HAUJARIBIWI WEWE ILA IMANI YAKO…

Mara nyingi changamoto ziitwazo Majaribu zikiwajia wana wa Ufalme wa Mungu, huwa wanachanganyikiwa, na wengine wanapoteza mwelekeo kabisa, na hata wengine wanamlaumu Mungu kwa kuruhusu hilo litokee kwao…Jaribu ni changamoto yoyote ile inayokufikisha njia ya panda ya kuendelea kumwamini Mungu na Neno lake au la…Si kila changamoto unayopitia ni jaribu, ila Jar

ibu si jaribu mpaka likufikishe mahali pa njia panda pa kuhoji UWEZA, NGUVU, UPENDO na UBABA wa Mungu kwako na UHAKIKA WA NENO LAKE MAISHANI MWAKO!

Jaribu haliji kwako kwa sababu ni swala la kawaida tu, jaribu linakuja kwako kwa sababu kuna kivutio kinachovutia majaribu ulichonacho…Kivutio hicho cha majaribu ni tishio kwa Shetani, Ufalme wake, Dunia, Dhambi na kila changamoto yako. Kivutio hiki kinaitwa IMANI!

imani,kuza imani
JARIBU HUIJARIBU IMANI YAKO NA SI WEWE

Lengo kubwa la jaribu lolote linalokuja kwako si kukujaribu wewe, bali ni kuijaribu Imani yako uliyonayo…Mtu mwenye kiwango kikubwa cha Imani na majaribu yake pia ni makubwa…Mwenye Imani ndogo pia majaribu yake ni ya kawaida ambayo kwa mtu wa Imani kubwa anabaki kushangaa ukimwambia kwamba hilo kwako ni jaribu!
Biblia imeweka wazi ya kuwa kinachojaribiwa au kufuatwa ili kitikiswe na jaribu si wewe, bali Imani yako iliyomo ndani yako…”Basi hesabuni ya kuwa ni furaha mnapoangukia majaribuni(japo majaribu hayana radha yoyote ya utamu) maana KUJARIBIWA KWA IMANI YENU huleta saburi” (Yakobo 1:2-3)
Kwa hiyo jaribu lolote linalokuja kwako, liko ndani ya kiwango cha Imani yako, na halijajajjjjjjj kwako bali limeifuata Imani yako, ila kwa sababu Imani yako imo ndani yako na inadhihirishwa na wewe ndio maana ule mchuano kati ya IMANI YAKO na JARIBU unakugusa wewe na hata kukuathiri kwa namna moja ama nyingine

KWANINI MAJARIBU YANAIFUATA IMANI YAKO ILI KUIJARIBU?

Ziko sababu kadha wa kadha ni kwanini majaribu yanapenda kuja kushikana mieleka na Imani yako, au kuijaribu imani yako, baadhi yake ni hizi zifuatazo;

1.IMANI INAWEZA KUHAMISHA MILIMA (Marko 11:23, 1Kor 13:2-3)

Kila mlima au changamoto uliyonayo, au inayoweza kutokea mbele yako inaweza kuondoshwa na silaha moja kuu na ya pekee iitwayo IMANI. Milima haiondoki kwa machozi wala kwa vilio au hata maombi au dua ama sala…IMANI INANG’OA MILIMA…Ndio maana shetani kwa kupitia majaribu anajitahidi kushambulia IMANI YAKO…SILAHA YAKO PEKEE YA KUHAMISHA MILIMA YAKO YOTE!

2.IMANI NI KIUNGANISHI KATI YAKO NA MUNGU (Waebrania 11:6)

Shetani anajua ya kuwa huwezi kuendesha maisha yako NJE YA UWEPO WA MUNGU. Anajua akifanikiwa kukutoa kwenye UWEPO WA MUNGU, ni sawa na KUMTOA SAMAKI MAJINI…Kwa kulijua hili, Yesu alisisitiza tulisome NENO LA MUNGU SANA, kiasi cha kulifanya kuwa sehemu ya maisha yetu, kuwa sehemu ya kila mazungumzo na mawazo yetu yote…Yaani tukae NDANI YAKE NA NENO LAKE LIKAE NDANI YETU(Yohana 15:7)…Likikaa linaibua IMANI, ambayo chanzo chake ni kusikia NENO LA KRISTO (War 10:17) na kwa kulijaza Neno litakaloibua Imani ndani yetu, TUNAJUA UWEZO WA MUNGU, Hivyo hatupotei!

3.IMANI YAKO INAUSHINDA ULIMWENGU (1Yohana 5:1-4)

Yesu alipokuwa hapa duniani, alikuwa mshindi katika maeneo yote, hakuwa na waa wala doa kokote, na kwa ujasiri aliwaambia wanafunzi wake, “MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU” Lakini hakuishia hapo bali aliwaambia wanafunzi ya kuwa Ulimwenguni humu tunayo dhiki na mateso na changamoto za kila namna maana sisi wa ULIMWENGU HUU (Yohana 17:13-15)
Ila hakutuacha yatima bali alitupatia MSAIDIZI, ROHO MTAKATIFU, AMBAYE NDIYE ROHO YULE YULE WA IMANI ALIYEKUWA NDANI YA KRISTO YESU….Ndio maana kwa ujasiri mkuu na wa ajabu, mtu wa Mungu, mtume Yohana anasema, “KILA KILICHOZALIWA NA MUNGU HUUSHINDA ULIMWENGU….NA HUKU NDIKO KUSHINDA KUUSHINDAKO ULIMWENGU, YAANI HIYO IMANI YETU”
Kwahiyo basi, Mkuu wa ulimwengu huu, na mungu wa dunia hii anajua siri ya nini kinaweza kukufanya umweke chini ya miguu yako, hivyo hakushambulii wewe bali hiyo silaha ya maangamizi uliyonayo iitwayo IMANI. Na anaishambulia kupitia changamoto tata kwako ziitwazo MAJARIBU!

4.IMANI NI ULINZI KWAKO (1 Petro 1:5)

Imani ni ulinzi kwako, inamzuia shetani, mapepo, wachawi, waganga na mawakala wote wa kuzimu wasikushambulie wala kukudhuru…IMANI ni ngao inayozima mishale yote ya moto ya yule adui shetani na majeshi yake ya pepo wabaya (Waefeso 6:10-18)…Mtume Petro alipopata ufunuo huu wa Ulinzi wa Mungu kusababishwa na kiwango cha Imani ulichonacho, aliamua kuandika kauli hii, “KWA MAANA TUNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU KWA NJIA YA IMANI…”

5.IMANI INAMFANYA MWENYE NAYO APATE KILA ATAKACHO NA INAFANYA YOTE YAWEZEKANE KWA MWENYE NAYO (Marko 9:23, Marko 11:23-24)

Shetana anajua kuwa ukiamua kuenenda kwa IMANI na wala si kwa kuona (2Kor 5:7) utapata kila utakacho hapa duniani…Nasema shetani anajua kuwa usipokuwa na mashaka wala wasiwasi na ahadi za Mungu UTAPATA KILA UKITAKACHO haijalishi itachukua muda gani kukiona katika macho ya nyama na kukigusa kwa mikono, ila UKIAMINI SIKU ZOTE, UTAUONA UTUKUFU WA MUNGU!
Shetani anajua siri hii, ndiyo maana anakutia uvivu usiende kanisani kwenye Mafundisho ya Neno la Mungu maana utasikia Neno la Kristo ambalo litaileta na kuiinua Imani yako…Atakuruhusu uangalie movie masaa kadhaa, atakuruhusu uwe online facebook masaa kadhaa, atakuruhusu uwe busy na kuchat kwa meseji lakini hatakuruhusu Usome Biblia na Vitabu vya kiroho vinavyoijenga Imani yako na kukufanya uwe mshindi…akikuona unakazana kujikwamua, ataleta majaribu ili yaishambulie Imani yako…ila usichoke wala kukubali kushindwa, ILISHE ROHO YAKO, ILISHE IMANI YAKO, SIKILIZA NA HUDHURIA MAFUNDISHO, SOMA NENO LA MUNGU KWA BIDII, HUDHURIA SEMINA ZA MAFUNDISHO nk na kwa kufanya hivyo utapandisha Imani na kuwa mshindi na zaidi ya mshindi (War 8:37)
Kumbuka: YOTE YAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE! MTU WA IMANI HASHINDWI KAMWE, YOTE YAKO NDANI YA UWEZO WAKE! HUONA NJIA PALE WENGINE WASIPOONA! HUONA MWANGA NA NURU WENGINE WAONAPO GIZA! HUONA UZIMA WENGINE WOTE WAONAPO MAUTI! HUONA UHAI PALE WENGINE WOTE WAONAPO KIFO! HUONA KUSTAWI NA KUCHANUA MAHALI AMBAPO WENGINE WANAHAMA KWA KUSHINDWA!
Mimi ni mtu wa Imani, Imani yangu imemshinda shetani, imeyashinda mapepo, imeushinda umasikini, imeushinda ujinga, imeshinda kifo cha mapema, imeshinda kuishi kama watu wengine, imeshinda u-kawaida na kunivika ukuu na uweza, imenipa kustawi kila iitwapo leo!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “HAUJARIBIWI WEWE ILA IMANI YAKO…
  1. Frank says:

    Ubarikiwe sana!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: