SABABU HALISI YA MAKANISA KUCHOMWA TANZANIA

image

Ni watu wachache sana waliookoka Tanzania wanaojua kwamba hili swala la uchomaji wa makanisa lina mzizi wake KUZIMU na hawa WANA UAMSHO wametumiwa tu na haya Mapepo na Wakuu wa Giza wa Tanzania!

Hili jambo Mungu alinidokeza muda mrefu na kama mna kumbukumbu nzuri niliandika status yenye kichwa “USIWANYOOSHEE WAISLAMU KIDOLE CHAKO KWA YALE YANAYOTOKEA TANZANIA” Na katika status ile niliwahimiza waombaji wakazane KULENGA SHABAHA, WASISHUGHULIKE NA WALE AMBAO SI MIZIZI…YAANI WAACHE KU-CONCENTRATE NA WACHOMA MAKANISA AMBAO NI MATAWI TU, BALI WASHUGHULIKE NA NGUVU ZA KUZIMU ZINAZOJARIBU KUPIGANA NA KANISA [WATU WACHACHE WALIOO

KOKA NA WANAKAA KWENYE NAFASI ZAO KUHAKIKISHA CHA MUNGU TU KINAPITA KWENYE TAIFA HILI NA SI VINGINEVYO]..!

Jana nilikuwa namsaidia dada mmoja alikuja akiwa na shida ya kichwa kuuma, kifua na pia mashambulizi ya adui kupitia ndoto maana alikuwa anaota ANAKULA NYAMA KWENYE NDOTO!
Wakati nimemwita Yesu na kuanza kuziitia nguvu za Mungu na uweza wake, yule dada alianza kutapika mfululizo…wakati anaendelea kutapika pale, Bwana alinipa msukumo wa kutomruhusu yule pepo kuondoka bila kujieleza yeye ni nani na amekuja kufanya nini na kwanini…nikawa nimeanza kumhoji yule pepo kwa MAMLAKA NA NGUVU YA MUNGU ILIYOKUWA PALE…Akajieleza Yeye ni MAKATA na ametumwa kuharibu maisha ya yule dada, ametumwa na bibi yake kwa sababu yule bibi hakuwa anapenda mama wa yule binti kuolewa na mwanae [baba wa yule binti] na yule bibi ni mshirikina sana ni mtu wa kwenda kwa waganga wa kienyeji na huko ndiko ambako yule PEPO alipewa jukumu la kuhakikisha anamharibia maisha yule binti…nikamuuliza kwanini umekubali kufanya hiyo kazi wakati unajua kuwa huyu binti ameokoka na Yesu yumo moyoni mwake? akajibu akaniambia, alimpa msukumo yule binti kwenda kwa shangazi yake, ambako hakuna MAOMBI WALA NGUVU ZA MUNGU na wakati yule binti alipolala usiku, yule pepo alimwingia kupitia ndoto ya kumlisha nyama ndotoni….na tangu hapo yule binti yule alianza kuteseka na kusumbuka na matatizo ya kifua, kichwa na upinzani kwenye maisha yake…

Yule binti ni mwimbaji sana, yule pepo akaizuia sauti yake, kwa sababu yule binti akiimba, nguvu za Mungu zinashuka…hata hiyo jana kabla sijafundisha, yule dada alipaswa kuongoza nyimbo za sifa na kuabudu lakini ghafla sauti yake ikakata, ikabidi akae tu!

Nikamuuliza yule pepo ni mambo gani kwenye maisha ya yule binti ameyaharibu na kwa njia gani? akanijibu akaniambia, huyu binti anataka kuwa mtu mkuu, anataka kuwasaidia watoto yatima, hata akiwaona anawahurumia sana mpaka anaanza kulia…Tangu akiwa form one amekuwa akiandika ndoto zake na namna ya kuwasaidia watoto yatima na mabinti wadogo wajitambue wasije kuharibikiwa…na kikubwa zaidi tayari huyu binti ameanza kutekeleza sehemu ya maono yake…kwa hiyo kama sitamzuia lazima atatimiza ndoto zake na hakuna cha kumzuia kwa sababu ANAZIOMBEA ZILE NDOTO NA ANA MOYO WA UPENDO NA TAYARI AMEANZA KUSHIRIKIANA NA WATU SAHIHI AMBAO WATAMSAIDIA KUTIMIZA NDOTO ZAKE…sitamruhusu maana atafanikiwa sana na atakuwa mtu mkuu!

Baada ya yule pepo kunidokeza siri kuhusu yule binti na familia yake na yale ambayo amefanya kwenye familia ya uharibifu, nikamgeuzia kibao anipe siri za hali ya nchi yetu inavyokwenda, na swala la makanisa kuchomwa na vurugu za wana uamsho…

Yule pepo alitaka kunigomea na kudai yeye ametumwa kuharibu maisha ya yule binti na familia yake na si nchi…kwahiyo yeye yule pepo hajui kitu kuhusu maswala ya nchi…nikagundua jinsi ambavyo amesema uongo…nikamwambia, si mimi ninayehitaji kujua siri ya kinachoendelea Tanzania, bali YESU WA NAZARETH, MFALME WA WAFALME ANATAKA KUJUA…

Baada ya kuwa nimembana hapo yule pepo akaanza kueleza, “KINACHOSABABISHA MAKANISA YACHOMWE SI SWALA LA KUKOJOLEA KURAAN, ILE NI GERESHA TU, SISI [MAPEPO] TUNATAKA WAOMABJI WAACHE KUOMBA KWA USAHIHI WAAMISHIE MAOMBI NA UMAKINI WAO KWENYE HAYO MATUKIO NA WAANZISHE VURUGU ZA KIDINI NA WAISLAMU”
Nikamwambia yule pepo, “Hilo najua, ila Yesu anataka useme chanzo hasa/ halisi cha ninyi kuamua kuanzisha hizo vurugu” akajibu akasema, “KUNA WAOMBAJI WANAOMBA SANA KWA AJILI YA NCHI, HASA MWALIMU MWAKASEGE NA JOSEPHAT MWINGIRA NA WATU WAO NA WANASABABISHA MAMBO YETU YA UENDESHAJI SERIKALI KWA MSINGI WA UFALME WETU [SHETANI] NA MIKATABA YA UFISADI NA MAKUBALIANO KATI YA VYAMA NA SIASA NA SERIKALI YA KUIHUJUMU NCHI NAYO YAMEKUWA YAKIDHIHIRIKA NA HAWAPATANI TENA, WANAGOMBANA NA MIKAKATI YETU INAHARIBIWA NA NCHI INAFUNGULIWA KWENDA KULE AMBAKO MUNGU WENU ANATAKA IENDE”

Nikamuuliza tena, sawa lakini mnatumia njia gani kufanikisha uchochezi na uvunjifu wa amani katika nchi yetu na kuwapoteza waombaji? akanijibu na kusema, “TUNAWATUMIA MASHEKHE NA WAISLAMU WA NGAZI ZA CHINI KWA KUWADANGANYA KAMA TULIVYOFANYA KUPITIA KURAAN KULE MBAGALA”

Baada ya kupata mambo ya muhimu ambayo niliyataka mimi na Bwana Yesu, kisha yule pepo akatolewa kwenda shimoni!
Na Mungu akaniambia, hakikisha hili linawafikia watu waliookoka kwa wingi uwezavyo, ili warudi kwenye nafasi zao na waombee nchi iende kule ambako Mungu alikusudia iende, mnakaribia kufika mahali pa ustawi enyi Watanzania…
SHARE STATUS HII KWA WINGI UWEZAVYO ILI WATEULE WALIOOKOKA TANZANIA NA WAKRISTO WAENDELEE KUMCHAPA SHETANI NA KUHARIBU MBINU NA MIPANGO YAKE YA KUHARIBU NCHI YETU…Mungu ameibariki Tanzania!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “SABABU HALISI YA MAKANISA KUCHOMWA TANZANIA
  1. marko daudi says:

    nipatie mafundisho

  2. PETER says:

    wachungaji wengi wamejikita kupata pesa kuliko kumtumikia katika roho na kweli BwanaYESU , Maoni YANGU tufanye kilicho tuita, fedha itatupeleka pabaya. MIMI NI PETER KALINDA THE DUROS OF CHRIST JESUS

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: