Elewa na kutambua haki yako

image

Moja kati ya mambo yanayochangia SWALA LA KURITHI LAANA toka kwa waliotangulia ni KUTOJUA KUWA WOKOVU UMEFANYA KWAKE YAFUATAYO…  Wokovu Umeshughulika na maeneo yote ya mtu; ROHO, NAFSI NA MWILI… Wakristo wengi sana (karibu wote) wanadhani WOKOVU umeshughulikia ROHO ZAO TU na umeacha NAFSI NA MIILI YAO ikiwa vilevile. Wanaupima na kuupokea Wokovu kwa HISIA… Wanajitazama, Wanajiona NDANI YA ROHO ZAO WAMEPATA UHAI, WANAICHUKIA DHAMBI, NA HAWANA TENA KIU YA DHAMBI mara baada ya MAOMBI YA IMANI KUMPOKEA YESU kupitia SALA YA TOBA… Lakini wanaendelea KUWA CHINI YA LAANA kwenye NAFSI (Eneo linaloshughulika na maswala yote ya AKILI, UFAHAMU, FIKRA, MAWAZO, MAAMUZI NA MACHAGUO) na kwakuwa wanaishi kwenye MIILI, LAANA ZINAONEKANA KWENYE MAISHA YAO kwa KUTOFANIKIWA KWENYE MASWALA NA MAENEO MBALIMBALI YA MAISHA, KUKWAMA, KUTOVUKA VIWANGO FULANI VYA MAISHA, KUKUMBWA NA MATUKIO MABAYA YALIYOWAHI KUWAKUTA WAZAZI, NDUGU WALIOWATANGULIA, KUKOSA AMANI NA FURAHA YA MAISHA, KUYACHUKIA MAISHA NA HATA KUCHUKUA MAAMUZI MABAYA IKIWEMO HATA KUJIUA, nk! UKWELI NI KWAMBA: Shetani anatumia NAFASI ALIYOPEWA na hawa WAKRISTO kwenye NAFSI NA MIILI YAO kwa kutojua (kukosa maarifa) kwamba WOKOVU NI UUMBAJI WA MTU KUFANYWA KIUMBE KIPYA KABISA AMBACHO HAKINA UHUSIANO NA MAMBO YA ZAMANI, ZIKIWEMO LAANA ALIZOKUWA NAZO KABLA YA WOKOVU (2 Kor 5:17)… Kiumbe huyu anapewa NAFSI MPYA; NIA/ AKILI YA KRISTO (1 Kor 2:16) inayomfanya awe na kiu ya KUFANYA MAPENZI YA MUNGU NA KUMPENDEZA MUNGU kama alivyokuwa Kristo Yesu… na mwisho kiumbe huyu aliyeokoka MWILI WAKE UMEUMBWA UPYA, Si ule uliokuwa ukikandamizwa na MAPEPO, NGUVU ZA GIZA, MIZIMU, UCHAWI, MAGONJWA nk, MWILI WA ALIYEOKOKA ni HEKALU LA MUNGU NA ROHO MTAKATIFU ANAKAA NDANI YAKE (1 Kor 3:16-17) na tangu hapo MUNGU ANACHUKUA UDHIBITI… Ila HAIFANYI KAZI Mpaka MWAMINI AJUE HILI, LIWE MFUMO WAKE WA MAISHA, UKIRI WAKE MBELE YA WATU NA SHETANI! Pia ni muhimu MKRISTO AELEWE NA KUTAMBUA HAKI, UHALALI,NA NAFASI YAKE MBELE ZA MUNGU kupitia AGANO JIPYA!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: