USIENDE…USISIMAME…USIKAE

 

Zaburi 1:1

jesus,usiende,usikae

“Heri [amebarikiwa] mtu yule ASIYEENDA katika shauri la wasio haki, Wala HAKUSIMAMA katika njia ya wakosaji, Wala HAKUKETI katika baraza la wenye mizaha”

Watu ambao wameokoka na mambo yao hayaendi, hayaeleweki wala hawapigi hatua kubwa za kiroho,kiuchumi na kimaisha wamenaswa katika maeneo haya makuu 3;

1.WANAKWENDA KATIKA SHAURI LA WASIO HAKI

Wana mfumo

wa maisha unaotegemea nini wanaona, nini wanasikia, nini wanahisi, nini wanaonja, na nini wanagusa…wanaishi kwa kutegemea ripoti ya milango mitano ya fahamu…Wanaishi kama wasio na Roho yule yule aliyemfufua Yesu toka kwa wafu…Wanaishi kama watu wasio na Roho yuleyule wa Imani aliyekuwa kwa Kristo Yesu…Wanaishi kama wasio kuwa na Roho wa Uzima yule yule aliyekuwa kwa Yesu na Kanisa la kwanza la Mitume…Wanaishi kama wanadamu wengine wa dunia hii wanavyoishi…wakisikia wengine wanasema hakuna pesa, uchumi mgumu, maisha ni magumu, na wao wanadakia hapo hapo na kulipokea hilo kwa furaha mioyoni mwao…Wanaanza kulia na kusikitika na kuhuzunika…Wanakubali kupokea ripoti ya dunia hii badala ya ripoti ya Ufalme wa Mungu…Hawataki kuliamini NENO na AHADI ZA MUNGU kwao…Wanaidhi kwa KUFUATA NAMNA YA DUNIA HII…WANAISHI KWA NA KWENENDA KWA SHAURI LA WASIO HAKI…WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA!

2.WANASIMAMA KATIKA NJIA YA WAKOSAJI

Wameruhusu maisha yao yachafuliwe na mifumo ya maisha ya watu wa dunia hii, wanaishi kana kwamba wamefika…wanaamini kila kijacho kwenye masikio yao, wanakitafakari hicho mchana na usiku kuliko NENO LA MUNGU…Wana muda mwingi wa kusoma magazeti, kusikia hotuba, kukaa vijiweni au katika maongezi ya watu wasiomjua Mungu na Uweza wake…WANAKUBALI KULISHA MAWAZO, FAHAMU NA MIOYO YAO KWA MANENO YA WAKOSAJI…Mwisho wa siku hayo unayopokea yanakujengea mfumo hasi na yanakukandamiza usiende mbele…Unaanza kwa kusikia, kusikia kunakujengea Imani ya kushindwa na kutokaa katika kusudi na mapenzi ya Mungu…Unaanza kubadilika taratibu, mwisho unakuwa mfumo wako wa maisha, japo kwa mdomo unasema, “YESU NI BWANA, NITAFANIKIWA, NITASOGEA, NITAPIGA HATUA”….Hii haitabadilika mpaka pale utakapojielewa na kuamua kujitoa katikati ya Wakosaji uliokaa kati yao kama marafiki, washauri, mashoga zako nk

3.WANAKETI KATIKA BARAZA LA WENYE MIZAHA

“…Mazungumzo mabaya[mizaha ikiwemo] huaribu tabia njema” na kama tabia njema ikiharibika au kufa…tabia mbovu inachipuka na kustawi, na inakua na kujiimarisha kadri udumuvyo kukaa katika hilo baraza la wenye mizaha…Linda sana Moyo wako kuliko yote ulindayo…Taa ya mwili ni macho, Linda macho yako…Yesu alisema, “ANGALIENI JINSI MNAVYOSIKIA”…Linda masikio yako…Kuwa mwangalifu sana…NENO LA MUNGU NI TAA YA MIGUU NA MWANGA WA NJIA ZETU!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: