UMEUWEZA ULIMI WAKO AU UMEKUWEZA?

Mithali 18:20-21 inasema, ” Tumbo la mtu litashiba matunda ya kinywa chake…Uwezo wa mauti na Uzima viko kwenye ulimi, nao waupendao watakula matunda yake”

Kwenye ulimi wako kuna maneno, na maneno hayo uyatamkayo yana athari kubwa sana kwako na kwa wale unaowatamkia…Kwenye mdomo wako yanaweza kutoka maneno ya kutia UZIMA au ya KUUA/MAUTI…Inategemea na we unauelewa kiasi gani kuhusu nguvu ya Ulimi wako…Silaha kubwa na ya mabadiliko hasi ama chanya kwenye ulimwengu wa roho ni maneno yako…Kwa maneno yako unatengeneza maisha na kwa maneno yako unatengeneza mauti yako na ya wale unaowatamkia!

neno la mungu
Kwenye ulimi wako kuna nguvu ya ajabu, ambayo inafanya kazi hata kama unajua au hujui…ni silaha ifanyayo kazi mara tu uamuapo kufungua kinywa chako…”KWA KINYWA MTU UKIRI HATA KUPATA WOKOVU” (Warumi 10:10)…Kama ukinena maneno mema na kukiri mema katika hali zote bila kuangalia mazingira yako, uwe na uhakika unakuwa umefaulu kuulazimisha ulimwengu wa roho ufungue milango yake ya mema na mafanikio sawa ba ukiri wako mwema….Ukikiri au kuungama mabaya, kushindwa, lawama, manung’uniko na kutofanikiwa, sekunde ile ile mambo hayo yanatokea kwenye ulimwengu wa roho! Kwanini? Ni kwa sababu, “MUNGU UYAUMBA MATUNDA YA MIDOMO YETU” (Isaya 57:19) na sote tunajua kinachozaliwa toka mdomoni [matunda] ni MANENO YETU…Na Mungu anasema anayaumba tu, bila kujali ni mema au mabaya, kwanini? Kwa sababu ameshalisema hilo katika NENO LAKE, HAWEZI KULIBATILISHA NENO LAKE...ANALIANGALIA APATE KULITIMIZA (Yer 1:10-12)

KWANINI MANENO YAKO YANA NGUVU?

1.UMEUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU (Mwanzo 1:26)
Mungu amekuumba wewe kwa sura na mfano wake, na alivyo Yeye ndivyo wewe ulivyo Ulimwenguni humu (1Yoh 4:17)
Aliumba vyote kwa NENO…Alisema na ikawa…na ameweka uwezo na asili yake hiyo ndani yako…ujue ama usijue haitabadili utendaji wa KANUNI HII YA UUMBAJI!

2.WEWE NI MUUNGU, MWANA WA ALIYE JUU (Zaburi 82:6)

Ulipompokea Yesu kuwa BWANA na mwokozi wa Maisha yako ulipewa uwezo wa kuwa mwana wa Mungu (Yoh 1:12) na ili kukupa udhibitisho na uhakika, Mungu amekupa ROHO WAKE MATAKATIFU anayeshuhudia na roho yako ya kuwa wewe ni mwana wa Mungu(Warumi 8:16) na kama mtoto wa nyoka alivyo nyoka, na hata mtoto wa Mungu ni Muungu…sisi ndio watawala na wamilki wa dunia hii (Ufunuo 5:8-11) ila lazima tubadili mambo kwenye ulimwengu wa roho kwanza…kwa MANENO YETU YA USHINDI NA IMANI…TUKISHIKA SANA MAUNGAMO YETU MEMA, NA YA MEMA (Waebrania 4:14)
Aliye DHAIFU na aseme nina nguvu, aliye tasa na aseme ninao watoto wengi, aliye mgonjwa na aseme Yesu amelipia Afya yangu pale Kalvari, aliye masikini na aseme Mungu wangu atanijaza yote ninayo yahitaji kwa kadri ya utajiri wake katika utukufu katika Kristo Yesu, aliye katika kufa na aseme Sitakufa bali nitaishi nami nitayasimulia matendo makuu ya Mungu wangu!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “UMEUWEZA ULIMI WAKO AU UMEKUWEZA?
  1. John Kifaru says:

    Somo zuri sana ahsante na Ubarikiwe.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: