MAMBO MAWILI YA MSINGI YA KUFANYA UWEPONI MWA BWANA

Kuna mambo mawili ya msingi sana ambayo mtu aliye wa familia ya Mungu anaweza kuyafanya wakati anapokuwa Uweponi mwa Mungu au anapojihudhurisha mbele za Mungu aliye hai…

Na mambo hayo yapo katika Marko 11:23-24 na yametokana na maneno ya Yesu Kristo Mwenyewe, naye anasema, ” Amin, amin nawaambia, Yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘ng’oka na utu

pwe baharini’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini ya kuwa yale ayasemayo yametukia, yatakuwa ya kwake. Yoyote muyaombayo mkisali, aminini ya kuwa mnayapokea nayo yatakuwa yenu”

JAMBO LA KWANZA: KUIAMURU MILIMA ING’OKE NA KUTUPWA BAHARINI, KWA IMANI PASIPO SHAKA MOYONI (mst 23)…

Si kila jambo linalokuja au kuletea changamoto maishani mwako ni la kwenda mbele za Mungu kwa machozi au kilio ili aje akusaidie, au aliondoe, mambo yote ambayo ni ya KUHARIBU, KUCHINJA na KUIBA katika maisha yako, yanatoka moja kwa moja kwa shetani na pepo wabaya katika Ulimwengu wa roho…Maana kazi ya shetani[mwizi] na jeshi lake la pepo wabaya ni KUCHINJA, KUIBA NA KUHARIBU (Yohana 10:10) kwa hiyo unapoona kuna mambo kwenye maisha yako move mountainhayako sawa, japo umejitahidi kufanya sehemu yako kwa uaminifu, na pia yanazidi KUHARIBIKA au haki zako na ahadi zako ZINAIBIWA na hazitokei kwako sawa na Mungu alivyosema, au kuna mambo yako YANAKUFA, Ndoa, kazi, uchumba, biashara, uchumi nk ujue tayari Shetani na kamapani yake wameweka mikono yao hapo na wanakuzuia…Kwa hili wala usisumbuke na kumsumbua Bwana Yesu, Shetani na jeshi lake wako ndani ya uwezo wako….UMEPEWA AMRI KUKANYAGA NYOKA NA NG’E NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI (Luka 10:19)…UMEPEWA MAMLAKA NA AMRI JUU YA PEPO WOTE NA MAGONJWA (Luka 9:1)…Mungu amekuamini, UKIMPINGA SHETANI ATAKUKIMBIA, ILIMRADI TU WEWE NI MTIIFU KWA MUNGU NA NENO LAKE (Yakobo 4:6-7)…UMEPEWA JINA LA YESU KAMA URITHI WAKO, KWA HILO KILA GOTI LINAPIGWA NA KILA ULIMI UNAKIRI YAKUWA YESU NI BWANA (Wafilipi 2:9-11)…Mungu aliye hai amekuhakikishia kuwa KILA MLIMA UTASHUSHWA NA KILA KILIMA KITASHUSHWA, KILA BONDE LITAINULIWA, NA KILA PALIPOPARUZA PATASAWAZISHWA (Isaya 40:4-5)
Simama ujitetee mbele ya Milima inayokukabili, Itazame milima kwa ujasiri, maana msaada wako u katika Bwana wa Majeshi aliyeziumba mbingu na nchi…Kwa Ujasiri kabisa iamuru hiyo milima yako iwe nchi tambarare, isage milima na kuvifikicha vilima (Isaya 41:11-14) fanya hivyo kwa IMANI pasipo Mashaka!

JAMBO LA PILI: UOMBE NA UAMINI YA KUWA UMEYAPOKEA YALE UYAOMBAYO MUDA ULE UOMBAPO, NAYO YATAKUWA YAKO (Mst 24)…

Ukiwa kwenye uwepo wa Bwana wa Majeshi, Mungu mkuu aliye hai, kama hauko hapo ili UZIPINGE HILA ZA IBILISI (Waefeso 6:10-18) basi jambo la pili la kufanya uweponi mwa Bwana ni kumsahau shetani na majeshi yake na KUPELEKA HOJA ZAKO ZENYE NGUVU…MKUMBUSHE NA MUHOJIANE, ELEZA MAMBO YAKO NAYE ATAKUPA HAKI YAKO (Isaya 43:26)…Ni wakati wa KUOMBA naye ATAKUPA, ni wakati wa KUBISHA naye ATAKUFUNGULIA, ni wakati wa KUTAFUTA naye ATAKUONESHA (Mathayo 7:7-8)…Ni wakati wa KUOMBA LOLOTE KWA JINA LAKE NAYE ATALIFANYA (Yohana 14:13-15, Yohana 16:23-24)…Ni wakati wa KUMWITA NAYE ATAITIKA NA KUKWONYESHA MAMBO MAKUBWA NA MAGUMU USIYOYAJUA (Yer 33:3)…Ni wakati wa kwenda Mbele za Mungu ukiwa na ushahidi wa NENO LAKE ambalo ndilo MAPENZI YAKE, na kuomba, KISHA YEYE ATAKUSIKIA, NA KAMA ATUSIKIA TAYARI TUNAZO HAJA ZOTE TUMWOMBAZO (1Yohana 5:14-15)..!
Kikubwa na cha muhimu kuzingatia ni kwamba, “YOYOTE MUYAOMBAYO MKISALI, AMININI YA KUWA MNAYAPOKEA [wakati uleule wa kuomba] NAYO YATAKUWA YENU”
Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “MAMBO MAWILI YA MSINGI YA KUFANYA UWEPONI MWA BWANA

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: