KWANINi WAFANYABIASHARA WAKRIST0 WANACHEMKA???

image

mfanya biashara

Wafanyabiashara Wakristo, walio mali ya Kristo Yesu wanachemka, wanapanda leo kesho wanashuka, wanajaribu biashara hii na ile na hawatobozi [breakthrough] wanavutwa na kuishia kuwa na madeni na biashara zao kuvurugika….ziko sababu kadhaa ambazo zinawafanya wasipenye na kuwa na ustawi, nazo ni;

1.HAWANA UHUSIANO WA DHATI NA MUNGU ALIYE HAI, ATOAYE

NGUVU YA KUPATA UTAJIRI (Kumb 8:18)

Biblia inasema, “AKUSANYAYE BILA BWANA, HUTAPANYA”
Wafanyabiashara wengi walio wafuasi wa Kristo wanasota na kutopanda hatua kubwa za mafanikio kwa sababu mara wapatapo fursa za kibiashara, na mambo yao kuanza kuchanua, wakajenga nyumba, au wakakodisha nyumba nzima, wakanunua pikipiki,baiskeli, bajaj au kigari kimoja,  UTAJIRI (Kumb 8:12-18)
Wanakosa muda wa kukaa na Mungu…walikuwa waombaji, wasomaji wazuri wa Neno, Waliokuwa wakitafuta shauri la Mungu kwa kila jambo kabla ya kufanya chochote, lakini mafanikio kidogo yanawafanya wapate majina ya MR na MRS BUSY [Be Under Satanic Yoke]!

2.HAWANA NGUVU YA MUNGU (Waefeso 6:10)

Kwa sababu hawa wafanyabiashara wanaanza kuwa mbali na Mungu kwa kigezo cha U-BUSY…Nguvu za Mungu za kuwasaidia kuwa matajiri zinakata, wanaanza kuchechemea na wanachemka!
Biblia inaweka wazi, “HATIMAYE MZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA NA KATIKA UWEZA WA NGUVU ZAKE”
Hivyo wanaanza vizuri na wakishapata mafanikio kidogo, wanajitoa kwenye USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU….Wanaanza KUZITEGEMEA AKILI ZAO WENYEWE (Mith 3:5-7)…Hivyo wanakosa NGUVU YA MUNGU IWEZAYO KUYANYOOSHA MAPITO YAO…Wanadondoshwa na NGUVU ZA UPINZANI WA SHETANI NA MAJESHI YAKE YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (Waefeso 6:12)
Biblia iko wazi, “AZIMIAYE SIKU YA TAABU, NGUVU ZAKE NI CHACHE”

3.HAWAZINGATII HAKI (Mithali 8:18-21)

Neno la Mungu liko wazi katika hili…Mungu anasema, “UTAJIRI NA HESHIMA ZIKO KWANGU, NAAM, UTAJIRI UDUMUO NA HAKI PIA” (Mith 8:18)
Utajiri na Heshima ziko kwa Mungu aliye hai, ila utajiri wake unakujia pale unapoamua kukaa miguuni mwake na kuwa mtu wa HAKI katika mambo yote ufanyayo…Wafanyabiashara wengi walio Wakristo wamekosa katika eneo hili, HAWALIPI KODI STAHILI…WANATOA VIRUSHWARUSHWA ILI KUPATA HUDUMA FULANI FULANI…WANAWANUNUA WATU ILI WAWASAIDIE KUPATA TENDA AU KAZI, na WANATOKA NJE YA HAKI…NA UKITOKA TU NJE YA HAKI, UMEPISHANA NA MKONO WA MUNGU WA KUTAJIRISHA….Maana imeandikwa, “[Mimi BWANA] NAPITA KATIKA NJIA ZA HAKI, KATIKA MAPITO YA HUKUMU. NIWARITHISHE MALI WALE WANIPENDAO, TENA NIZIJAZE HAZINA ZAO” (Mith 8:20-21)
Ni lazima ujitahidi KUWA MTU WA HAKI….Mungu anasema, “WAAMBIE WENYE HAKI YA KUWA WATAKUWA HERI, MAANA WATAKULA MATUNDA YA MATENDO YAO” (Isaya 3:10)
Kila muda wewe Mfanya biashara Mkristo, “VAA DRII YA HAKI KIFUANI MWAKO” (Waefeso 6:14)
HAKI ina nguvu ya kuinua taifa…na kama inaweza kuinua taifa uwe na uhakika inaweza kukuinua wewe mtu mmoja ukiishi na kuilinda na kutoikwepa!

4.UAMINIFU KATIKA ZAKA[FUNGU LA KUMI] NA DHABIHU (Malaki 3:8-11)

Wanaokwenda kwa Shetani kutafuta utajiri, kabla hawajapewa Mashetani ya kuwasaidia huwa wanatoa SADAKA kwa Miungu hiyo…na Mungu pia ameweka utaratibu wa kurejeshewa 10% ya kila ukipatacho katika utendaji wako na uzalishaji wako (Walawi 27:30)
Wengi wa wafanyabiashara si waaminifu katika maeneo haya ya zaka na dhabihu, na kwa sababu hiyo wanakosa msaada wa Mungu ANAYEMKEMEA YULE ALAYE…Na kwa sababu hiyo kila wakikusanya, shetani anatawanya…yanaibuka mambo yanayosababisha pesa ziteketee, magonjwa, dharura za kila namna ili mradi tu pesa zinapukutika na biashara inadumaa au kufa…Hazina zako zinakuwa tupu na hakuna maongezeko.5.WENGI HAWAWAPI WATU VITU/ SI WAKARIMU (Luka 6:38)

Wafanyabiashara wengi hata wale wasiokuwa na Mungu wa kweli, wana utamaduni wa kuwapa watu misaada na kuigusa jamii kwa njia mbalimbali…Hii ni kanuni ya Biblia…”WAPENI WATU VITU NANYI MTAPEWA KIPIMO CHA KUJAA NA KUSUKWASUKWA NA KUSHINDILIWA, NDICHO WATU WATAKACHOWAPENI VIFUANI MWENU” (Luka 6:38)
Kumbuka, “ANYWESHAE HUNYWESHWA” na pia, “AMHURUMIAYE MASIKINI, HUMKOPESHA MUNGU, NAYE ATAMLIPA KWA TENDO LAKE JEMA”
Pia kumbuka, “AZUIAYE MKONO WAKE KUTOA ISIVYO SAWA, HUELEKEA UHITAJI”
Siku zote,”MKARIMU HUWANDISHWA/HUNENEPESHWA”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: