Kanisa La Sasa Tuna “WANGOJA MIUJIZA” Wengi Kuliko “WATENDA MIUJIZA”

miujiza

tendeni

Wakati Yesu Anawalisha Wanaume 5000, Wanawake Na Watoto Wasio Na Idadi, HAKUOMBA ULE MUUJIZA TOKA MBINGUNI; Biblia Inasema YESU ALIJUA MWENYEWE ATAKALOTENDA (Yohana 6:6).
Yesu Hakujiuliza Mara Mbilimbili Kuhusu Wale Makutano, Alijua Atakachofanya!
Unakumbuka Wakati Wale Waombolezaji Wanampeleka Kumzika Mwana Wa Pekee Wa Yule Mjane? Yesu Alijua Nini Atakachofanya, Hakuomba Ili Yule Kijana Afufuke, Alisema tu, “Kijana Amka”

Unaweza Kusema, “Lakini Mwalimu, Yule Alikuwa Yesu, Hakuwa Mwanadamu Wa Kawaida, Alikuwa Mungu”
Uko Sawa Kabisa, Hujakosea, Ila Ukweli Yesu Alikuwa Kielelezo Ili Sisi Tujifunze Kwake (Mathayo 11:29), Alikuwa Hapa Dunia Akituonyesha Aina, Mfumo Na Kiwango Cha Maisha Tunachotakiwa Kuwa Nacho Kama Wana Wa Mungu Na Mabalozi Wa Serikali Ya Mbinguni Hapa Duniani.

Unamkumbuka Petro Na Yohana Na Habari Ya Yule Kiwete Aliyekuwa Kwenye Mlango Wa Mzuri? Matendo 3 na 4 Petro ALIJUA AWEZACHO NA ATAKACHOFANYA; HAIKUWA AJALI, HAIKUWA BAHATI.
Kwa Uhakika Petro Alimwambia Yule Kiwete, “… NIKUPACHO Ndicho Hiki, Kwa Jina La Yesu, Simama Na Uende”
Petro ALIJUA Nini ATAKACHOMPA. Hakuwa akibahatisha!

Unamkumbuka Paulo Na Yule Mchawi Elima? Paulo ALIJUA NINI ATAFANYA, ALIJUA NINI KINAWEZA KUWA. Bila Kujiuliza Uliza Aliamuru UPOFU UWE JUU YA YULE MCHAWI NA MPOTOSHAJI WA INJILI ELIMA, Na Ikatokea Palepale… Hakuwa Akibahatisha, Alijua Nini Anaweza Kufanya!

Kuna Kitu Kimekosa Kwa Kanisa La Sasa; Kwa Kizazi Chetu. Kile Kilichokuwa Kwa Yesu Na Kwa Mitume Kinakosekana Kwetu. Ndio Maana Wakitokea Watumishi Wa Mungu Walioijua Siri Ya Kufanya Kama Yesu Na Mitume, Wachungaji Na Viongozi Wa Dini Zetu Wanawainukia Na Kuwatukana Na Kuziita Zile Kazi Kuwa Ni Za Shetani. Wanawaita Majina Yote Wanayoweza, Ili mradi tu Kuwazuia Wasitembee Na Kutenda Kwenye Kiwango Hicho!

Nakuhakikishia Hizi Nyakati Tulizomo, Kuna Mambo Ambayo Macho Hayajawahi Kuona, Wala Masikio Kusikia, Wala Hayakuwahi Kuingia Kwenye Mioyo Ya Wanadamu, Mambo AMbayo Wale Wampendao BWANA, Wenye Muda Na Yeye, Neno Lake Na Ushirika Na ROHO WAKE Watayatenda!

Hizi Ni Zama Ambazo Roho Mtakatifu Yuko Kazini Isivyokuwa Kawaida, Anawatafuta Watu Wa Kawaida KAMA MIMI Ili Alete Mapinduzi Ya Mwisho Kabla Yesu Hajalinyakua Kanisa Lake.
Unaweza Kuwa MMOJA KATI YA WATU WATAKAOBEBA KIJITI HIKI Katika Nyakati Hizi Za MWISHO… Mungu Anawahitaji WENYE KIU, WANYENYEKEVU, WATAUWA, WALIOCHUKIA DHAMBI NA UOVU, WENYE HAKI NA WENYE HURUMA NA WANADAMU WENZAO WANAOTESWA NA IBILISI, Ili Awapake Mafuta (AWAPE UPAKO) Wasimame Na Kuifanya Miujiza Hapa Duniani Kwa Niaba Yake!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: