Maana halisi ya wokovu

https://yesunibwana.files.wordpress.com/2013/01/you_must_born_again_draft.jpg?w=300

unatakiwa uokoke

Vijana Wengi Ambao Nimekutana Nao Na Kuwashhudia Habari Za Yesu Na Swala Zima La Kuokoka, Wanaelewa Umuhimu Na Uzuri Wa Kuokoka Ila HAWATAKI KUWA WANAFIKI; Hawataki Kuokoka Halafu Baada Ya Muda Wakaonekana Wamerudi Dhambini Tena.
Mioyo Yao Inatamani KUMPA YESU NAFASI lakini Wasiwasi Wao Unakuja Kwenye Swala La KUKIDHI VIWANGO VYA UFALME WA MUNGU… Wengi Wanasema KULIKO KUOKOKA HALAFU WAKARUDI TENA KUTENDA DHAMBI, NI BORA WASIOKOKE NA WAENDELEE NA MAISHA YAO YA DHAMBI Kuliko Kuwa WAIGIZAJI Kama WALOKOLE Wengi Wa Siku Hizi!

Tarehe 19/01/2013 Kwa NEEMA YA MUNGU Nitakuwa Natimiza Miaka 10 Tangu Nilipofanya MAAMUZI BORA KULIKO YOTE DUNIANI YA KUMPA YESU MAISHA YANGU AWE BWANA NA MWOKOZI WANGU a.k.a KUOKOKA.

Ujumbe Huu Nimeuandika MAKUSUDI KABISA Kwa Wale Wote Mnaojua UMUHIMU NA ULAZIMA WA KUOKOKA, Lakini Mmekuwa MNAKWAMA Kufanya Maamuzi Kwa Kuhofia Kwamba HAMTAWEZA KUUTUNZA WOKOVU Na Kuishi Maisha Ya Kumpendeza Mungu, JAPO MNAELEWA FIKA KWAMBA MKIFA LEO HAMNA UHAKIKA NA UMILELE WENU… HII NI SAUTI YA MUNGU KWENU, ZINGATIA UJUMBE HUU NA UUTENDEE KAZI!

WOKOVU NI NINI?

Wokovu Ni MFUMO WA[..] MAISHA, Ambapo Mwanadamu Mwenye DHAMBI NA MAPUNGUFU Anapata Fursa Ya Kuwa Mtu Wa Nyumbani Kwa Mungu (Waefeso 2:19). Anapata Nafasi Ya Kuwa Mwakilishi/ Balozi/Mjumbe Wa Serikali Ya Mungu (2Wakorintho 5:20). Anapata Nafasi Ya Kuwa Wakili Wa Siri Za Mungu (1 Wakorintho 4:1). Anapata Nafasi Ya Kuwa Mtawala Hapa Duniani Kwa Niaba Ya Serikali Ya Mbinguni (Ufunuo 5:9-10). Anapata Nafasi Ya Kuamua Mambo Yanayotokea Duniani; Analolifunga Duniani Linafungwa Mbinguni, Analolifungua Duniani Linafunguliwa Mbinguni (Mathayo 16:19, Mathayo 18:18).

Hayo Yote Hapo Juu Yanatokea MARA TU Baada Ya Mtu Kufanya UAMUZI WA IMANI WA KUYATOA MAISHA YAKE KWA YESU, NA KUKUBALI MOYONI MWAKE KWAMBA YESU AMELIPIA DENI YA DHAMBI ZAKE NA KUAMINI HILO MOYONI MWAKE (Kwakuwa Haumwoni Yesu Pale Kwa Macho Wakati Unafanya Maamuzi).
Na Tokea Hapo, KAMA MTU HUYU AMEFANYA MAAMUZI YA DHATI NA YA KUMAANISHA MBELE ZA MUNGU; Ghafla Anapokea NGUVU YA MUNGU YA KUMFANYA KUWA MWANA WA MUNGU (Yohana 1:12) Na Baada Ya NGUVU Hii Kuingia Ndani Yake, Mtu Huyu Anajikuta AMEKUWA NA HASIRA NA CHUKI DHIDI YA MAISHA YA DHAMBI, ANAPATA ALLERGY NA DHAMBI, NA NDANI YAKE INATOKEA KIU YA DHATI YA KUMPENDEZA MUNGU NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU. Mtu Huyu VIPAUMBELE VYAKE VINABADILIKA, ANAANZA KUTAMANI MARA ZOTE KUMTANGULIZA MUNGU NA KUMFURAHISHA MUNGU… Kwakweli Ni Maisha Mapya Kabisa Ambayo UZIMA WA MUNGU, UZIMA WA MILELE UNAINGIA NDANI YA MTU KUMFANYA AWE NA BADILIKO NA KUWA NA MAISHA MASAFI NA YA UTAKATIFU, JAMBO AMBALO HALIKUWEPO KABLA YA KUOKOKA (Najua Unaelewa Haya Ninayoyasema Maana Utakuwa Umewaona Ndugu, Marafiki, Wazazi, Mme/Mke, Jamaa Ambao Wamebadilishwa Na NGUVU YA MUNGU, NGUVU YA WOKOVU Na Kuwa Watu SAFI NA BORA Kabisa, Kiasi Cha Hata Wewe Au Watu Wengine Wanaomzunguka Kutamani Kuwa Kama Yeye).
Hiki Ndicho Ninachokizungumzia, Huku Ndiko KUOKOKA KWENYEWE, TABIA NA ASILI YA MUNGU KUINGIA NDANI YA MWANADAMU NA KUMFANYA KIUMBE KIPYA KABISA!

NAMNA YA KUISHI MAISHA YA WOKOVU; MATAKATIFU NA YA KUMPENDEZA MUNGU NA WANADAMU

Watu Wengi Wanaoogopa Kuokoka Wanadhani KUOKOKA Kunategemea JITIHADA ZAO BINAFSI KUMPENDEZA MUNGU NA KUTII AMRI ZAKE, HUU SI UKWELI, NI UONGO!

KWENYE KUOKOKA Wewe Unashiriki Hasa KWENYE KUFANYA MAAMUZI YA KUMPOKEA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI, Halafu Tokea Hapo, Mungu Kupitia ROHO WAKE MTAKATIFU Anaweka MAKAO NDANI YAKO, NA ANAANZA KUTENDA KAZI NDANI YAKO, KUTAKA KWAKO NA KUTENDA KWAKO KWA AJILI YA KUSUDI LAKE JEMA (Wafilipi 2:13).
Yeye Ndiye Anayekupa Msukumo Wa Ndani Wa Kuyaendesha Maisha Na Namna Ya Kuyaendesha Kwa Ufasaha.

KUMBUKA: Mungu Mwenyewe Ndiye MWANZILISHI wa WOKOVU wako Na Ndiye Anayesimamia Na Kuliendesha Zoezi Zima La Wewe Kuyatoa Maisha Yako Kwa Yesu… YESU ANASEMA HAKUNA AJAYE KWAKE ASIPOVUTWA NA BABA YAKE [MUNGU]… Kwahiyo Hata Mtu Kuchukua Uamuzi Wa Kuokoka Ni Kwa Msaada Na Uwezesho Wa Mungu Mwenyewe. Hivyo Mungu Ndiye Anayekuwa MWANZILISHI NA PIA ANA WAJIBU WA KUTIMIZA ALICHOKIANZISHA NDANI YAKO HADI SIKU YA KURUDI KWA YESU (Wafilipi 1:6)

KWA HIYO BASI: Usiogope Kufanya Uamuzi Wa Kumpokea Yesu Na Kuokoka, Maana MARA TU Baada Ya Kuokoka Kwako, Mungu Anachukua Usukani Ndani Yako Na Kuanza Kukusaidia Kuishi Maisha Matakatifu, Huu ndio Ukweli Kaka/ Dada Yangu, Mie NIMEKUWA SHAHIDI WA HILI KWA MIAKA 10 Sasa, Kama Mungu Amenisaidia Nimeweza Kuokoka Na Nimedumu Kwenye Wokovu Kwa Muda Wote Huu Na Wanaonijua Na Kunizunguka Ni Mashahidi Wanaona Maisha Mapya Ya Ushindi Niliyonayo Na WANAWEZA KUSIMAMA NA KUSEMA KWA UHAKIKA KWAMBA “DICKSON AMEOKOKA”

Shetani Anatumia NJIA YA KUKUHUBIRIA MOYONI MWAKO KUWA HAUTAWEZA, UTARUDI NYUMA, UTARUDI TENA DHAMBINI, Lengo lake Anataka Usifanya UAMUZI. Maana ANAJUA Ukikata tu Shauri KUOKOKA, Utapata MSAADA WA MUNGU NA HAUTARUDI TENA DHAMBINI… Amua Leo, Okoka dada/kaka, Hii Ni Fursa Yako, Mungu atayahifadhi Maamuzi Yako Na Utakuwa na Maisha Ya Amani Na Ushindi Kila Siku Hapa Duniani!

KUOKOKA NDIO FASHENI ILIYOBAKI HAPA DUNIANI, WAJANJA WOTE TUKO HUKU, CHUKUA HATUA, FANYA MAAMUZI, NJOO KWA YESU!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: