Ishi kwa malengo

 Napenda huu Mwaka Mpya 2013 Ukiwa Unayajua, Kuyakumbuka, Kuyaamini Na Kuyaishi Mambo Haya Yafuatayo;

1.Mungu Alikujua Hata Kabla Mimba Yako Haijtungwa Kwenye Tumbo La Mama Yako (Yeremia 1:4-5)… Kwa Lugha Nyingine Rahisi, “MIMBA YAKO ILITUNGWA KWANZA KWENYE MAWAZO YA MUNGU KABLA YA TUMBO LA MAMA YAKO”

2.Mungu Ametangaza Mwisho Wako Tangu Mwanzo Wako (Isaya 46:9-10)… Ila Usije kufanya Kosa La Kukaa tu Ukidhani Kuwa Mungu Ameshafanya Kila Kitu Kwa Ajili Yako Na Ukaacha Kuwajibika Ili Kuacha Alama Hapa Duniani… Una Sehemu Yako Ya Kufanya, Kwanza Unamuuliza Mungu, Unapitia Neno Lake Na Kupata Wazo Na Mtazamo Wake Kisha Unautendea Kazi Na Kujenga Juu Yake Kama Msingi!

3.Mungu Anakuwazia Mawazo Mema Na Ya Amani (Yeremia 29:11)… Mabaya Yote Yanayotokea Kwako Hayatoki Kwake, Yanatoka Kwa “mungu wa dunia hii- shetani”…. Japo Mungu Anaweza Kuyaruhusu Kwako Kwakuwa Anajua Una Misuli Ya Kuyahimili Na Zaidi Atakupa Mlango Wa Kutokea… Atakuwa Pamoja Nawe Taabuni!

4.Mungu Anajua Ya Kuwa Unahitaji Kula, Kunywa Na Kuvaa, Na Kubwa Zaidi Hapendi Upoteze Umakini Wako Na Kuacha Kumwabudu Yeye Na Kuyatafuta Hayo Kwa Kuyapa Nafasi Ya Kwanza Badala Ya Kile Alichosema Katika Neno Lake (Mathayo 6:28-33)… Mungu anatumia muda wake, Akili Na Ufahamu Wake Kuwalisha Ndege Wa Angani, Kuyavika Maua Ya Kondeni, Hauhitaji Kufikia Hatua Ya Kutenda Dhambi Ili Kupata Chakula Au Mahitaji Ya Kimaisha!

5.Mungu Ana Kawaida Ya Kuwasaidia Na Kuwapandisha Wanyenyekevu, Na Huwa Anawashusha Wenye Viburi Na Wajikuzao (Yakobo 4: 6)… Yesu Amepata Hadhi Na Heshima Baada Ya Kufa Na Kufufuka Kwa Sababu Alikuwa Mnyenyekevu, Akatii Hata Mauti Ya Msalaba, Akayafanya Mapenzi Ya Baba Yake, Kiasi Cha Kufikia Kusema Mapenzi Ya Baba Yake Ndicho Chakula Chake… Anatuhimiza Tujifunze Kwake Maana Yeye Ni Mpole Na Mnyenyekevu Wa Moyo!

6.Usifikie Hatua Ya Kumkasirikia Mungu Au Kumlaumu Mungu Kuwa Amekuacha Au Amekutelekeza… Huo Si Ukweli, Amekuchora Kiganjani Mwake Na Kuta Zako zi Wazi Mbele Yake Daima (Isaya 49:16)…. Yuko Nawe Siku Zote Hata Ukamilifu Wa Dahari (Mathayo 28:20)… Hatakuacha Wala Kukupungukia, Hata Nyakati Ambazo Hauhuhisi Uwepo Wa Mungu Ni Hakika Anakuwa Nawe Kukusaidia Na Kukushika Mkono (Isaya 41:10)!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: