FAHAMU UWEZA NA NGUVU YA KUSHUKURU

uweza wa kushukuru

Je Ulikuwa Unajua Kuwa Kushukuru Ni Hatua Ya Kwanza Na Ya Muhimu Kuelekea Kupokea Muujiza Wako Na Majibu Yako Toka Kwa Mungu?

Huu Ndo Ukweli Tunaoupata Kwenye Neno La Mungu; Kushukuru Kabla Ya Kukiona Kile Ukitarajiacho Kwa Mungu Ni Ishara Ya Nje Ya Kuonesha Kuwa Unaamini Mungu Ni Mwaminifu Na Atakupatia Hicho Ukitarajiacho Kwake. Kushukuru Ni Ishara Ya Nje Ya Kupokea Yale YASIYOKUWEPO NA YASIYOONEKANA BADO… Kushukuru Ni “MKONO WA KUYAPOKELEA MAMBO YA ROHONI KUJA MWILINI”

Unaukumbuka Muujiza Wa Bwana Yesu Kuwalisha Watu Wanaume Elfu Tano, Bila Kusahau Idadi Ya Wanawake Na Watoto? Tena Kwa Mikate Mitano Na Samaki Wawili?
“Akawaambia Mnayo Mikate Mingapi? Nendeni Mkatazame. Walipokwisha Kujua Wakasema, Mitano Na Samaki Wawili. Akawaagiza Wawaketishe Wote, Vikao vikao, Penye Majani Mabichi. Wakaketi Safu safu, Hapa Mia Hapa Hamsini. Akaitwaa Ile Mikate Mitano Na Wale Samaki Wawili, Akatazama Mbinguni, AKASHUKURU, Akaimega Ile Mikate, Akawapa Wanafunzi Wake Wawaandikie; Na Wale Samaki Wawili Akawagawia Wote. WAKALA WOTE WAKASHIBA. WAKAOKOTA VIPANDE VILIVYOMEGWA VYA KUWEZA KUJAZA VIKAPU KUMI NA VIWILI; NA VIPANDE VYA SAMAKI PIA. Na Walioila Ile Mikate Wapata Elfu Tano Wanaume” (Marko 6:38-44)

Ukiisoma Kwa Umakini Habari Hii Na Muujiza Huu Utagundua Jambo La Ajabu Sana. BIBLIA Haisemi ALIFUNGA NA KUOMBA Ili Muujiza Huu Utokee, La Hasha! Biblia Inaeleza Wazi Kuwa Yesu ALISHUKURU; ALIMSHUKURU MUNGU Na Muujiza Ukatokea!
Sijaribu Kukana Au Kukataa Ama Kupinga Nguvu Na Umuhimu Wa Maombi Katika Utendekaji Wa Miujiza, Hapana. Ila Nilitaka Uone Kilichotokea Hapa, Yesu Alishukuru Tu; Alionesha Imani Iliyo Moyoni Mwake Kuhusu Mungu Na Uweza Wake Wa Kutupatia Mema Na Mara Muujiza Ukatokea, Haleluyaah!

Je Unaukumbuka Muujiza Wa Kufufuliwa Kwa Lazaro, Yule Rafiki Wa Bwana Yesu Kule Bethania? Huyu Ndugu Alishakuwa Kaburini Kwa Zaidi Ya Siku Tatu… Lakini Kwa Kumshukuru Mungu, Na Kudhihirisha Ujasiri Na Imani Yake Kwa BWANA, Yesu Aliufanya Muujiza Huu!
“Basi Yesu, Hali Akiugua Tena Nafsini Mwake, Akafika Kwenye Kaburi. Nalo lilikuwa Ni Pango, Na Jiwe Limewekwa Juu Yake. Yesu Akasema, Liondoeni Jiwe. Martha, Dada Yake Yule Aliyefariki, Akamwambia, BWANA, ANANUKA SASA; MAANA AMEKUWA MAITI SIKU NNE. Yesu Akamwambia; MIMI SIKUKUAMBIA YA KWAMBA UKIAMINI UTAUONA UTUKUFU WA MUNGU? Basi Wakaliondoa Lile Jiwe. YESU AKAINUA MACHO YAKE JUU, AKASEMA, BABA, NAKUSHUKURU KWA KUWA UMENISIKIA…Naye Akiisha Kusema Hayo, Akalia Kwa Sauti Kuu, Lazaro, Njoo Huku Nje. Akatoka Nje Yule Aliyekufa, Amefungwa Sanda Miguu Na Mikononi, Na Uso Wake Umefungwa Leso. Naye Yesu Akawaambia, Mfungueni, Mkamwache Aende Zake” (Yohana 11:38-44)

Katika Muujiza Huu Pia Tumegundua Kuwa Yesu ALIMSHUKURU TU MUNGU, Akionesha Imani Yake Na Uhakika Wake Kwa Mungu, Na Muujiza Ukatokea!

Mungu Anaendelea Kutufundisha Kuhusu Siri Hii Iliyomo Ndani Ya Kushukuru Kupitia Kinywa Cha Mtumishi Wake Paulo, ” FURAHINI SIKU ZOTE; OMBENI BILA KUKOMA; SHUKURUNI KWA KILA JAMBO; MAANA HAYO NI MAPENZI YA MUNGU KWENU KATIKA KRISTO YESU” (1 Wathesalonike 5:16-18)
Ni Lazima Sana, Kwa Kila Mkristo Anayependa Kuyafanya Mapenzi Ya Mungu Kujenga Tabia Ya KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO.

Daudi Anatukumbusha Tena Juu Ya Hili Pia, Anasema, ” NI NENO JEMA KUMSHUKURU BWANA” (Zaburi 92:1)

Kama Unataka Kuidhihirisha Imani Yako Nje; Tutaangalia Kauli Zako, Tutayatazama Maneno Yako, Kama Umejaa Shukurani Za Dhati Kwa Mungu Kwa Yale Aliyokupa Sasa Na Hata Yale Unayoyatarajia Kwa Bwana!
“SHUKURANI HUVUTA MIUJIZA”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
8 comments on “FAHAMU UWEZA NA NGUVU YA KUSHUKURU
 1. MWL.EVODIUS YOHANA says:

  UBARIKIWE SANA MTUMISHI MUNGU AKUONGEZEE UFUNUO

 2. Edward S Mshana says:

  Kweli hapo nimejifunza kitu kipya katika imani kushukuru sio tu kwa nilivyovipata dhahiri katika ulimwengu wa mwili wa damu na nyama bali ni zaidi kuwa mtu wa shukurani kwa vile nivitarajiavyo kwa imani nimshukuru Mungu kana kwamba ninavyo tayari na kwa mapenzi ya Mungu itathibitika machoni pangu ili sifa na utukufu zimrudie yeye.Ameni

 3. Elinikunda says:

  Namshukuru Mungu aliyekuwezesha kutoa somo hili kwa Maana nimejifunza jambo kubwa sana la kumshukuru Mungu kila wakati na kila hali tuliyonayo bila kuchoka, na ndipo Neema , Upendo Wema na Baraka za Mungu zitazidishwa kwetu. Barikiwa Sana.

 4. Sam says:

  Shukrani kwa hili fundisho…mbarikiwe!

 5. JOSEPHAT says:

  nimefurahi sana MUNGU AWABARIKI

 6. tine says:

  Mshukuruni BWANA, kwa maaana fadhili zake ni za milele

 7. Pst David says:

  Fundisho La Ajabu, Bwana Akuinue

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: