MAMLAKA NA NGUVU

Mammlaka na nguvu

Shetani Anajua Kuwa Wakristo Wanayo Mamlaka [Authority] Katika Kristo Yesu, Lakini Bado Anaendelea Kuwakandamiza Na Kuwaburuza Wengi Wao… Ishu Si Kuwa Na Mamlaka, Kinachoyafanya Mamlaka Yako Yawe Na Thamani Ni Nguvu [Power] Uliyonayo Ambayo Ni Udhihirisho Wa Nje Wa Mamlaka [Authority] Uliyonayo!
Yesu Alikuwa Tishio Kwa Shetani Na Jeshi Lake Kwa Kuwa Alikuwa Na Vyote; Mamlaka Na Nguvu. Hata Alipokuwa Akiyapigisha Kwata Mapepo, Wale Walioona Walisema, “Mtu Huyu Ni Nani Hata Kwa Mamlaka Na Nguvu Anawatoa Pepo?”
Wakristo Wengi Wanadhani Watamtisha Shetani Kwa Mamlaka Tu Bila Nguvu, Lakini Nakuhakikishia Hakika Haitafanya Kazi, Maana Binafsi Nimekuwa Shahidi Wa Hili Katika Maisha Yangu Ya Utumishi!
Ufalme Wa Mungu Si Maneno Bali Ni Katika Udhihirisho/ Utendaji Wa Roho Na Nguvu… Yesu Amefanya Yote Aliyofanya Kwenye Huduma Yake Kwa Kuwa Mungu Alimpaka Mafuta Kwa Roho Na Kwa Nguvu (Matendo 10:38)
Hauwezi Kuwa Na Matokeo Aliyokuwa Nayo Yesu Kama Unatumia Kanuni Tofauti Na Alizokuwa Nazo Bwana Yesu!
Watumishi Wa Mungu Wanakula Tangu Jumatatu Hadi Jumapili; Kuanzia Chai, Chakula Cha Mchana Na Hata Cha Jioni
Wakikaa Kwenye Maombi Kwa Saa Moja Tu Tayari Wanaona Wamemaliza Kila Kitu, Yesu Alikuwa Akikesha Usiku Kucha Akiomba!
Watumishi Hawa Hawana Hata Muda Wa Saa Moja Wa Kusoma Neno La Mungu Na Kulitafakari Ili Kupata Ufunuo!
Watumishi Wa Aina Hii Huduma Zao Zitakua Kwa Staili Gani? Washirika Wao Watakuwa Na Maisha Ya Aina Gani Kiroho Na Kimwili?
Unadhani Watumishi Wa Aina Hii Wataacha Kuwasema Na Kuwatukana Akina TB JOSHUA, BENNY HINN, BG MALISA, MWINGIRA, MWAKASEGE, CHRIS OYAKHLOME nk Ambao Wanatumia Zaidi Ya Nusu Siku Na Mungu?

Kila Mkristo Ana Mamlaka Ndani Ya Kristo, Lakini Nguvu Zina Gharama Yake, Zinatafutwa, Haziji Tu Kama Upepo!
Unataka Upako; Fanya Kama Yesu Alivyofanya, Lipa Gharama!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “MAMLAKA NA NGUVU
  1. jane says:

    nzuri sana

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: