Nini umepata kupitia wokovu?

Unajua Wakristo, Walioamua kwa dhati kumwamini na kumpokea Yesu wanaishi maisha ya dhiki na ya chini sana kwa sababu wengi wao hawajui nini wamepata kupitia WOKOVU na kazi njema ya Yesu msalabani…hapa nitakudokeza baadhi tu ya hayo yote ambayo Umeyapata na ni haki yako kama Mkristo, haijalishi unajua au hujui…nayo ni;

.Umesamehewa DHAMBI ZAKO ZOTE…HAZIJAFUNIKWA NA WALA HAKUNA KUMBUKUMBU LA

DHAMBI ZAKO…DAMU YA YESU IMEZIONDOA KABISA…MUNGU AMEZITUPA DHAMBI ZAKO NYUMA YAKE…AMEKUTENGA WEWE NA DHAMBI ZAKO KAMA MASHARIKI ILIVYO MBALI NA MAGHARIBI… YESU AMECHUKUA DHAMBI ZAKO MWILINI MWAKE… (Ufunuo 1:4-5, Isaya 1:18, Isaya 38:17, Isaya 43:25, 1 Petro 2:24, Zaburi 103:12)

.WEWE NI UZAO MTEULE[Umeteuliwa kati ya watu wengi kumjua Mungu na siri zake], UKUHANI WA KIFALME[Umepewa nafasi ya kusimama kama Mfalme kwa niaba ya Mungu na kufunga chochote duniani na Mungu naye akakifunga, au kukifungua chochote duniani na Mungu akakifungua…USIPOFANYA HIVYO, HATA MUNGU HAWEZI KUFANYA LOLOTE DUNIANI, NDIO MAANA SISI NI WATENDA KAZI PAMOJA NA MUNGU…Pia umepata Cheo cha kuwa KUHANI, Kwa ujasiri kabisa waweza kusimama mbele za kiti cha enzi cha Mungu kwa DAMU YA YESU, na KUHOJIANA NAYE, UKAPELEKA HOJA ZAKO ZENYE NGUVU, UKAMKUMBUSHA, NA HATA KUMWAGIZA KWA HABARI YA KAZI YAKE NA MAMBO YA WANAWE…], WEWE NI MTU WA MILKI YA MUNGU [ni mali ya Mungu, Mungu mwenye enzi, mamlaka na uweza wote ndiye anayekumilki na kukutunza, uko kwenye mikono salama, hakuna wa kukugusa, AKUGUSAYE ANAIGUSA MBONI YA JICHO LA MUNGU…KILA SILAHA INAYOFANYIKA KINYUME CHAKO HAIWEZI KUFANIKIWA, LABDA WEWE UAMUE NA UKUBALI…WANAOKUSANYANA JUU YAKO LAZIMA WAANGUKE…Wewe ni mtu wa nyumbani kwa Mungu, ni mwenyeji wala si mpitaji au mgeni]…WEWE NI TAIFA TAKATIFU…[Mungu anajivunia uwepo wako duniani, kama alivyokuwa akijivuna kuhusu Ayubu, ndio maana Shetani anajaribu kuleta changamoto ili akupofushe udhani Mungu amekusahau au hayuko upande wako…Uko kwenye mikono salama, WEWE NI MTAKATIFU ALIYEKO DUNIANI AMBAYE MUNGU ANAJIVUNIA…Wewe ni wakili wa siri za Mungu…Roho Mtakatifu aliyemfufua Yesu anakaa ndani yako… Yule Roho wa Bwana anayefungua waliofungwa, anayehubiri habari njema kwa masikini, anayeweka huru waliosetwa, anayewapa vipofu kuona tena anakaa ndani yako…Yule Roho anayetufundisha, anayetuongoza, anayetufunulia siri za Mungu na Mafumbo yote anakaa ndani yako…]
(1Petro 2:9-10, Warumi 8:29-30, Mathayo 16:16-18, Mathayo 18:18-20, Zaburi 115:16, Waebrania 10:19, Isaya 43:26, Isaya 41:21, Isaya 45:11, Zekaria 4:8, Isaya 54:14-17, Waefeso 2:19, Ayubu 1:1-3, 2:6-11, Zaburi 16:3, 2Wakorintho 4:1, Warumi 8:11, Luka 4:18, Yohana 14:26, Yohana 16:13-15, Warumi 8:14, 1Wakorintho 2:9-12)

KWAKUWA WENGI WENU NI WAVIVU WA KUSOMA BIBLIA NADHANI NIISHIE HAPA KWA LEO…HAKIKISHA UNAPITIA HAYA MAANDIKO, YAAMINI, YAKIRI, YATENDE NA HAUTAKUWA WA KAWAIDA… (Share hii kwa wingi kadiri uwezavyo)

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: