Wanadamu watakusifia

Linapokuja Swala La Maisha Yako Hapa Duniani, Wanadamu Watakusifia Au Watakusema Vibaya Bila Kuwa Na Ushahidi Wa Kweli… Ukienda Misibani Ndiko Kumejaa Usanii Kweli… Viongozi Wa DINI kwa Kutaka “Kuwafariji” Waombolezaji Na Wafiwa Utasikia Wanasema, “Marehemu Alikuwa Kijana Mwema Kweli, Alipenda Maendeleo Na Kusaidia Wengine, Lakini Leo Ametangulia, Amekwenda Kupumzika Kwenye Nyumba Yake Ya Milele, Tutamwona Mbinguni”
Sio Rahisi Namna Hiyo, Kuna Mashahidi Watatu Wanaojua Maisha Yako Ya Sasa Yamekaaje Na Uko Upande Gani Kwa Sasa!
Mashahidi Hao Ni MOYO WAKO, MUNGU NA SHETANI…
Moyo Wako Ni Shahidi Mwaminifu; Unajua Wapi Umejisajiri, Unajua Wazi Kama Ukifa Leo Unakwenda MBINGUNI ama JEHANAMU.
Mungu Pia Anajua; Anajua Kama Wewe Ni Wake Au Ni Wa Upande Wa Pili.
Shetani Pia Anajua: Anajua Wazi Kama Wewe Ni Wake Ama Ni Wa Mungu.

Hawa Wanadamu Wengine Waliobaki Ni Wapambe tu… Maoni Yao Mema Au Mabaya Hayabadili Upande Uliopo.

Mwenye Uwezo Wa Kutengeneza Maisha Yake Ni Mhusika, Mwenye Maisha, WEWE MWENYEWE!
Na Muda Pekee Wa Kutengeneza Maisha Yako Ni WAKATI UNAISHI, UKIKATA TU ROHO YAKO; UMEINGIA TAYARI KWENYE MAISHA YA MILELE, MBINGUNI AU JEHANAMU; YAANI NI KUFUMBA NA KUFUMBUA, UNAJIKUTA SEHEMU MOJAWAPO KUTEGEMEA NA UHUSIANO WAKO NA BWANA YESU ULIPOKUWA HAI DUNIANI!

Ninatamani Kukutana Na Wewe Mbinguni, Sitamani Tuishie Kuwa Marafiki Hapa Duniani, Maisha Ni MARA MOJA TU; HAYANA MAPUMZIKO [HALF TIME] UKIONDOKA UMEONDOKA.

Nataka Nikupe Siri Ya Maisha; Mpe Yesu Maisha Yako, Kubali Awe BWANA NA MWOKOZI WAKO… Mimi Nitakusaidia Namna Ya Kukua Kiroho Na Namna Ya Kuishinda Dhambi… Kama Unataka KUMPA YESU MAISHA YAKO YAANI KUOKOKA ILA UNA CHANGAMOTO ZINA KUZUIA KUOKOKA, NJOO KWENYE SEHEMU YANGU YA MESEJI, NITAKUSAIDIA… SI MAPENZI YA MUNGU WEWE KWENDA JEHANAMU, TUMIA NAFASI HII VIZURI!
Ubarikiwe.

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: