atakalo wambia lolote fanya

Njia Rahisi Ya Kupata Vya Mungu, “ATAKALO KWAMBIA LOLOTE FANYA”
Unaikumbuka Ile Harusi Kule Kana Ya Galilaya? Mariam Alijua KITUFE sahihi cha Kubofya… Aliwaeleza Watumishi/ wafanyakazi, Nendeni Kwa Bwana, ila “LOLOTE ATAKALOWAAMBIA FANYENI” (Yohana 2:5)… Ule Muujiza Ulitegemea Utii Wa Walioambiwa, Kama Wasingetenda Sawa Na Neno La Kristo Kusingekuwa Na Divai Mpya, Kusingekuwa Na Muujiza!
Unapokuwa Kwenye Uhitaji, Changamoto Au Ugumu, Chukua BIBLIA YAKO, Mwombe Mungu Akupe WAZO LAKE, Fungua Na Uchukue Kile Alichokusemesha, Halafu Usiishie Hapo, Nenda Kakitende!

MIUJIZA YOTE KATIKA HUDUMA YA YESU HAPA DUNIANI NI MATOKEO YA UTII WA WALE WALIOKUJA KUPATA SULUHU KWAKE:

Wale Wakoma Hakuwaombea; Aliwaambia Wakajionyeshe Tu Kwa Kuhani Na Kufanya Kama Musa Alivyoagiza, Wakiwa Njiani Kwenda Kutekeleza AGIZO, KAULI NA NENO LA YESU, MUUJIZA UKATOKEA!

Yule Aliyepooza Kwa Miaka 38 (Yohana 5): Hakumwombea, Hakukemea Pepo Wa Udhaifu, Ila Alimwambia,” SIMAMA, JITWIKE GODORO LAKO NA UENDE” Na Yule Mtu Alipotii Ile KAULI YA MAMLAKA, NENO TOKA KINYWANI KWA YESU, AKAWA MZIMA!

Yule Kipofu Aliyezaliwa Hivyo (Yohana 9) : Yesu Hakumwombea, Bali Alitema Mate Chini, Akampaka Tope Za Macho Halafu Akamwambia, “NENDA KWENYE BIRIKA YA SILOAMU NA UNAWE” Na Yule Kipofu Alipotii Na Kutendea Kazi AGIZO, SAUTI YA YESU, MUUJIZA UKATOKEA!

Muda Wowote Unapokutana Na Neno La Mungu, Madhabahuni Au Kwenye Biblia Moja Kwa Moja, Lichukue, Usiishie Kulisikia Au Kulisoma tu, Litende Kama Lilivyo, Bila Kuongeza Au Kupunguza Chochote, Utakutana Na Muujiza Wako!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: