Tunajambo lakushuhudia

Mungu akikupa nafasi ya kuiona siku mpya, na kuwa hai katika siku hiyo, huo ni ushahidi tosha kuwa; 1. Mungu ana kazi na maisha yako bado na kama ana kazi na wewe, uwe na uhakika Mungu atayagharamia maisha yako katika maeneo yote… Lakini itatokea pale tu utakapojua kitu gani au jambo gani Mungu anataka ufanye kwa niaba yake na kuanza kulitenda 2. Mungu amekupa nafasi ya kuyagusa maisha ya weng

ine na kuyapa thamani 3. Mungu amekupa nafasi ya kuweka rekodi na alama ya maisha yako hapa duniani… Rekodi au alama hiyo inaweza kuwa ya mema au mabaya, uchaguzi ni wako, hata Mungu hawezi kuingilia 4.Mungu ameiondoa jana, amekupa leo, Mungu anataka ujue kuwa haiangalii jana yako kukutengenezea kesho yako njema. Hivyo jizoeze kuyasahau mabaya yaliyopita, unaweza kuwa bora leo na kuandika historia mpya, unamkumbuka Rahabu yule kahaba? Unamkumbuka Ruthu mkwe wa Naomi? Unamkumbuka Yabezi? Wote hawa walikuwa na JANA/ HISTORIA MBAYA lakini walipoelewa thamani ya LEO YAO kila kitu kikabadilika 5. Mungu anapokupa fursa ya kuwa hai anataka ujue kuwa amekupa MTAJI WA KUPATATA YOTE UYATAKAYO hapa duniani. Anataka ujue kuwa bila MAISHA/ UHAI yote uyatakayo hautayapata… Anataka ujue kuwa ni BORA MARA MIA kuwa MBWA ALIYE HAI kuliko kuwa SIMBA ALIYEKUFA! 6. Mungu anapokupa fursa ya kuwa hai, anataka uutumie muda huo kujiandaa kwa ajili ya MAISHA YA MILELE, MAISHA BAADA YA KIFO… Ndio maana Mungu anakupa nafasi kunisikia nikizisema habari za Yesu, Msamaha wa dhambi, Uzima wa milele, Hukumu, Mbinguni na Jehanamu nk. Lakini UAMUZI NI WAKO… Ila uamuzi huo utakupa furaha au kilio milele… Tukutane mbinguni ukipenda au Mpotezee Yesu wangu naye hakupotezee siku UKIKATA PUMZI!
Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: