YESU NI NANI??

Usipojua cheo na hadhi sahihi ya huyu Yesu aliye hai, hautakuwa na kiwangoi cha umakini na nidhamu ya kutosha kwake, na leo ninataka ujue kwa neema ya Mungu, kupitia Neno la Mungu, Yesu ni nani?

yesu ni nani

1.Yesu ni Emmanuel…Ni Mungu mzima mzima, aliyeziumba mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, akiwa katika hali ya MWILI WA KIBINADAMU (Mathayo 1:23)

2.Yesu Kristo ni Mungu mkuu (Soma Tito 2:13)

3.Yesu Kristo ni BWANA na Kristo (Matendo 2:36)
Na kama ni BWANA, maana yake ni Mungu…maana jina hili BWANA, ni la Mungu aliye hai peke yake…na lilitumika sana kwenye agano la kale!

4.Yesu ni Neno la Mungu katika Mwili (Yohana 1:14)
ila ni muhimu ukumbuke ya kuwa Neno lilikuwepo toka mwanzo kabisa, na ndilo lililoumba vyote, na pasipo Neno hakikufanyika chochote, na Huyu Neno alikuwako kwa Mungu na Neno alikuwa Mungu (Yohana 1:1-3) Na ndo huyu huyu alifanyika mwili akaja kwetu tukauona utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa Neema na Kweli!

5.Alipofufuka na kuingia ndani ya nyumba waliyokuwemo Mitume wamejifungia kule Yerusalemu, na kumwambia Thomaso, weka vidole vyako kwenye mikono, miguu na mbavu zangu ili ujionee ya kuwa ni mimi…Thomaso alipata Ufunuo wa Kiungu kuhusu Yesu na akasema, “WEWE NI MUNGU WANGU NA BWANA WANGU” kisha Yesu akamwambia” WEWE UMESADIKI KWA SABABU UMEONA…HERI YAO WANAOAMINI PASIPO KUONA” (Hii habari iko katika sura za mwishoni za Injili ya Luka, unaweza kuitafuta na kusoma na kujipatia Ukweli)

KUANZIA LEO, USIMCHUKULIE YESU POA, YEYE NI MUNGU MKUU…KABLA IBRAHIMU HAJAWEPO, MIMI NIKO…hii ni kauli yake kwa wale wayahudi kwenye Injili ya Yohana sura ya 8…Na kama alikuwepo kabla ya Ibrahimu, WASOMAJI WA BIBLIA MNALOJIBU!

Huyu ndiye Yesu, mwenye Mamlaka yote Mbinguni na duniani (Mathayo 28:18)

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: