UNAWEZA KUWA BORA KWA KIWANGO KILEKILE ALICHOKUWA NACHO YESU

yesu kristo

Wakristo Wengi Wanadhani Kile Alichofanya Yesu Hakiwezekani Kufanywa Na Mtu Wa Kawaida Kama Au Wewe… Hiyo Si Kweli, Yesu Mwenyewe Anasema, TUNAWEZA KUFANYA YOTE ALIYOFANYA, NA HATA MAKUBWA KULIKO HAYO, KAMA TUKIMWAMINI (Yohana 14:12).
Lakini Hauwezi Kusema Kuwa UNAMWAMINI YESU; Kama Hauishi Na Kufanya Kama Yeye Alivyofanya. Huo Utakuwa Ni UNAFIKI tu. Leo Nataka Uyajue Baadhi Ya Mambo Ya Msingi Yaliyomfanya Yesu Aweze Kutenda Maajabu Hapa Duniani. Na Kama Ukiyatenda Pia, Yatakupa Matokeo Kama Aliyokuwa Nayo Yesu; Maana Ni KANUNI ZA KUDUMU Zinazofanya Kazi Kwa Kila Mtu… Karibu Ujifunze!

Kati Ya Mambo Yaliyomfanya Yesu Awe Wa Aina Yake Hapa Duniani Na Aache Alama Hapa Duniani (Legacy) Isiyowezwa Kufutwa Kwenye Huduma Yake Na Maisha Yake Kwa Ujumla, Ni Pamoja Na:

1.Alijua Uhusiano Wake Na Mungu, Na Hakuona Haya Kusimama Mbele Za Watu Kuutaja Na Kuueleza Wazi (Yohana 5:17-47, Yohana 6:32-40)

Yesu Alijua Mungu Ni BABA YAKE Na Alisimama Mbele Ya Watu Pasipo KUMUNG’UNYA MANENO Na Kueleza Kuhusu Hilo. HAKUJALI KWAMBA WATABISHA, WATAMPINGA, WATAMBEZA AU KUSEMA ANAJIDAI AU KUJIKUZA… Alisema Kile Anachojua, Bila Kujali Nini Kitampata.[..]

Wakristo Wengi Waliompokea Yesu; Kwa Lugha Rahisi Waliookoka Wanakosa Ujasiri Wa Kusimama Mbele Za Wazazi Wao, Ndugu Zao, Marafiki Zao, Jamaa Zao, Na Watu Wanaowazunguka Na KUTANGAZA KWA UJASIRI KWAMBA WAMEOKOKA NA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO… Wanaogopa; MANENO, VIJEMBE, KEBEHI, MATUSI, KASHFA, VIPIGO, KUFUKUZWA AU KUTENGWA nk… Ila Kwangu Mimi Dickson; NIMEOKOKA, YESU KRISTO NI BWANA WANGU NA MWOKOZI, MUNGU NI BABA YANGU… Sioni Haya Kusema Hili, Wote Wanaonijua Na Kunizunguka Wanajua MIMI SI MTU WA KAWAIDA, MUNGU ANAKAA NDANI YANGU… Simwogopi Yeyote Wala Lolote. Niko Tayari Kwa Lolote Maana NI MTU WA NYUMBANI KWA MUNGU.

2.Alijua Kuwa Yeye Si Wa Dunia Hii, Alijua Kuwa Yeye Ni Wa Juu
Na Alilitangaza Hilo Kila Alipokuwa Na Kila Alipopata Nafasi Ya Kusema Na Watu. Wala Hakuhofia Lolote (Yohana 3:31, Yohana 6:33-37)

Wakristo Wengi Wa Sasa, Wala Hawajui Wao Ni Akina Nani. Hawajui Kuwa Wao Ni Watu Wa Nyumbani Kwa Mungu (Waefeso 2:19), Hawajui Kuwa Wao Ni Uzao Mteule, Taifa Takatifu, Watu Wa Milki Ya Mungu (1 Petro 2:9-10), Hawajui Kuwa Wao Ni Mawakili Wa Siri Za Mungu Na Watumishi Wa Kristo (1 Wakorintho 4:1), Hawajui Kuwa Wao Ni Mabalozi/ Wajumbe/ Wawakilishi Wa Serikali Ya Mbinguni Hapa Duniani (2 Wakorintho 5:20), Hawajui Kuwa Wao Ni Watawala Hapa Duniani Kwa Niaba Ya Serikali Ya Mungu (Ufunuo 5:9-11), Hawajui Kuwa Wao Ndio Wenye Nafasi Ya Kumruhusu Mungu Au Shetani Kutenda Au Kumzuia Asitende Chochote Duniani (Mathayo 16:18, Mathayo 18:18-20)… Wote Wasiojua Haya, Wanaishi tu Ilimradi, Maisha Yao Hayana TIJA; Wapo wapo Tu Wanakula tu Pumzi Ya Bure Bila Kufanya Mambo Hapa Duniani… Hama Kutoka Huko, Jua Haya, Yaishi Na Ulete Mapinduzi!

3.Hakuwa Tayari Kufanya Chochote Kama Kiko Nje Ya Mapenzi Ya Mungu. Alikuwa Tayari Kuyafanya Mapenzi Ya Mungu Hata Kama Itamgharimu Maisha Yake Na Uhai Wake (Yohana 4:34, Mathayo 26:39, 42)

Wakristo Wengi Wamechoka, Hawana Nguvu Ya Mungu Wala Mafuta (Upako) Kwa Kuwa Hawako Tayari Kumtii Mungu Na Kufanya Cha Kwake. Wanajihurumia, Wanajitanguliza Mbele, Hawako Tayari Kutanguliza Maslahi ya Mungu Na Haki Yake. Wanaishia Kuwa Na Majina Ya Kuwa Hai Lakini Kwakweli Wamepoa Na Hata Kufa Kabisa. KAMA HAUTII CHA MUNGU NA KUFANYA MAPENZI YAKE, HAUFAI KUMWITA BWANA KWAKO WALA MUNGU KWAKO; MAANA HAUNA HATA NIDHAMU KWAKE!
Na USIPOTEZE MUDA WAKO Kujiita Mkristo au Aliyeokoka!

4.Alikuwa Na MUDA WA KUTOSHA NA MUNGU (Luka 6:12, Marko 1:35)

Yesu Amefanya Mambo Yote Aliyofanya Kwenye Maisha Na Huduma Yake Hapa Duniani, Kwa Sababu Ya Kitu Kimoja Kikubwa: Aliutumia Muda Wake Mwingi Na Mungu.
Kuna Wakati Alikesha Akiomba…. Kuna Wakati Alikuwa Busy Akifunga Na Kubadilishana Mawazo Na BABA YAKE.
Kwenye Eneo La Maombi, Waebrania 5:7 inasema, “Alimtolea Mungu DUA, SARA, MAOMBI, MACHOZI na KULIA SANA, Na Mungu Akamsikiliza…”
YESU ALIKUWA MTU WA MAOMBI SANA, ALIPENDA KUKAA NA MUNGU SANA… ALITUMIA MASAA NA MUNGU HALAFU ALITUMIA SEKUNDE AMA DAKIKA KUFUFUA MAITI, KUPONYA WAGONJWA, KUFUNGUA WALIOFUNGWA nk
“Unapotumia Muda Mwingi Na Mungu, Utatumia Dakika Au Sekunde Kadhaa Kutatua Matatizo/ Changamoto Za Maisha”
“Utakapotumia Muda Kidogo Na Mungu, Utatumia Muda Mwingi Kutatua Changamoto Na Matatizo Ya Maisha”

5.Alikuwa MCHA MUNGU (Waebrania 5:7)

Kutokana Na Ucha Mungu Wake Aliweza Kupata Mambo mengine Kwa Urahisi;.Alisikilizwa Na Mungu Kwa Haraka Na Kwa Urahisi Mno, Kutokana Na Kumcha Mungu Alikuwa Na Hekima Ya Juu Sana, Akili Kubwa Mno, Ufahamu Wa Kina nk (Mithali 1:7, Zaburi 111:10).

6.Alikuwa Amejaa Roho Wa Mungu, Na Pia Alikuwa Na Ushirika Wa Dhati Na Roho Mtakatifu (Mathayo 3:16, Luka 4:1, Luka 4:18, Matendo Ya Mitume 10:38 )

Roho Mtakatifu Ndiye Alikuwa MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZOTE Katika Huduma Ya Yesu… Haukufanyika Muujiza Wowote Kwenye Huduma Ya Yesu Bila “Kidole Cha Mungu- Roho Mtakatifu Kuwepo”… Yeye Ndiye Aliyetenda Yote.

Hata Kwenye Kitabu Cha Matendo Ya Mitume, Hatuoni Mitume Wakifanya Lolote Bila Kuwa Na Huyu Roho Mtakatifu Na Ushirika Wa Dhati Na Yeye… Hakuna Muujiza Kwenye MATENDO YA MITUME Usiomuhusisha ROHO MTAKATIFU.

Hakuna Muujiza, Ishara au Maajabu Kwenye Huduma Yoyote Iliyopo Sasa, Bila Roho Mtakatifu Kuwapo. Roho Mtakatifu Ndiye Anayemtukuza Yesu. Roho Mtakatifu Ndiye Mkono Na Kidole/ Chanda Cha Mungu Kinachotenda Kila Muujiza Unaotokea Hapa DUNIANI… Ukimuondoa Roho Mtakatifu, Umeondoa Utendaji Wa Mungu.
Mtumishi Yeyote Wa Mungu Anayemjua Vizuri Roho Mtakatifu, Halafu Akawa Na Ushirika Naye Wa Uhakika, Anatoa Matokeo Yaleyale Aliyotoa Yesu!

7.Yesu Alikuwa Mnyenyekevu (Mathayo 11:29, Wafilipi 2:5-8)

Kabla Ya Heshima Yoyote Toka Kwa Mungu, Kabla Ya Kuinuliwa Au Kupandishwa, Unatangulia Kwanza Unyenyekevu.
Maana Mungu Huwapinga Wenye Kiburi Na Huwapa Neema Wanyenyekevu.
Yesu Alikuwa Mpole Na Mnyenyekevu Wa Moyo. Hii Ilikuwa Pia Ni Tiketi Yake Ya Kuinuliwa, Kukubaliwa na Mungu Na Kutumiwa Na Mungu Kufanya Maajabu!

Haya Niliyotaja, Ni Msingi Wa Maisha Ya Ubora, Ukuu, Ufanisi, Na Upako Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako.
Kitakachokutofautisha Na Wengine Hapa Duniani, Ni AINA YA MATOKEO UNAYOTOA… Na Hautakuwa Kama Yesu Kama Hautafanya Kile Ambacho Yeye Alifanya!

Wanafunzi Wangu, Je Bado Mwanipenda?

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
2 comments on “UNAWEZA KUWA BORA KWA KIWANGO KILEKILE ALICHOKUWA NACHO YESU
  1. Asant rowland says:

    Mungu ameweka content nzito ndan yako,endelea kuubadilisha ulimwengu;Mungu akubariki….!

  2. Henry sadiki says:

    Kiukweli mambo haya munayo tufunza ni mambo ambayo yanatufanya tuishi maisha yanayo mmpendeza mwenyezi mungu katika hali ya ubinafsi kweli bwana wetu akubariki sana baba

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: