Amani na Furaha Yako

Haijalishi unapitia CHANGAMOTO, TATIZO, UGUMU au SHIDA gani… Usiruhusu zikuibie AMANI NA FURAHA YAKO… Jifunze kuwa kimya, mtulivu na kuilinda amani yako kwa gharama zote… Usiyaitikie maisha kutegemeana na nini UNAONA AU UNASIKIA AMA KUHISI… Matatizo na Changamoto ni sehemu ya safari ya maisha, Hivi vyote huja ndani ya muda na kuondoka! Hakuna Shida, tatizo au Changamoto ya Milele, VYOTE VI

NA MWISHO… Mtu ALIYEFANIKIWA ni yule anayeweza kutunza FURAHA NA AMANI yake wakati wa magumu badala ya Kukata tamaa na kuzama. Ndio maana ni MUHIMU SANA NA LAZIMA kujizoeza kutafuta MAARIFA YA NENO LA MUNGU toka kwenye BIBLIA NA VITABU VYA WATUMISHI WA MUNGU WALIOFANIKIWA… Haya maarifa hubadili kabisa MTAZAMO NA DEFINITION YAKO YA MAISHA… Unapoyaweka kwenye MATENDO unaitwa mwenye HEKIMA… Maisha yanakuwa yamejengwa juu ya MWAMBA, Hautikiswi na MVUA, UPEPO wala MAFURIKO YA MAISHA… Unakuwa IMARA kama MLIMA SAYUNI, hautikiswi wala kuyumbishwa na chochote! Usifungue kinywa chako na kuanza kuzungumzia UKUBWA/ UGUMU wa tatizo/ shida yako, ni sawa na KUYAWEKEA MBOLEA NA MAJI MAGUGU HUKU UKIAMINI YATANYAUKA… Jizoeze kuikabili Changamoto yako kwa NENO LA MUNGU… Hata nyakati GIZA LIMETANDA likabili kwa NENO, NENO LA MUNGU NI KWELI… Mungu hatakuacha wala kukupungukia, atakuwepo muda wote kukusaidia… Ila HATAFANYA LOLOTE mpaka umpe Nafasi kwa kumfungulia MLANGO huitwao IMANI… Huu ndo mlango pekee utakaomfanya Mungu awavuke binadamu wengine bilioni 7 wanaomhitaji kuja kujishughulisha na mambo yako! Kumbuka, “Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu”… (share ujumbe huu uwasaidie na wengine)!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: