FAHAMU UWEZA NA NGUVU YA MSALABA…(Part 2)

Bwana Yesu asifiwe sana, wiki iliyopita tulipitia mambo 6 ambayo yametokea pale msalabani na ambayo ni mali yetu na haki yetu ndani ya Kristo Yesu…Leo tunaendelea na mambo mengine 3 ambayo Msalaba wa Yesu umetenda kwa ajili yetu, karibu na Roho wa Mungu akupe neema ya kupata kitu cha kukusogeza hatua kadhaa katika kumjua Yeye na Kristo Yesu aliyemtuma

7.ALISHUGHULIKIA SWALA LA MASHITAKA YA SHETANI DHIDI YETU (Wakolosai 2:13-14)

Biblia inaeleza kwa uwazi ya kuwa Kristo Yesu alitufufua na kutuweka hai pamoja naye, akatusamehe dhambi na makosa yetu, kisha AKAIONDOA HATI YA MASHITAKA iliyokuwa ikileta uadui kati yetu na Mungu…Unajua dhambi na makosa yetu hutufarakanisha na Mungu na kuweka uadui kati yetu na Yeye, ila shetani ndiye afanyaye kazi ya kukusanya kila kosa, na dhambi zetu na kuziwasilisha mbele ya Mungu ili kutushtaki…Biblia inasema “ANATUSHITAKI MCHANA NA USIKU” (Ufunuo 12:11)…Lakini ushukuriwe msalaba, na kazi njema ya Yesu aliyoitenda kwa DAMU YAKE YA THAMANI aliifuta hati ya mashitaka, mara moja na milele, kila shetani akikuletea hukumu moyoni mwako, Mkumbushe ukweli huu, mwambie DAMU YA YESU IMENITENGA MBALI NA HUKUMU, SIKO KATIKA HUKUMU, NIMEVUKA TOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI, HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YANGU NDANI YA KRISTO YESU…Mkumbushe shetani mara kwa mara juu ya kile ambacho DAMU YA YESU ILIFANYA PALE MSALABANI…
Kumbuka: TUNAMSHINDA SHETANI KWA DAMU YA MWANAKONDOO NA KWA NENO LA USHUHUDA WETU…SI KWA MACHOZI AU VILIO!

8.MAMLAKA YA UFUNGUO WA JINA LA YESU (Wafilipi 2:5-11)

“…Kristo Yesu alikuwa mtii, akajinyenyekeza hata mauti ya MSALABA…Na alipomaliza kutii na kunyenyekea na kwenda msalabani, Mungu aliye hai ALIMKIRIMIA JINA KUU LIPITALO MAJINA YOTE…ILI KWA JINA LA YESU; VITU VYOTE VYA MBINGUNI, DUNIANI NA CHINI YA DUNIA(KUZIMU)…Ndio maana alipofufuka na kukutana na wanafunzi wake aliwaambia “NIMEPEWA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI” (Mathayo 28:18)…Ili Jina la Yesu liwe na utendaji mkubwa kwako, lazima ujue uhusiano wake na MSALABA…
UNAWEZA KUPATA MENGI KUHUSU JINA LA YESU KATIKA KITABU CHANGU KIITWACHO; FAHAMU UWEZA NA NGUVU YA JINA LA YESU, JINA 1 FUNGUO 3 TOFAUTI

9.UFUNGUO WA DAMU YA YESU (Waefeso 1:7, Ufunuo 1:4-5, 1Yohana 1:6, 1Petro 1:18-19, Ufunuo 5:8-11)

Msalabani, Yesu alimwaga damu yake ya thamani, toka mikononi, miguuni, ubavuni na mgongoni kwa mijeledi aliyopigwa…na katika DAMU YA YESU umekaa ushindi na ukamilisho wa Mkristo!
Mistari iliyopo hapo juu imebeba baadhi tu kati ya kazi nyingi za DAMU YA THAMANI YA YESU…Ipitie na upate maarifa ya kukusaidia kuwa bora katika maisha yako ya kiroho, kimwili na maisha kwa ujumla!MUNGU AKUBARIKI NA TUTAENDELEA TENA NA SEHEMU YA TATU YA SOMO HILI WAKATI MWINGINE…KUMBUKA NI MUHIMU PIA KWA WEWE KUNIOMBEA, MAANA NIKISTAWI NAWE UTAPATA SEHEMU YAKO KILA WAKATI…KAMA NIKIKWAMA, HATA WEWE HAUTAPOKEA HIKI UKIPATACHO…AMEN!
Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “FAHAMU UWEZA NA NGUVU YA MSALABA…(Part 2)

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: