HAKUNA UKRISTO BILA NGUVU YA MUNGU

nguvu ya mungu

Hauwezi Kumtenganisha Mkristo Na Nguvu Ya Mungu, Ni Sawa Na Samaki Na Maji, Sawa Na Mizizi Na Ardhi, Ama Pumzi Na Mtu!

“Bali Wo

te Waliompokea Aliwapa Uwezo [Nguvu] Ya Kufanyika Wana Wa Mungu, Ndio Wale Waliaminio Jina Lake” (Yohana 1:12)

Hauwezi Kuwa Mkristo na Kuishi Maisha Ya Ushindi Dhidi Ya Shetani, Dhambi Na Changamoto Kama Hauna Nguvu Ya Mungu!

Hatuokoki Kwa Kusema Tu Maneno Midomoni BILA NGUVU YA KUTUFANYA WANA WA MUNGU, Katu na Abadani! Kama Huna Nguvu Ya Mungu, Wokovu Hauwezekani… Kuishinda Dunia na Tamaa Zake Kwako huo Utakuwa Ni Msamiati Mgumu!

Ndio Maana Mtu Wa DINI (Mshika Dini, Mapokeo Na Taratibu za Wanadamu) Hawezi Kuamini Kwamba Mtu Anaweza Kuokoka Akiwa Duniani, Hii Ni Kwa Sababu Mtu Wa Dini Hajakutana Na NGUVU YA MUNGU Inayotufanya Sisi WALIOOKOKA Kuwa INVICIBLE… Anadhani Kwa sababu Yeye ameshindwa Kumshinda Shetani Na Dhambi na tamaa za Dunia Hii, Na Wengine wote tumeshindwa!

Asikudanganye Mtu, Nguvu Ya Mungu Inapatikana Bure Kwa Mungu Mwenyewe… Mwenye Kiu aje Anywe Bure, Aje Anunue Divai (Roho Mtakatifu) na Maziwa (Neno) (Isaya 55:1-2, Yohana 7:37-39)!

Nguvu Ya Mungu tunaipata wapi?

 1. Kwenye Neno Lake          Waebrania 4:12 “Kwa Maana Neno La Mungu LI HAI, TENA LINA NGUVU…” Yohana 1:3 “Vitu Vyote Vilifanyika Kwa NENO LA MUNGU. Pasipo NENO HAKUNA CHOCHOTE KILICHOFANYIKA” Yeremia 23:29 “NENO LA MUNGU NI KAMA MOTO, NI KAMA NYUNDO IPONDAYO MIAMBA KUIFANYA VIPANDE VIPANDE” Kama Ukiamua Kutumia MUDA WAKO, NGUVU YAKO, GHARAMA YAKO YA KIFEDHA nk Kutafuta NENO LA MUNGU Utakutana Na Nguvu Ya Mungu Ya Kubadili Maisha Yako! Tumia Muda wako: Kujisomea Mwenyewe NENO LA MUNGU Kwenye Biblia Yako. Pia Kama Kuna SEMINA Za Neno la Mungu Na Mafundisho Usikose… Wekeza Muda Wako katika Neno Utakutana Na Nguvu ya Kuyabadili Maisha Yako! Tumia PESA YAKO Kununua VITABU VYA WATUMISHI WA MUNGU VYA MAFUNDISHO Mbalimbali Ya Neno La Mungu… Nunua CD, DVD Za Mafundisho Ya Neno La Mungu Kwa Kadri Mungu atakavyo kuwezesha… Nakuhakikishia Ukiweka Pesa Yako Katika Neno lililo Kwenye Vitabu Na CD, DVD Za Watumishi Wa Mungu WALIOITWA NA WALIOTUMWA NA MUNGU, Maisha Yako Hayatabaki vile yalivyokuwa!.
 2. Maombi         Wekeza Muda Wako Kwenye Maombi. Zama tulizomo Hizi Ni za Hatari sana. Shetani yuko Kazini Kuliko Wakati Mwingine Wowote. Tuko Katika Nyakati za Mwisho. Ni nyakati ambazo wale walio MAKINI KWENYE MAOMBI Na Kumsikiliza Mungu WATASALIMIKA. Hakikisha Unakuwa[..] na Muda Wa Kutosha Kwenye Maombi. Usisingizie kwamba Uko Busy au Muda haupo. Huu ni UONGO WA IBILISI. KUNA MAMBO MENGI UNAFANYA YASIYO NA TIJA Ambayo kama UKIYAACHA au KUPUNGUZA MUDA WAKE, Utapata muda wa kutosha wa KUOMBA. Kuna Wakristo Wengi kuomba Hata NUSU saa tu kwao ni kazi sana. Ni sawa na ADHABU. Lakini kwakweli ni mbinu ya SHETANI TU hii. MAMBO YA KUOMBEA NI MENGI SANA; Familia yako (ndoa; mme/mkeo, watoto), dada na kaka zako, ndugu wengine ulionao, Kanisa lako, Watu waokoke, Yesu apate heshima yake, miujiza, ishara na maajabu viwepo kwenye Ibada zenu, Maisha yako pia yanategemea sana maombi yako kwenda kule ambako Mungu anatamani yaende. Kama Hauombei Maisha yako, Unamruhusu Shetani aingilie na kupitisha AGENDA zake za UHARIBIFU, KUIBA NA KUCHINJA (Yohana 10:10), Unapoyaombea Maisha yako UNAJIWEKEA ULINZI (Zaburi 32:6, Mathayo 26:41-44), Ombea TAIFA LAKO; Mambo yote mabaya au mazuri ndani ya taifa lako ni matokeo ya ULIMWENGU WA ROHO; UKIOMBA UTABADILI NCHI YAKO, UTALIPONYA TAIFA LAKO (2 Nyakati 7:14)
 3. Kufunga              Jitahidi Uanze Kujizoeza MAOMBI YA KUFUNGA pia; anza kwa kufunga maombi ya saa 12 (asubuhi hadi jioni)… walau hata mara 2 au 3 kwa wiki. Halafu baada ya hapo Mungu atakusaidia kuweza Kufunga maombi ya Siku nzima (masaa 24), baadaye utakavyozidi kukomaa utaweza kufunga siku 3, 7 nk kutegemea maendeleo yako katika SHULE YA MAOMBI NA KUFUNGA. KUFUNGA NA KUOMBA HUACHILIA NGUVU NA UPAKO WA KUVUNJA Vifungo vya Kiroho kama LAANA, DHAMBI, KUTOFANIKIWA nk (Isaya 58:5-9)
 4. Ushirika Wako Na Roho Mtakatifu        “Neema Ya Bwana Wetu Yesu Kristo, Na Upendo Wa Mungu Baba, NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU, Ukae pamoja nasi, sasa na hata milele, amen” (2Wakorintho 13:14) Roho Mtakatifu Ni: Mwalimu: Anatufundisha mambo yote ( Yohana 14:26, 1Yohana 2:27) Kiongozi: Anatuongoza Na Kututia katika Kweli Yote (Yohana 16:13-15, Warumi 8:9-16) Shahidi: Anatushuhudia juu ya dhambi tukikosea au kutenda dhambi na kutukumbusha kutubu LAKINI Pia Anatushuhudia mioyoni mwetu kuwa sisi ni WANA WA MUNGU (Yohana 16:7-8, Warumi 8:16) Msaidizi: Roho Mtakatifu Ni Msaidizi wetu, anatusaidia kuyaendesha maisha ya Imani kwa uhakika na ushindi (Yohana 14:16) Roho Mtakatifu ni Roho Wa NGUVU, UWEZA, SHAURI, HEKIMA, UFAHAMU, UCHAJI MUNGU, UPENDO, KIASI ( Isaya 11:1-2, 2Timotheo 1:7) Tangu Siku ya Pentekoste, ROHO MTAKATIFU yuko Hapa Duniani, Anakaa na WAAMINI, ANAKAA NDANI YAO( Yohana 14:17)

Utakavyozidi KUMPA NAFASI, KUMPENDA, KUMTHAMINI na KUWA NA USHIRIKA NAYE, Utafurahia NGUVU YA MUNGU muda wote! (TAFADHALI CHUKUA BIBLIA YAKO NA USOME MISTARI YOTE NILIYOANDIKA KATIKA STATUS HII) Ubarikiwe!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
7 comments on “HAKUNA UKRISTO BILA NGUVU YA MUNGU
 1. daniel says:

  Ubarikiwe mtumishi endelea kuweka masomo zaidi mungu akubariki sana

 2. johnson solomon says:

  amen, nimebarikiwa na neno hilo, Mungu Awabariki

 3. martha selemani says:

  amen ubarikiwe kwa kufundisha neno hili nimejifunza mengi

 4. Robert says:

  Ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu. Umetulisha chakula kitamu cha Roho zetu.

 5. ISAYA says:

  UBARIKIWE SANA MTUMISHI WA MUNGU. NIMEJIFUNZA MENGI NA NIMEPIGA HATUA NZURI KATIKA WOKOVU.

 6. MSAWA YONA JORAM says:

  BLESSES

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: