YATAKAYOKUWAKO YAMEKWISHA KUWAKO…

Ni muhimu ujue jambo hili wewe ambaye Yesu ni Bwana na Mwokozi wako, na wewe ambaye Mungu ni Baba yako kupitia kwa Kristo Yesu!
Kila utakalo kwa ajili ya Maisha yako ya kila siku na kwa ajili ya utauwa, vyote umeshatengenezewa hata kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa…Ndio maana Biblia haisemi tutabarikiwa, bali inasema, “ATUKUZWE BABA MUNGU, BABA WA BWANA W

ETU YESU KRISTO ALIYETUBARIKI KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI”
Unaweza kuniambia “Lakini Mwalimu, si ni za rohoni na hajasema za mwilini?” Jibu langu kwako ni hapana, anaposema za ROHONI anazungumza kwa lugha ya kiungu (divine language) akitaka kuweka msisitizo kuwa kila kinachoonekana hapa duniani kina msingi wake kwenye ULIMWENGU WA ROHO…Kwa sababu VITU VILIVYO DHAHIRI[Vinavyoonekana] vimetokana na VITU VISIVYO DHAHIRI[visivyoonekana]…
Mungu amekupa NAFASI YA KUAMUA KIASI CHA KIWANGO GANI CHA MAISHA UNATAKA UISHI UKIWA HAPA DUNIANI…KIWANGO CHAKO CHA MAISHA HAKIWEZI KUWA ZAIDI YA VILE UNAVYOJIONA NAFSINI MWAKO NA KUKIRI MBELE ZA WATU KILA SIKU BILA KUJALI UNA NINI MKONONI, UNAMILKI NINI AU UNA KIWANGO GANI KINACHOONEKANA KWA MACHO NA KUSHIKIKA KWA MIKONO…Kwa kuwa, “AJIONAVYO MTU NAFSINI MWAKE; NDIVYO ALIVYO”
Usije kufanya kosa la kuyatafsiri, au kuyaamua maisha yako kwa kile ulichonacho au hali yako ya maisha ya sasa…Thamani ya mtu haiko kwenye kile alichonacho bali katika KILE AWEZACHO KUFANYA…Kwangu ni bora kuwa na rafiki MASIKINI MWENYE HEKIMA NA MAWAZO YASIYODHIBITIWA AU KUTATIZWA NA KILE ANACHOKIONA, AU KUKIPITIA KWENYE MAISHA kuliko kuwa rafiki wa TAJIRI MKUBWA ASIYEWEZA KUONA TENA MBALI, NA ANAYELIA KILA APATAPO CHANGAMOTO AU SHIDA!
Kila kitu ambacho unakitaka kwenye maisha yako, kipo tayari, kiko hatua chache kutoka hapo ulipo, usipojua hilo utakula kila makombo, na mataputapu yanayokuja mbele zako!
Mungu aliye hai, Baba yako, ametangaza mwisho wako tangu mwanzo wako (Isaya 46:9-10)
Alikujua hata kabla ya mimba yako haijatungwa tumboni kwa mama yako (Yeremia 1:4-5)
Mimba yako ilitungwa kwanza kwenye mawazo ya Mungu kabla ya kutungwa kwenye tumbo la mama yako, wala kabla haujawekwa kwenye viuno vya baba yako…Mwamini Mungu, Anakuwazia mawazo mema na ya amani, kukupa tumaini kwenye siku zako zijazo (Yeremia 29:11)
MWAMINI MUNGU, MWACHE ATENGENEZE KESHO YAKO!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: