TOFAUTI YA KUSADIKI NA KUAMINI (DIFFERENT BETWEEN BELIEF AND FAITH)

Wakristo wengi wanazijua ahadi nyingi za Mungu zilizo kwenye Neno la Mungu, na hata kuzikiri kwa kinywa na kuziamini kwa moyo lakini bado maisha yao hayana PAMBAZUKO wala KUCHANUA…Si kwa sababu Neno la Mungu si kweli au limepungua nguvu zake na uweza wake, la hasha! ila kuna mambo kadhaa wanayachanganya…Mahali pa kuamini wao

wanasadiki na mahali pa kusadiki wao wanaamini…kwa mfumo huu haitawezekana kupata kitu kwa Mungu, maana Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, siku zote anatenda kazi kwa yule aliyefanya maelekezo yote kwa usahihi na si nje ya hapo!

NINI MAANA YA KUSADIKI(BELIEVING)?

Kusadiki ni kuamini jambo au kitu ulichosikia moyoni mwako japo hujakiona wala kukigusa, na kisha unasubiri kijidhihirishe kwako.
Kusadiki huja pale Mungu au mtu anapokupa ahadi ya kukupatia kitu fulani ndani ya muda fulani ambapo wewe hauhitajiki kufanya chochote ili kupata kitu hicho ulichoahidiwa!

MFANO WA MARIAMU NA MIMBA YA YESU;

Mariamu alipoambiwa na Mungu ya kuwa atapata mtoto wa kiume, bila kukutana na mwanaume, tena akiwa bikra, kwa hali ya kawaida haikuwa inaingia akilini wala kupokelewa na fahamu zake…lakini alipopata uhakika na udhibitisho wa hilo, wala hakuendelea kusumbuka, maana jambo lenyewe halikuitaji yeye kushiriki kwa namna yoyote, ilikuwa ni Mungu mwenyewe kazini, yeye alihitajika tu kukubali ile kazi…ALIPOSADIKI MOYONI MWAKE ya kuwa Mungu anaweza kulitenda hilo, IKAWA KWAKE SAWA NA IMANI YAKE ILIYOKO MOYONI, BILA YEYE KUFANYA LOLOTE JUU YA KUTUNGA KWA MIMBA HIYO!

NINI MAANA YA IMANI(FAITH)?

Imani ni kile kitendo cha kuamini moyoni mwako maelekezo ya Mungu, na kisha kuyaweka kwenye matendo. Kwa lugha ya kimahesabu, IMANI= KUSADIKI+MATENDO
Na Imani inahusisha matendo juu ya ile ahadi ya Mungu kwako. Unayachukua maelekezo ya Mungu kwako, na unayatenda kama yalivyoletwa kwako bila kwenda kulia wala kushoto, bila kuarifu neno mojawapo kati ya hayo!

MFANO WA MAOMBI YETU KWA MUNGU

Mungu ametupa mwaliko wa kuja mbele zake kuomba na kama tukiomba kwa Imani pasipo shaka, yeye anatupa yale tumwombayo. LAKINI kama mtu ataishia kusema, “MIMI NAAMINI NIKIOMBA HIKI AMA KILE KWA BWANA NITAKIPATA” Halafu mtu huyu akaishia hapo bila kuchukua hatua ya kwenda kuomba (kitendo cha kudhibitisha Imani yake) uwe na uhakika hatakipata kile akitakacho japo Mungu ni yuleyule aliye ahidi na uaminifu na wema wake haujabadilika hata sasa…shida si kwamba huyu mtu hajui Neno la Mungu, anajua na ni NENO lililompa uhakika wa kupata ila hatapata kwasababu ameiruka kanuni…hajaweka kwenye matendo ile Imani yake, ameishia KUSADIKI mahali ambapo panahitaji IMANI…Hajaweka kwenye matendo!

MFANO WA MWANAMKE ALIYETOKWA NA DAMU (Mark 5:28-34)

Huyu mama alipata KUSADIKI baada ya kuwa amesikia habari za Yesu na matendo yake kwa wengine…alisikia habari za Yesu, moyoni mwake akapata IMANI, na ikampa kuona kitu cha tofauti ambacho wengine wote hawakuwa wakiona…akaenda akajipenyeza akaligusa pindo la vazi la Yesu, AKAPONYWA!
Kama huyu mama angeishia KUSADIKI, na akasema tu kwa mdomo wake, lakini akawa hajachukua hatua ya kuligusa pindo la vazi la Yesu, uwe na uhakika tusingekuwa na MUUJIZA HUU KWENYE BIBLIA ZETU!

MFANO WA BALTIMAYO KIPOFU

Tunamjua ombaomba maarufu wa kwenye Biblia ambaye Yesu alimponya tatizo lake la Upofu. Mtu huyu aitwaye Baltimayo alikuwa AKISADIKI moyoni mwake ya kuwa Yesu mwana wa Daudi anayewaponya vipofu wengine anaweza kumponya na yeye pia…lakini hakuishia hapo tu…alifanya sehemu yake, ALITENDA, ALIWEKA IMANI KWENYE MATENDO, Hakukubali kukaa kimya, alifanya kitu, alipiga kelele, “MWANA WA DAUDI UNIREHEMU”
Kama angeishia kuamini moyoni tu, bila kutenda na kufanya sehemu yake, asingelipata muujiza wake!

MUHIMU SANA

Kwenye Biblia kuna baadhi ya ahadi zinahitaji wewe KUSADIKI tu moyoni mwako halafu Mungu anafanya hilo kwako moja kwa moja (automatically) lakini ahadi nyingi sana zilizoko kwenye Neno la Mungu zinahitaji IMANI (USADIKI MOYONI KUHUSU HILO, KISHA UTENDE SAWA NA NENO LA MUNGU)…Unahitaji kujua hili ili uwe na utele na ustawi Mungu aliokukusudia, usomapo Biblia yako na kuiona ahadi ya Mungu, ichunguze kwa Umakini, je ni ya KUSADIKI tu na kupokea au inahitaji pia na wewe KUTENDA?
Ukizingatia hili, baada ya muda mfupi utayapata yote uyatakayo na utakuwa vile ambavyo Neno la Mungu linasema kuhusu wewe!
NAKUTAKIA UFANISI KATIKA KUMJUA MUNGU…Amen!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: