KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA

https://i1.wp.com/s2.hubimg.com/u/2106957_f260.jpg

kupanda na kuvuna

Kinachowafanya Wakristo Wengi Waliookoka Washindwe Kufanya Vizuri Kwenye Maswala Ya Maisha Ni Kule Kushindwa Kuelewa KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA!
Ni Kweli Kabisa Kuwa Mungu Anapenda Wakristo Wafanikiwe Na Kustawi; Kila Walifanyalo Lifanikiwe Kama Miti Iliyopandwa Kando Ya Vijito Vya Maji (Zaburi 1:3, Yeremia 17:7-8).
Lakini Tatizo Kubwa Walilonalo WANA HARAKA SANA; Wanataka WAKIPANDA MBEGU LEO, WAKUTE KESHO ZIMEOTA, NA KESHOKUTWA WAVUNE… Hii HAIWEZEKANI, SI SAWA!

Hata MBEGU za Kawaida Kule Mashambani HAZIOTI NA KUVUNWA NDANI YA WIKI 1 AU MWEZI MMOJA… Ni Zaidi Ya Hapo.

Ukiona NENO LA MUNGU Linakuhimiza KUWAPA WENGINE VITU ILI NAWE UPATE KUPOKEA TOKA KWA WATU (Luka 6:38), Haimaanishi Utapokea Palepale Kile Ulichotoa Kwa Wengine. Japo Wakati Mwingine BWANA Anaweza Kukupa Kile Ulichotoa Palepale, Ndani Ya Siku Hiyohiyo. Lakini Mara Nyingi Inachukua Muda Kutokea Kwako.

UNAPOTOA KITU KWA MTU KAMA MBEGU; Maana Yake UMEFANYA UWEKEZAJI KWENYE UFALME WA MUNGU. UMEWEKA HAZINA YAKO KWENYE BENKI YA MBINGUNI KWA AJILI YA KESHO YAKO [FUTURE]… “Maana Pale Hazina Ya Mtu Ilipo Ndipo Na Roho Yako Itakapokuwa… Basi Wekeni Hazina Zenu Mbinguni Pasipokuwa Na Nondo Wala Kutu, Wala Wezi Hawavunji Na Kuiba”

BIBLIA INASEMA UNAPOMPA MASIKINI [MHITAJI, ALIYEPUNGUKIWA] UNAKUWA UMEMKOPESHA MUNGU.

“Amhurumiaye Masikini Humkopesha BWANA; Naye ATAMLIPA Kwa Tendo Lake Jema” (Mithali 19:17)

Hapa Duniani, Kama Taasisi Ya Kifedha Kama Benki, Saccos, Vicoba Wakikukopesha Kiasi Fulani Cha Fedha, LAZIMA UKIRUDISHE KIKIWA PAMOJA NA RIBA(FAIDA YA ZIADA)… Ndivyo Ilivyo Hata Kwa BWANA, Unapoyagusa Maisha Ya Wengine, HAKIKA MUNGU NAYE ANAKUWA COMMITTED Kwa Ajili Ya Maisha Yako, Anakuwa Tayari Kuwa Mchungaji Wako Mwema Ili Ahahakikishe HAUPUNGUKIWI, NA HATA WAZAO WAKO WASIOMBEOMBE (Zaburi 23:1-6, Zaburi 37:25-26).

UNAPOMPA MTU KITU Awe Mchungaji Wako, Askofu, Mtumishi Fulani Wa Mungu, Masikini, Yatima, Mjane nk USIWE NA WAZO LA KUPOKEA HAPO KWA HAPO, JAPO BWANA ANAWEZA KUKUPA HAPO KWA HAPO, LAKINI NDANI YAKO UWE NA UHAKIKA KUWA UMEWEKEZA KWENYE UFALME WA MUNGU, NA KWENYE UFALME WA MUNGU KUVUNA NI LAZIMA!

Je Wewe Ni Masikini Sasa? Una Mahitaji Mengi Kwenye Maisha? Unapungukiwa Na Haujauona Utoshelevu? HATA MIMI NAZIPITIA CHANGAMOTO HIZI; LAKINI USIACHE KUTOA SADAKA, USIACHE KUWAPA WATUMISHI WA MUNGU VITU VILIVYO NDANI YA UWEZO WAKO, USIACHE KUWAPA KIDOGO ULICHONACHO YATIMA NA WAJANE, USIACHE KUWAKUMBUKA MASIKINI KWA HICHO ULICHONACHO… “Usiache Kutenda Mema, Maana Utavuna Kwa Wakati Wake Usipozimia Roho (Usipochoka Na Kukata Tamaa Kwenye Eneo La Kutenda Mema)”

Miaka Michache Sana Ijayo, Sisi WAPANZI TUTAVUNA TU… “MUNGU HADHIHAKIWI, APANDACHO MTU NDICHO ATAKACHOVUNA, APANDAYE UHARIBIFU ATAVUNA UHARIBIFU, APANDAYE HABA ATAVUNA HABA”

Mpende Mtumishi Wa Mungu ANAYEKUHIMIZA KUTOA SADAKA… Mpende Sana Mtumishi Wa Mungu Anayekuonesha Fursa Za KUPANDA MBEGU. Huyo Anakuonesha Mahali pa KUWEKEZA!

Je Bado Unanipenda Mwanafunzi Wangu Mzuri?

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
2 comments on “KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA
  1. stephen msalale says:

    MUNGU hahitaji tu kwamba tulisikie neno bali hutuhitaji tutamani nguvu kutoka kwake ya kutusukuma kulifanya hilo neno,naam KULIISHI

  2. John Kifaru says:

    We mwalim mzuri. Hongera.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: