MTU MWENYE NDOTO KUBWA YA MUNGU NDANI YAKO…

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanawawinda watu wenye ndoto kubwa ya Mungu;

1.Roho ya Uzinzi

-Yusufu alikumbana na mke wa Potifa akashinda na kutunza ndoto yake
-Daudi alinaswa hapo, kwa Beltsheba na hiyo laana ikapita hadi kwa wanawe, mwanae Absalomu akalala na wake za babaze mchana kweupe
-Suleiman alidakwa hapa pia, akawa na wake 300 na masuria 700

-Samsoni alinasa kwa DelilahWachunguze watu wengi waliofanya makuu, wana kashfa nyingi za uzinzi, na ngono…ziwe za kweli au za uongo, kashfa ni kashfa tu, na hiyo roho ya adui ipo

2.Roho ya Mauti

-Yusufu alinusurika kutupwa na kufa mle shimoni kama si Mungu kuachilia Wafanyabishara wa Kiishmaeli waliomnunua
-Daudi aliwindwa kwa miaka zaidi ya 10 na Mfalme Sauli ili auwawe
-Musa alinusuriwa na mkono wa Mungu asiuwawe kwenye amri ya kuua watoto wa Kiebrania
-Yesu alinusurika kwa kukimbizwa Misri wakati Herode alipotaka kuua watoto wote wa kiumeYote haya yanahitaji kukaa miguuni kwa Mungu, na kujiachia kwake!
Mtu mwenye ndoto ya Mungu ni adui wa zinaa, hatembei ovyo ovyo na wanadada/kaka kama nguo, anajitunza na kujiheshimu, maana anajua ya kuwa “AZINIYE NA MWANAMKE/MWANAMME HANA AKILI KABISA…”(Mith 6:32) Na Mungu hatumii MATAAHIRA!
Mtu mwenye ndoto ya Mungu anakaa na Mungu siku zote, anakazana kumjua Mungu ili kwa msaada wake atende makuu(Zab 60:12)…Mtu mwenye ndoto ya Mungu anaijua thamani ya maisha na pumzi ya uhai, hachezei maisha wala kujihatarisha kwa upuuzi wowote ule…anakuwa na bidii katika kumpenda Mungu, na kwa kufanya hivyo, Mungu huwa anamshibisha kwa WINGI WA SIKU (Zaburi 91:11-16)

MIMI NINA NDOTO YA MUNGU, NAKAA NA MUNGU…NDANI YAKE NAISHI, NAKWENDA NAKUWA NA UZIMA WANGU (Matendo 17:28)
NINA UHAKIKA WA KUFIKA KILA MUNGU ANAPOTAKA NIFIKE, NINA UJASIRI WA KUYATANGAZA YASIYOKUWEPO KANA KWAMBA YAMEKUWEPO (Rumi 4:17)
NINAKUSUDIA NENO NALO LINADHIBITIKA KWANGU, NA MWANGA UNAZIANGAZIA NJIA ZANGU (Ayubu 22:28)
NINAFANYA BIDII SANA ILI NIMJUE MUNGU SANA KILA LEO, MAANA KWA KUFANYA HIVYO NITAKUWA NA AMANI NA NDIPO MEMA YATAKAPONIJIA[sitayafuata] (Ayubu 22:21)

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: