SHETANI SI TISHIO, DHAMBI NDIO ADUI YAKO NAMBA MOJA…

Unajua Wakristo wanatumia muda wao mwingi kumshughulikia shetani, wana kila aina ya maneno na misemo ya kumwinua shetani kwenye maisha yao…KILE AMBACHO KIMEJAA MDOMONI MWAKO, NDICHO CHENYE NAFASI KUBWA KWAKO…NAFASI HIYO INAWEZA KUWA YA MEMA AU YA MABAYA!

Ila kwa Wakristo wengi, Shetani ni topic yao kubwa, wanatamka na kusimuliana jinsi A

LIVYOJIINUA, ALIVYOTAKA KUWAMALIZA, ALIVYOTAKA KUWAHARIBIA FAMILIA ZAO, ALIVYOHARIBU NDOA ZAO, ALIVYOHARIBU MAISHA YAO, BIASHARA ZAO nkHivyo wanatumia muda wao mwingi kupambana na shetani, wakisema wako vitani, wanakaa katika mapigano [kama wasemavyo] na pepo, wachawi na majini…Hii si mbaya, ni njema kabisa, ila inahitaji tu ujue namna ya kumdhibiti Shetani na timu yake, kisha uache kupoteza muda wako kwa kupambana naye kila siku!

Biblia inatueleza nini cha kufanya ili kila iitwapo leo tuwe washindi dhidi ya Shetani na Jeshi lake, si kwa kutoa jasho, si kwa kukauka sauti na makoo kwa kukemea, ni rahisi sana…Yafuatayo ni mambo ya Msingi ya kufanya ili Shetani awe chini ya miguu yako siku zote na katika maeneo yote:

1.KUWA ADUI WA DHAMBI

Dhambi ni kitu chochote kile mtu afanyacho, au asemacho, au awazacho, kilicho kinyume na NENO LA MUNGU…Yaani kilicho kinyume na MAPENZI YA MUNGU, YALIYO WAZI KATIKA NENO LAKE!
Adui mkubwa wa dhambi, atakayekusaidia uwe mshindi dhidi ya dhambi ya aina yoyote kwenye maisha yako ni NENO LA MUNGU. Kwani ndani ya NENO LA MUNGU utakuta MAELEKEZO, TARATIBU, SHERIA, AMRI na MFUMO WA MAISHA WA UFALME WA MBINGUNI ambao kama ukiuweka kwenye MATENDO, Dhambi inapoteza udhibiti na utawala kwako…Daudi anasema, “MOYONI MWANGU NIMELIWEKA NENO LAKO ILI NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI” (Zaburi 119:11)
Tunza utakatifu kwa gharama yoyote, UTAFUTE UTAKATIFU KWA GHARAMA ZOTE, NA PIA JITAHIDI KUWA NA AMANI NA WATU WOTE…Kuwa mwepesi wa kuomba msamaha ukikosea, na uwe mwepesi wa kusamehe wanaokukosea, hata kama hawataki hata kukusalimia au hata kukuona, hata kama wanataka hata kukuangamiza, usilipe baya kwa baya, ushinde ubaya kwa wema, hakikisha hakuna mtu aliyefungiwa moyoni mwako, ili shetani na mapepo wasije wakatumia hiyo fursa kukumaliza!

2.WEKA NENO LA MUNGU KWENYE MATENDO

Watu wachache sana ambao wanapitia BIBLIA zao walau dakika 5 au 10 kwa siku, na kati ya hao wachache ni watu wachache zaidi ambao wanapata UFUNUO kwenye yale MANENO YA UZIMA WAYASOMAYO, na kati ya hao wachache wapatao Ufunuo wa Neno la Mungu ni wachache zaidi WANAOTENDEA KAZI KILE AMBACHO MUNGU AMEWASEMESHA KWENYE NENO LAKE…Ndio maana Wakristo wengi wamejaa mistari mingi ya maandiko lakini hawana UFANISI KWENYE MAISHA…Andiko huua bali ROHO huuisha!
Yule anayelipata NENO LA MUNGU na KULITENDA anafananishwa na MTU MWENYE HEKIMA, IKIJA MVUA, MAFURIKO, GHARIKA NA DHORUBA ZA MAISHA; YEYE ANAENDELEA KUTHIBITIKA NA KUSTAWI WAKATI WENGINE WOTE WANALIA!3.DUMISHA USHIRIKA NA MUNGU

Mungu amekupa uhakika, ufuatao:

 • -Yeye ni Mungu aliye karibu wala hayuko mbali
 • -Amekupa mwaliko wa kumtafuta maadamu anapatikana
 • -Mungu hana upendeleo, hana watu maalum tu wa kumsogelea na kuzijua siri zake, kinachotutofautisha ni BIDII YA KUMTAFUTA
 • -Amekuhakikishia ukimwita atakuitikia
 • -Amekuhakikishia atakuwa Mungu wako nawe utakuwa mwanae wa kiume na wa kike
 • -Amekuhakikishia HATAKUACHA WALA KUKUPUNGUKIA
 • -Amekuhakikishia hata HESABU YA NYWELE ZAKO ANAIJUA…Kama anaweza kutenga muda wa kuhesabu nywele zako, atakosa muda wa kuzungmza na wewe ukimwendea kwa lengo la kuongea naye?
 • -Amekuhakikishia msaada wakati wote
 • -Amekuchora kwenye viganja vyake
 • -Akugusaye anaigusa mboni ya jicho lake

Mimi nakushauri, kati ya masaa yako 24, hakikisha una muda wa kuwa mbele za Mungu walau mara 3 kwa siku…
Unaweza kuniambia muda haunitoshi, majukumu ya ofisi, familia, mke/mme nk lakini nataka ujue hili; DANIEL ALIKUWA WAZIRI MKUU WA BABELI [KIONGOZI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI WA BABELI] LAKINI ALIKUWA AKIKAA MBELE ZA MUNGU MARA 3 KWA SIKU KAMA DOZI!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
7 comments on “SHETANI SI TISHIO, DHAMBI NDIO ADUI YAKO NAMBA MOJA…
 1. John Matiku says:

  Mungu aibariki huduma yako na azidi kukuinua! Namshukuru Mungu kwa ajili yako kupata Mwal. mzuri! maana namwona Mungu katika masomo haya!!

 2. paulo yakobo says:

  Mungu akubari kwa kutujuza adui yetu mkubwa kuwa ni dhambi

 3. Nalysis Kaiza says:

  Be blessed

 4. Michael mgalla says:

  Hakika nimebarikiwa na mafundisho yako nashukuru kwa kuweka wazi namna inavyositahiri kuishi katka UTAKATIFU WA MUNGU na kutenda mema kila uitwapo leo hata milele, binafsi najivunia kupata ujumbe huu hakika umenipa nguvu,maarifa na hatimaye nimetoka sehemu moja na kwenda nyingine.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: