Eee Bwana Usitete Nao Wanaoteta Nami, Wala Usipigane Nao Wanaopigana Nami… Maana Inatisha Sana Kwa Mwanadamu Kuangukia Katika Mikono Yako… Wote Wanaoshindana Nawe Huwa Hawachomoki; Hupondwa pondwa Kabisa… Pumzi Zako Zasukuma Na Kutawanya Bahari… Mikono Yako Yasaga Milima Na Kufikicha Vilima, Mbingu Nzima Ni Kiti Chako Cha Enzi, Dunia Nzima Na Ukubwa Wake Wooote Ni Mahali Pako Pa Kuweka Miguu Yako Miwili Tu… Usipigane Nao Bwana, Maana Hata Utukufu Na Uwepo Wako Tu Unatisha Sana… Badala Ya Kupigana Nao Bwana, Nakuomba Unipe AKILI, MAARIFA, UFAHAMU NA HEKIMA Kuliko Wao… Maana HEKIMA Yako Ni Ulinzi Kwake Aipataye… Nikiwa Na HEKIMA Yako Tu, Nitajua Namna Ya Kutoka Na Kuingia Kwangu… Nitaweza Kula Chakula Ulichoniandalia Machoni Pa Watesi Wangu… Nitaweza Kuenenda Kwa Ufanisi Kama Kondoo Katikati Ya Mbwa Mwitu… Nikiwa Na HEKIMA Yako; Nitajua Wakati Gani Wa Kuwa Mpole Kama Hua Na Wakati Gani Wa Kuwa Mjanja Kama Nyoka… Nitajua Namna Ya Kuteta Na Adui Langoni… Haya Ni Maombi Yangu Kwako BWANA, Usiwapige Adui Zangu, Nawahitaji Kwa Ajili Ya Kunipa Changamoto Kwenye Maisha, Nawahitaji Maana Wao Ni Ngazi Za Kupandia Kuelekea Ukuu; Eee BWANA, Kwa Pendo Lako Nawapenda Adui Zangu, Hivyo Kumbuka Rehema Kwao, Maana Wao Ni Mavumbi Tu Bwana… Haina Haja Kwa MFINYANZI Kushindana, Kuteta Au Kupigana Na UDONGO; Ahsante Baba Kwa Kunisikia, Asante Kwa Kujibu Hoja Zangu, Kwa Jina La Yesu Aliye Hai, Amen!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in sala

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: