Dhambi adui mkubwa wa Imani,Ujasiri na Mamalaka

http://touchyaneighbor.files.wordpress.com/2011/05/sin12.jpgHAKUNA ADUI MKUBWA wa IMANI, UJASIRI na MAMLAKA kama DHAMBI… Dhambi inakuvua mavazi ya WOKOVU, HAKI, SIFA na NEEMA… Badala ya Mungu kuwa BABA wa karibu na RAFIKI wa kumkimbilia na kumfurahia, anaonekana kama ADUI na MHUKUMU wako… Badala ya FURAHA, AMANI na UHAKIKA, DHAMBI inaleta HUZUNI, MASHAKA, WOGA na HOFU… Badala ya kumsogelea SHETANI kwa UJASIRI na JEURI YA KIFALME na kumgusa machoni,

Unaanza KUKIMBIA HATA KIVULI CHAKO…Hata paka au bundi akilia nje ya nyumba yako UNAANZA kumwona SHETANI NA JESHI LAKE wakija kukumaliza… DHAMBI ZOTE zina RADHA NZURI na zinaonekana kama zinalipa au zina faida kwa muda ule mchache wa kuzifanya, NGOJA UMALIZE ndipo utakapojua DHAMBI INAVYOUMIZA NA KULEMEA KULIKO MZIGO MWINGINE WOWOTE…AMNONI alipombaka dadake TAMALI alifurahia kwa dakika kadhaa kukaa mapajani mwake [KAMA WEWE DADA/ KAKA MZINZI UNAYEDHANI KUBADILI WANAWAKE/WANAUME NI FAHARI] lakini alipomaliza ALIMCHUKIA KWA MACHUKIO MAKUU MNO… Wakati YUDA ISKARIOTI anakusanya vipande 30 vya FEDHA [KAMA WEWE MFANYAKAZI WA UMMA UNAYEPOKEA NA KUTOA RUSHWA HALAFU UNASEMA SIKUWA NA JINSI HATA MUNGU ANAJUA] alipomaliza kumuuza Yesu hakufaidi hata ile hela aliishia KUJINYONGA… Petro alipomkana YESU mara 3 hakuona kuwa ni issue sana lakini JOGOO alipowika mara ya 3 aliangua kilio kama mtoto mdogo kwa uchungu[Kama wewe unavyomkana Yesu na Imani yako kama mwanafunzi wa Yesu kwa ajili ya kupata manufaa mawili matatu lakini mwisho wa siku unaishia kuumia, kulia na kukosa amani na furaha ya maisha pale SHETANI ANAPOANZA KUKUSHITAKI NA KUULIZIA JUU YA UKRISTO WAKO]…DHAMBI NI MBAYA…Itakupeleka umbali ambao hukutaka kwenda…Itakufanya ulipe gharama ambazo hukuwa umejiandaa nazo!
UKIONA MTU ANATESWA NA MAPEPO, WACHAWI, MIZIMU, SHETANI, MAGONJWA, KUJITUMA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII SANA ILA ANAISHIA KUPATA MATOKEO YA CHINI AU HAKUNA…UWE NA UHAKIKA MAISHA YAKE SI MATAKATIFU…KUNA MIFEREJI YA DHAMBI MAISHANI MWAKE NA YEYE AMEIKUMBATIA… HATA KAMA ANANENA KWA LUGHA ZA WANADAMU NA ZA MALAIKA…PALIPO NA MZOGA NDIPO WAKUSANYIKAPO TAI… PALIPO NA MAVI NDIPO WAKUSANYIKAPO NZI… PALIPO NA MAUA NDIPO WAKUSANYIKAPO NYUKI!

“ATENDAYE DHAMBI NI WA IBILISI KWA MAANA YEYE HUTENDA DHAMBI TANGU MWANZO”
“YEYE MWENYEWE[YESU] ALICHUKUA DHAMBI ZETU MWILINI MWAKE JUU YA MTI, ILI TUKIWA HAI KWA MAMBO YA HAKI, TUWE WAFU KWA MAMBO YA DHAMBI”
“ALIYEZALIWA NA MUNGU HATENDI DHAMBI MAANA UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE”
“AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA,BALI AZIUNGAMAYE NA KUZIACHA ATAPATA REHEMA”
“TUKIZIUNGAMA DHAMBI ZETU, YEYE NI MWAMINIFU NA WA HAKI HATA ATUONDOLEA DHAMBI ZETU NA KUTUSAFISHA UDHALIMU WETU WOTE”
(Hakikisha una-SHARE ujumbe huu kadiri uwezavyo kwa utukufu wa Mungu au Post kwenye wall yako)!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: