Roho Mtakatifu ndani yako!
PAMOJA TUFURAHIE MAMLAKA NA NGUVU YA MUNGU KUPITIA KWA KRISTO YESU!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
One comment on “MAMLAKA NA NGUVU…
  1. Yusuph says:

    Nafurahi kuona kazi ya Bwana Yesu inasonga mbele kwa kiwango cha kumshangaza shetani,kwa kadri shetani anavyozidi kushangazwa ndivyo Mungu anaamua kutushangaza na sisi kwa wema wake kwa kutukirimia yale yapasayo utauwa. Halleluyah…!!!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: