MAISHA: UHAKIKA WAKO KUSTAWI NA KUFANIKIWA

“Kwa Sababu Hiyo Nawaambieni, Msisumbukie Maisha Yenu, Mle Nini Au Mnywe Nini; Wala Miili Yenu Mvae Nini. MAISHA Je! Si Zaidi Ya Chakula, Na Mwili Zaidi Ya Mavazi? ” (Kauli Ya Bwana Yesu Katika Mathayo 6:25)

Mungu Ameniumba Ili Niwasaidie Watu Wawe Na Mtazamo Sahihi Juu Ya Mungu Na Maisha, Hii Ndo Kazi Yangu Kubwa Hapa Duniani.
Kwa Hali Yoyote Nitaifanya, Na Najua Maisha Ya Wengi Yatakuwa Na Maana Na Kusudi Na Lazima Wafikie Hatma Yao Sahihi Mungu Aliyowakusudia.

Adui Mkubwa Wa Maisha Sahihi Ya Ubora Na Ustawi Ni Nafsi Yake [Akili, Ufahamu Na Mfumo Wake Wa Kufikiri Na Kuwaza)… Siku Zote Alivyo Mtu Ni Matokeo Ya Vile Alivyojaza Kwenye Nafsi Yake, “Maana Ajionavyo Mtu Nafsini Mwake, Ndivyo Alivyo” (Mithali 23:7)
Hauwezi Kuwa Na Mtazamo Hasi Wa Maisha Ndani Ya Nafsi Yako Halafu Ukawa Na Matokeo Chanya Kwenye Maisha Yenyewe; Ni Sawa Na Kutarajia Mbuzi Amzae Kondoo, HAIWEZEKANI!

Kabla Mtu Hajastawi Na Kuwa Na Maisha Ya Mafanikio, Lazima Kwanza Abadili Namna Ya Kuwaza Na Kufikiri Kwake. Ndio Maana Neno La Mungu Linatuhimiza, “Wala Msiifuatishe Namna Ya Dunia Hii; Bali Mgeuzwe Kwa Kufanywa Upya Nia Zenu” (Warumi 12:2)

Lazima Kwanza Ubadili Mtazamo Wako Kuhusu Maisha, Kauli Zako Na Namna Ya Utendaji Wako Katika Maisha!

Leo Ninataka Kukusaidia Ubadili Mtazamo Wako Kuhusu Maisha Na Mafanikio, Sawa Na Kristo Yesu Alivyotufundisha Katika Neno Lake!
Wengi Wetu Wanadhani Kustawi Kwenye Maisha Kunaamuriwa Na Kiwango Cha Elimu, Familia Uliyotokea, Idadi Ya Ndugu Na Marafiki Ulionao Kwenye Maeneo Yenye Fursa nk (Hapa Sijaribu Kupinga Umuhimu Wa Hayo Mambo Niliyotaja Hapo Juu, Ni Ya Muhimu Ila Hayaamui Kiwango Cha Maisha Ya Mtu Moja Kwa Moja Japo Yana Sehemu Na Umuhimu Wake Katika Kuboresha Maisha Ya Mtu).

Bwana Yesu Anatukumbusha Jambo La Muhimu Sana. Anatukumbusha Kuwa, ” LOLOTE UNALOTAKA AU UNALOTARAJIA KUPATA KWENYE MAISHA, HALINA THAMANI SANA KULIKO MAISHA YENYEWE”

Kwa Lugha Nyepesi, BWANA YESU anataka tujue ya kwamba, “Kama Hauna Maisha [Hauishi] Hauwezi Kupata Lolote. Ila Ukiwa Na Maisha Unaweza Kupata Chochote”

Kwa Kurahisisha Fundisho Ili, “MAISHA NDIO MTAJI WA KILA UKITAKACHO NA UKITAFUTACHO MAISHANI… KAMA UNAISHI UNAWEZA KUPATA CHOCHOTE, ILA KAMA UMEKUFA, HAUNA MAISHA, NDOTO, MALENGO, MIPANGO NA MAKUSUDI YAKO YOTE YAMEKUFA NA HAYAWEZEKANI TENA”

Mfalme Suleimani Anasema, “HERI MBWA ALIYE HAI KULIKO SIMBA ALIYEKUFA”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: