FAHAMU UWEZA NA NGUVU YA MSALABA…(Part 1)

Namwamini Mungu kuwa kabla ya mwaka huu kuisha, naweza kuwa nimemaliza kuandika kitabu hiki kizuri chenye Ufunuo kuhusu Msalaba(kile alichofanya Yesu Msalabani) na Nguvu yake kwa maisha yetu ya kila siku!
Yafuatayo ni baadhi tu ya Yale ambayo Msalaba wa Yesu umeyashughulikia;

1.UMEIVUNJA NGUVU YA DHAMBI( 1Yohana 3:8)

Yesu alidhihirishwa ili aiharibu N

GUVU YA DHAMBI…Alifanya hivyo kwa “KUZIBEBA DHAMBI ZETU MWILINI MWAKE JUU YA MTI[MSALABA], ILI TUKIWA WAFU KWA MAMBO YA DHAMBI TUWE HAI KWA MAMBO YA HAKI…” (1Petro 2:24)

2.ALILIPA GHARAMA YA DHAMBI KISHERIA (2Kor 5:21)

Yeye asiyeijua dhambi [Yesu] alifanyika dhambi ili sisi tupate kufanyika HAKI YA MUNGU…Badala ya sisi kulipia gharama ya dhambi, “MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI…” Yeye Yesu kama Mwanakondoo wa Mungu(Yohana 1:28,35) alichinjwa na kulipia adhabu ya dhambi zetu…Ndio maana alipokuwa Kalvari, kwa kule KUBEBA DHAMBI ZETU MWILINI MWAKE (1Petro 2:24), Mungu alimgeuzia mgongo na kumwacha, akapaza sauti na kulia, “MUNGU WANGU, MUNGU WANGU, MBONA UMENIACHA?”

3.AMETUFANYA WENYE HAKI WA MUNGU (Rumi 8:34)

Ni nani atakayewahukumu Wateule wa Mungu [sisi tulio ndani ya Yesu]? Mungu mwenyewe ndiye mwenye kuwahesabia haki, Maana Kristo Yesu alikufa, naam amefufuka na ndiye anayetuombea.
Ndiyo maana tuna ujasiri wa kumsogelea Mungu kama BABA na si HAKIMU kwetu kwa sababu ya kazi njema msalabani aliyoifanya Yesu….”TANGU SASA HAPANA HUKUMU YA DHAMBI JUU YAO WALIO KATIKA KRISTO YESU” (Rumi 8:1)

4.ALIYAPONYA MAGONJWA YETU NA UDHAIFU WETU (1Petro 2:24)

Mwenyewe alizichukua dhambi zetu mwilini mwake, ili tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki, NA KWA KUPIGWA KWAKE MLIPONYWA!
Biblia haisemi mnaponywa, inasema “MLIPONYWA” Ilifanyika pale msalabani tayari, sio kitu tunachokitafuta sasa au kesho…Msalaba ulioshughulikia DHAMBI ni huo huo uliokomesha Magonjwa yote na madhaifu yetu…UKIWA MGONJWA UMETAKA MWENYEWE, na wala usimsumbue Mungu kwamba akuponye…ALIFANYA HILO MIAKA ZAIDI YA MIAKA 2000 ILIYOPITA, Ndani ya kitabu changu “SABABU SABA ZA KIBIBLIA KWANINI USIWE MGONJWA” Nimelizungumzia hili kwa upana zaidi, JIPATIE NAKALA YAKO!

5.ALISHUGHULIKIA AMANI YETU (Isaya 53:5)
…Na adhabu ya AMANI YETU ilikuwa juu yake!
Kabla ya Kwenda msalabani, Yesu alitoa ahadi ya kutupatia AMANI YAKE, na akasema atupavyo Yeye ni tofauti na ulimwengu utoavyo (Yohana 14:27) na huo ulikuwa ni mkataba usiopitishwa, ulikuwa MSWADA wa kile ambacho alitaka kutupatia…alipokwenda Msalabani, alikamilisha hilo, sawa na nabii Isaya alivyotabiri zaidi ya miaka 600 kabla ya kifo chake!

6.ALIKOMESHA HUZUNI NA MASIKITIKO KWA KILA ALIYE WA KWAKE (Isaya 53:4)
Hakika ameyachukua MASIKITIKO YETU, amejitwisha HUZUNI ZETU!
Ndio maana tangu Kristo akishinde kifo na mauti, mahali pote ROHO MTAKATIFU kupitia kinywa cha Mtume Paulo aliwaambia Wafilipi, “FURAHINI KATIKA BWANA, TENA NASEMA FURAHINI, UPOLE WENU NA UJULIKANE NA WATU WOTE, BWANA YU KARIBU” (Wafilipi 4:4)
Hakuishia hapo, bali alizungumza tena na kanisa la Thesalonike akisema, “FURAHINI SIKU ZOTE. OMBENI BILA KUKOMA, SHUKURUNI KWA KILA JAMBO, MAANA HAYA NDIYO MAPENZI YA MUNGU KATIKA KRISTO YESU” (1Wathesalonike 5:16-18)
Ndio maana alipotupatia ROHO MTAKATIFU, kati ya MATUNDA anayoyatoa ni FURAHA (Wagalatia 5:22) kwa sababu alijua pasipo UWEZESHO NA NGUVU YA MUNGU MWENYEWE, tutapitia changamoto ambazo zitatuzuia kufurahi siku zote na nyakati zote, akamtoa MSAIDIZI-ROHO MTAKATIFU aje na package ya FURAHA pia kama kati ya MATUNDA YAKE!

TUTAENDELEA TENA WAKATI MWINGINE…MUNGU AKITUPA NEEMA…NAJUA MUNGU ANAWASEMESHA NA KUWASAIDIA KUPIGA HATUA KUBWA ZA IMANI KUPITIA HUDUMA HII…NAOMBA USISAHAU KUNIOMBEA ILI MUNGU ANIPATIE LAPTOP NA MODEM YA KWANGU, MAANA MAFUNDISHO HAYA NAYAPOST NIKIWA KWENYE INTERNET CAFE NA NI GHARAMA KUBWA SANA, NIKIPOST SOMO MOJA KAMA HILI, SH 1000 HADI 1400 ZINANITOKA…NAMI HII NDIYO KAZI YANGU, SIJAAJIRIWA NA KAMPUNI YOYOTE…HATA UKIJISIKIA KUNITEGEMEZA KWA PESA, AU HATA MODEM AU LAPTOP, MUNGU WANGU ATAKUBARIKI!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “FAHAMU UWEZA NA NGUVU YA MSALABA…(Part 1)
  1. EMMANUEL says:

    MUNGU awabariki

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: