NI MUHIMU UJUE HAYA KAMA UNATAKA KUWA MTU MKUU…

1.Hakuna mtu mkuu ambaye amekutanizwa na huo Ukuu wake, alikuwa akijiandaa na akifanya yale yatakayomleta pale anapotaka kuwa…Yusufu alikuwa akifanya mazoezi ya Uongozi na Usimamizi kule kwa Potifa na kule gerezani…Mungu anajua umuhimu wa Mafundisho/mafunzo kabla ya wewe kuwa kwenye nafasi aliyokuandalia…Ndio maana nawashangaa Wakristo wenza

ngu mkipita kwenye magumu mnamlaumu Mungu na kumtazama Shetani kwa kukuletea hilo gumu…Ni nadra sana kwa Mkristo kuangalia changamoto yake kama darasa au ngazi ya kwenda pale pazuri ambako Mungu amemwekea/amemwandalia!

2.Watu wakuu wote unaowafahamu wewe, ni watu wa nidhamu ya juu sana; Hawafanyi kila kitu kwa vile tu kiko ndani ya uwezo wao au ndani ya muda wao au kwa kuwa ni chema/ si kibaya…Ni watu ambao hawatoi jicho lao kwenye njia ya kuelekea kule waendako…Mtu mwenye Maono/ mtu mkuu hujizuia/ana nidhamu ya maisha!

3.Watu wakuu wote unaowafahamu, wanajua thamani ya kila mtu anayewazunguka, wanajua kuwa Watu ni rasilimali ya muhimu katika kufika pale waendapo. Hivyo hawachagui watu kwa kuangalia nini wanaweza kupata toka kwao, bali wanachagua watu kwa sababu ya uelewa kuwa kila aliyeumbwa na Mungu ana kitu cha thamani kinachoweza kubadilisha maisha au kukusogeza mahali kuelekea ukuu!

4.Watu wakuu unaowafahamu wewe, ni watu wenye nidhamu ya muda wao…Wanajua kuwa Pesa iliumbwa baada ya muda, muda kwanza mengine yote yanafuata nyuma…Wanajua kutumia vema masaa 24 yao waliyopewa na Mungu…Mimi kama mtu mkuu, nautumia muda wangu kufanya mambo haya matatu tu:
-a)Kuwasaidia wengine ili nao waboreshe fikra na mitazamo yao ya maisha, waishi kwa kiwango kile ambacho Mungu aliwaumba wakiishi, nafanya hilo kupitia mafundisho yangu hapa facebook, makanisani, fellowship nk
-b)Kujiongezea ufahamu, maarifa, hekima na elimu ya rohoni na pia kuulisha Ubongo wangu, kupitia vitabu, kuhudhuria semina, makongamano na kubadilishana mawazo na watu ambao tayari wameshafikia hatua fulani kubwa za Ukuu (role models/mentor wangu)
-c)Kufanya shughuli yoyote ile inayoweza kunipa shilingi kadhaa mfukoni, na pia kupumzika(kulala na muda wa kawaida wa mapumziko)

5.Watu wote wakuu unaowafahamu wewe, ni watu ambao hawafanyi kila kitu kwa sababu tu eti wanaweza kukifanya au kwa vile ni chema/ si kibaya au kwa vile ni cha maendeleo. Ni watu wanaofanya kile tu ambacho kwa mioyo yao yote wanajisikia amani na furaha kukifanya…Kiasi kwamba hawahitaji kusukumwa wala kugombezwa na mtu kufanya hicho/ hiyo kazi…Kwa sababu iko moyoni mwao, wanaweza kuamka asubuhi saa 10 alfajiri na kutoka ofisini saa 3 usiku lakini wala hawana lawama au manung’uniko kwa kuwa wanafanya walichoumbwa kufanya!

6.Watu wote wakuu unaowafahamu wewe, ni watu ambao hawafanyi kila kitu, bali wanafanya mambo sahihi, ndnai ya muda sahihi na mahali sahihi na wakiwa na watu sahihi…Wakilenga shabaha hawakosi, ndio maana wanang’ara kila wanachofanya!

KAMA UNATAKA MIAKA KADHAA TUWE WOTE KWENYE ORODHA YA WALIOHAMA TOKA DARAJA LA WATU WA KAWAIDA [ordinary people] KWENDA DARAJA LA WATU WAKUU, WASIO WA KAWAIDA [extra-ordinary people] weka haya kwenye matendo, usiwe unaishia ku-comment na ku-like…MABADILIKO NI MCHAKATO!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: