Motoni hau majini siyo mwisho wako

Naamini Mmezisoma Habari Za Wale Vijana Watatu Wa Imani; Shedraka, Meshaki Na Abednego… Hawa Kwa Sababu Ya Msimamo Wao Thabiti Wa Kusimamia Mapenzi Na Makusudi Ya Mungu Wao, Walitupwa Katika Tanuru La Moto. Lakini Moto Haukuwa Mwisho Wao (Danieli 3).

Ninaamini Pia Umezisoma Au Kuzisikia Habari Za Wana Wa Israeli Pale Bahari Ya Shamu, Na Pia Umezisikia Habari Zao Kule Mto Yordani. Katika Matukio Haya Yote Mawili Walipitia Kwenye MAJI. Lakini Maji Hayakuwagharikisha… Maji Hayakuwa Mwisho Wao!

Kama Ni Msomaji Wa Agano Jipya, Utakuwa Umekutana Na Habari Za Petro. Huyu Aliwahi Kumwambia BWANA YESU ampe ruhusa aje JUU YA MAJI. Biblia Inatueleza Kwa Uwazi Kwamba Petro Aliweza Kutembea Juu Ya Maji Japo Kwa Muda Kidogo Ingawa Alianza Kuzama Baada Ya Kutoa Jicho Lake Kwa Yesu Na Kuyatazama Mawimbi. Lakini Mbali Ya Changamoto Hiyo, MAJI HAYAKUWA MWISHO WA PETRO!

Kwenye Maisha Haya, Mungu Hajatuahidi Kwamba Hatutapita Kwenye Maji Au Kwenye Moto, HAPANA… Ila Ametuhakikishia Kuwa MAJI HAYATATUGHARIKISHA wala MOTO HAUTATUUNGUZA WALA KUTUTEKETEZA Maana Yeye Mwenyewe; MUNGU ALIYE HAI, ATAKUWA PAMOJA NASI (Isaya 43:2).

Ni Muhimu Tumjue Kwa Undani Mungu Wetu Na Uaminifu Wake Kwetu, Na Kama Ayubu Tuseme, ” Lakini Yeye [Mungu] Aijua Njia Niiendeayo; Akiisha Kunijaribu, Nitatoka Kama Dhahabu” (Ayubu 23:10)

Mungu Anataka Ujue Kuwa Majini Au Motoni (Jaribu/ Changamoto Uliyonayo) Si Mwisho Wako, Inapita Na Ina Mwisho. Na Kama Ukivumilia Na Kumwamini Mungu Na Neno Lake Kwa Kwa Moyo Wako Wote, Utatoka Salama Na Kuna Kuinuliwa Hatimaye!

Daudi Anaelezea Uzoefu Wake Katika Maisha Ya Imani, ” Tulipita MOTONI NA MAJINI; Ukatutoa Na Kutuleta Kunako Wingi (Kwenye Ustawi Na Utele)” (Zaburi 66:12).

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “Motoni hau majini siyo mwisho wako
  1. Godfrey Maendeleo says:

    ubarikiwe

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: