KUWENI MAKINI NA HUYU MTU ANAYETUMIKA NJE YA UFALME WA MUNGU [ASOMAYE NA AFAHAMU

Kati ya watumishi wa Mungu ambao hawana muda wa kuwazungumzia au kuwafuatilia watumishi wengine ni mimi Mwl Dickson Cornel Kabigumila…ndani yangu kuna mfumo wa kusimamia na kujenga Ufalme wa Mungu, sipendi hata kidogo kuona mtumishi fulani anasimama mahali na kumsema mwenzie au kumpinga. Lakini kwa mara ya kwanza nadhani na ya mwisho [labda], nasimama hapa kuwaletea tahadhari kuhusiana na ndugu mmoja hapa Jijini Dar es Salaam, ambaye kwa nje ana MFANO WA UTAUWA LAKINI YUKO NJE YA KRISTO NA ANATUMIKIA SERIKALI YA KUZIMU…Sitamtaja jina ila nitawapa baadhi ya vitu vitakavyowasaidia kutafakari na kumfahamu na kuchukua hatua ya kumwepuka na kuwasaidia wale ambao tayari walishanaswa naye…

image

na mwenye masikio

KUHUSU MTU HUYU ASIYEKUWA WA KRISTO JAPO ANAFANYA KWA MFANO WA KRISTO…

1.Ni mtu wa majigambo sana, kuhusu NGUVU, UWEZA na MIUJIZA…Hata kufikia hatua ya kusema baada ya miaka kadhaa atakuwa ASKOFU wa watu wote wa Dar na Tanzania.

2.Ni mtu wa Maneno yasiyokolea munyu, hekima ni haba au sifuri kabisa kwenye eneo la matamshi…aliwahi kuingia kwenye ligi na mamlaka fulani na akasema ikitokea kama walivyosema [walivyotabiri] basi yeye ataacha kutumika madhabahu

ni na KWENDA KUUZA BANGI

3.Ni mtu wa kupinga mafundisho ya Kibiblia ambayo watumishi wa Mungu wanayatoa madhabahuni sehemu, kisha yeye huandaa somo au kutoa tamko akipinga kile kilichofundishwa, tena mara nyingi hata bila udhibitisho wa kimaandiko…
Mfn: Miaka kadhaa aliwahi kusimama na kurumbana na mtumishi mwingine kuhusiana na maswala ya MAVAZI na ilichukua muda kweli kwenye televisheni mpaka nilipomtumia ujumbe wa simu na kumkemea juu ya hilo, akawa ameacha kurusha majibizano yale!
Pia kuna wakati fulani Mtumishi mwingine wa Mungu aliwahi kwenda Tabora na kufundisha juu ya swala la Uhusiano wa Uchumi na Ardhi na akaeleza jinsi mkoa huo usivyopiga hatua kwa sababu ya Kilimo cha tumbaku na ya kuwa Ardhi haizai kwa sababu ya zao hilo na kuwahimiza wenyeji wa mkoa huo kufanya TOBA KWA AJILI YA ARDHI…Lakini huyu ndugu naye alipokwenda mkoa ule, akawahimiza wananchi Walime tumbaku kwa wingi na akapinga kila alichosema mtumishi aliyetangulia….
Na kuna wakati mmoja mtumishi mwingine wa Mungu hapa jijini Dar aliwahi kufundisha juu ya UMUHIMU WA MAOMBI KWA MKRISTO lakini huyu ndugu akaandaa somo kupinga umuhimu wa maombi…

4. Ni mtu wa kupenda pesa…kitu ambacho ni kinyume na huduma za utumishi wa Ufalme wa Mungu [asomaye na afahamu]

KUHUSU HUDUMA YAKE:

1.Kanisani kwake hakuna swala la KUOKOKA WALA WOKOVU…Watu wa madhehebu yote wanaruhusiwa kuja kupata miujiza yao na kuendelea kusali pale tu hata kama watakuwa hawajampa YESU MAISHA YAO…[Hakuna huduma yenye msingi kwa Yesu isiyohusisha Wokovu na watu kusamehewa dhambi]

2.Kanisani kwake hakuna MADARASA YA KUFUNDISHA NENO LA MUNGU, WALA MADARASA YA KUUKULIA WOKOVU…kwake kuna siku mbili za ibada…Alhamisi ni siku ya MAOMBEZI na Jumapili ni siku ya IBADA YA JUMLA.

3.Hakubaliani na huduma kadhaa kati ya 5 zinazoujenga na kuukamilisha mwili wa Kristo…anasema hakuna MANABII WALA MITUME SASA…anakubali juu ya uwepo wa Wainjilisti, Wachungaji na Walimu…Kwa hili nadhani hata msingi alioupata wakati akiwa chini ya DHEHEBU FULANI KONGWE kabla ya kujitenga ni sababu pia ya msimamo huu…Lakini kibaya zaidi ni kuinuka na kutupa maneno ya kejeli, vijembe na matusi kwa hao MITUME NA MANABII…Hii si hekima ya mtu ambaye ROHO WA MUNGU ANAKIMILKI KINYWA CHAKE!

4.Kwenye huduma zake hakuna huduma ya kuwafungua waliofungwa na kuwaacha huru waliosetwa…Hata mara moja hakuna UTOAJI WA PEPO japo amewahi kufundisha kuhusu AINA ZA MAJINI kitu ambacho hakina maana kwa mtumishi wa AGANO JIPYA

5.Kwenye huduma yake hakuna UTENDAJI WA KARAMA NA VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU…Hakuna neno la maarifa, neno la hekima, karama ya unabii, kupambanua roho nk…Si mtu wa kumtukuza ROHO MTAKATIFU NA KAZI YAKE DUNIANI

6.Ni ngumu sana na mara chache sana kumsikia akilitumia JINA LA YESU KWENYE MAOMBEZI YAKE

7.Mafundisho anayotoa siku ya ibada ya jumapili, hayana msingi wa Neno la Mungu, ni hotuba tupu, ni maneno ya kushawishi akili yenye hekima ya kibinadamu ndani…Ni mara chache sana kwa yeye kufungua Biblia na kusoma Neno na kufundisha, yeye anasema Biblia iko kichwani!

8.Hakuna mafundisho kuhusu ROHO MTAKATIFU, KARAMA ZAKE NA VIPAWA na hata SWALA LA KUNENA KWA LUGHA MPYA HALIKO KWENYE HUDUMA YAKE, Japo anasema yeye ni Mpetekoste [mtu anayeamini juu ya kile Mungu alichofanya siku ya Pentekoste]

Niliamua kufanya uchunguzi wa haya yote baada ya kuwa nimembana PEPO MMOJA ambaye alieleza kila kitu kuhusu huyu ndugu na huduma yake ambayo inaendelea kukusanya mamia ya watu jijini Dar es Salaam…lengo la ujumbe huu ni kuwasaidia Wakristo wengine pia kuchukua tahadhari na kuwasaidia wengine waliokwishanaswa huko ili watoke…SHARE UJUMBE HUU KWA WINGI UWEZAVYO…SIKU ZOTE GIZA ALITAWEZA KUJIFICHA KATIKATI YA NURU!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: