NITAKUWA KIJANA MILELE

Sijawahi Kufikiria Kuhusu UZEE… Nitakuwa KIJANA Siku zote… Kuongeza Miaka Hakutabadili Mie Kuwa Kijana… Neno La Mungu Linanihimiza Nimkumbuke Mungu Katika SIKU ZA UJANA (Mhubiri 12:1)… Nimeshafanya UAMUZI Wa KUMKUMBUKA NA KUMUISHIA MUNGU Hadi Pumzi Yangu Ya Mwisho… Hii Inamaanisha Nitakuwa KIJANA HADI NIMALIZAPO MAISHA YA HAPA DUNIANI… Hata Kama Nitakuwa Na Miaka 120 Kama Musa, Nitakuwa KIJANA Bado… Nitakuwa Na MACHO Yasiyo Na Miwani… MIGUU Myepesi Kama Kurungu… AKILI Yenye Uwezo Wa Kutofautisha MZALIWA WANGU WA KWANZA NA KITINDA MIMBA Na Wajukuu Zangu Kama Alivyokuwa Mzee Yakobo Kwenye Mwanzo 49… Nitakuwa Na Uwezo Wa Kwenda Vitani Na Kuteka Nyara Hata Niwapo Na Miaka 85 Kama Kalebu… Nitakuwa Na Uwezo Wa Kuwaweka Chini Washirika Wangu Na Watu Wa Nyumba Yangu Na Kuwauliza NI NANI WATAKAYEMTUMIKIA Kama Alivyofanya Joshua Akiwa Na Miaka 110… Sihitaji Kuwa Na Mke Anayedhani Kuwa Mungu Anataka Tuwe Na Miaka 70 au 80 Tukiwa Na Nguvu, Maana Atanifanya Niishi Zaidi Ya Miaka 50 Peke Yangu Tangu Atakapofariki… After All; Mungu Amenihakikishia Ya Kwamba ” ATAUREJEZA UJANA WANGU KAMA TAI” (Zaburi 103:5)!

Hapa Kuna Watu Watakuwa Wamenikasirikia; Watakuwa Wanasema; Huyu Dogo Ana Majivuno, Anadhani Anampangia Mungu Ratiba? Hajui Kuwa Mungu Ndiye Anayeamua Kila Kitu?
Mko Sawa Kabisa, Ila Msisahau Kuwa, “MUNGU HAWEZI KUVUKA MPAKA WA NENO LAKE, HATENDI LOLOTE NJE YA NENO LAKE” Na Kila Nilichoandika Hapo Juu Ni Neno La Mungu Tu… Ni Ripoti Ya Mbinguni… Kwa Wanaojua, Wanaelewa!

++ I WILL BE FOREVER YOUNG, THE OLD OF ANCIENT LIVES IN ME++

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: