Imani ni zaidi ya ulichonacho

image

Imanl

Watu wa IMANI huwa hatuangalii nini tunacho, ama nini tunaona ama kusikia, au hisia zetu zinasemaje… Huwa na kitu kimoja tu kinacho yatawala maisha na misimamo yetu, kitu hicho kinaitwa NENO LA MUNGU… Kila alichosema MUNGU NI SHERIA… Hakina mjadala, LAZIMA KIWE! Mara zote macho yetu na akili zetu vimeelekezwa kwenye WAKATI UJAO [FUTURE] na katika MAMBO YASIYOONEKANA SASA… Tuna UHAKIKA NA MAMBO YATARAJIWAYO kuliko YAONEKANAYO… Na siku zote hatuna muda wa KUYAWAZA YALIYOPITA ama kupoteza muda kwenye MAKOSA YETU NA UDHAIFU WETU WA SASA… TUNAYAONA YASIYOKUWEPO [KWA KUWA YAPO KWENYE NENO TAYARI] na kwa Ujasiri TUNAYASEMA YASIYOKUWEPO KANA KWAMBA YAMEKUWEPO… Tuna Asili ya Mungu ndani yetu ya KUTANGAZA MWISHO WA JAMBO LOLOTE TANGU MWANZO WAKE… TUNAKUSUDIA NENO LOLOTE NALO LINATHIBITIKA KWETU… HATUWEZI KUONGEA MANENO MATATU BILA KUSEMA, MUNGU NI MWEMA, MWAMINIFU, ANATUWAZIA MEMA, ATATUPA TUMAINI, ANATAKA TUFANIKIWE… KATIKA NJIA ZETU ZOTE TUNAMKIRI YEYE, NAYE ANAYANYOOSHA MAPITO YETU… Wakati Dunia inawafundisha Vijana kuwa Mwanaume wa Ukweli ni yule aliye MZINZI, anayebadili akina dada kama MBWA… SISI TUNASIMA PAMOJA NA MUNGU NA KUWEKA WAZI, “AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA [NI TAAHIRA]”… Wakati dunia inajitahidi kupoteza thamani ya walio wengi kwa kuwaelekeza kwenye njia za UHARIBIFU NA MAANGAMIZO… WATU WA IMANI TUNASEMA, “KUMCHA MUNGU, UAMINIFU, UNYENYEKEVU NA HAKI VITAMPANDISHA YEYOTE KWENYE VITI VYA WAKUU TENA BILA GHARAMA”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: