Kua boss juu ya shetani na mawakala wake wote

SHETANI YUPO, MAPEPO, MAJINI, MIZIMU, UCHAWI NA UHARIBIFU, UCHAFU, WIZI NA UUAJI WAKE pia upo… HAIJALISHI UNAAMINI HILI AU HAULIAMINI KAMA SERIKALI, HAUTABADILISHA UKWELI WA HILI… Ila sisi tulio ndani ya Kristo Yesu, ni MABOSS juu ya kila FALME, MAMLAKA, WAKUU WA GIZA NA KILA AINA NA RANK YA PEPO WABAYA katika ULIMWENGU WA ROHO!
Kinachotupa JEURI ya kuwatambia hawa waharibifu na kuwatemea mate

usoni ni KUIJUA KWELI, NENO LA MUNGU, KATIBA YA UFALME WA MUNGU, UFALME MKUU WA WATU WAKUU, WALIONUNULIWA KWA DAMU YA THAMANI YA YESU, NA KUINGIZWA KATIKA HADHI YA UFALME NA UKUHANI, ILI WATAWALE JUU YA NCHI…WATU WALIOZALIWA NA BABA NA MAMA kama wewe, lakini WENYE URAIA WA MBINGUNI KUPITIA MSALABA…WATU WA MILKI YA MUNGU, WATU WA NYUMBANI KWA MUNGU, UZAO MTEULE, TAIFA TAKATIFU…WATU AMBAO MUNGU MKUU ANAKAA NDANI YAO…WATU AMBAO WANA MTAZAMO NA FIKRA ZA JUU…WATU WALIOKETISHWA PAMOJA NA MUNGU, JUU SANA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO!Mambo yanayomfanya Mkristo awe BOSS juu ya Shetani na mawakala wake wote ni;

1.Maisha matakatifu
2.Kujua hadhi na haki zako katika Ufalme wa Mungu ambako Yesu amekuingiza
3.Kuishi sawa na Neno la Mungu
4.Kuishi maisha ya Haki
5.Kuwa na Ushirika wa dhati na Roho Mtakatifu
6.Kusimamia maslahi ya Ufalme wa Mungu hata kama itakugharimu uhai wako
7.Kuishi vema na wanaokuzunguka; Kuwa na amani na watu wote, kujifunza kuwasamehe waliokukosea hata wasipoomba msamaha, kuushinda ubaya kwa wema
8.Kuishi maisha yaliyojaa UPENDO WA MUNGU; Upendo usio na sababu
9.Kujifunza kuumiliki na kuutawala MDOMO NA ULIMI WAKO
10.Kuishi maisha ya UNYENYEKEVU, UTIIFU NA UAMINIFU
(Kama umejifunza kitu, SHARE kwa wengine nao wapate maarifa)!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “Kua boss juu ya shetani na mawakala wake wote
  1. MWL.EVODIUS YOHANA says:

    Oh!Mungu akubarki sana mtumishi wa mungu somo limenibark sana

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: