HUKUMU YA MUNGU (sehemu ya kwanza)…

hukumu ya mungu

Yako Maeneo Ambayo Hukumu Ya Mungu Itayagusa, Na Hayo Maeneo Nilitaka Kila MMOJA Wetu Ayajue Na Ayatendee Kazi Kila Siku Kabla Ya Kumaliza Muda Wake Hapa Duniani!
Mara tu Mwanadamu Anapokufa, Kinachofuata Ni Hukumu, “Kama Vile Watu Wanavyowekewa Kufa Mara Moja, Na Baada Ya Kufa HUKUMU” (Waebrania 9:27)

Maeneo Ambayo HUKUMU YA MUNGU Itayagusa Ni:

1. MANENO YA VINYWA VYETU
“BASI, NAWAAMBIA, KILA NENO LISILO MAANA, WATAKALONENA WANADAMU, WATATOA HESABU YA NENO HILO SIKU YA HUKUMU. KWA KUWA KWA MANENO YAKO UTAHESABIWA HAKI, NA KWA MA[..]NENO YAKO UTAHUKUMIWA” (Mathayo 12:36-37)
Kinywa Ni Zawadi Ambayo Mungu Ametupatia, Matumizi Ya Ulimi Wako Utayatolea Hesabu Mbele Za Mungu Siku Ya Hukumu Mara Tu Baada Ya Kukata Pumzi Yako Ya Mwisho Hapa Duniani.
Matumizi Mazuri ya Maneno Yako, Yatakufanya Utakaposimama Mbele Za Mungu Siku Ya Hukumu Uhesabiwe Haki. Na Matumizi Mabaya Ya Ulimi Wako Yatakusababisha Kuhukumiwa Siku Ya Mwisho.
Yesu Alitoa Ushauri Ufuatao Kuhusu Mdomo, “Maneno Yenu Na Yawe Machache, Kama Ndiyo semeni Ndiyo Na Hapana Semeni Hapana; Kwa Maana Yazidiyo Hayo (Hapana na Ndio) Yatoka Kwa Yule Mwovu (Ibilisi/ Shetani)”
Suleimani Naye Alionya, “Kunako Maneno Mengi Hapakosi Dhambi” Punguza Kuongea Ongea Ovyo, Si Lazima Kila Neno Linalokuja Mdomoni Mwako Uliseme Nje, Si Kila Wazo Linalokuja Moyoni Mwako Ulitaje Nje.
Petro Naye Aliwahi Kuzungumzia Swala Hili Pale Alipoyarudia Maneno Ya Mtumishi Wa Mungu Daudi, “Kwa Maana Atakaye Kupenda Maisha, Na Kuona Siku Njema, Auzuie Ulimi Wake Usinene Mabaya, Na Midomo Yake Isiseme Hila (Uongo)” (1 Petro 3:10-11)
Kuna Watu Wanajikuta Hata Siku Yao Inakwisha Vibaya, Bila Furaha, Amani Na Changamko Mioyoni Mwao Kwa Sababu Tu Ya Kutoweza Kuuzuia Ulimi.
Paulo Anashauri Hivi, “Maneno Yenu Na Yakolee Munyu (Yawe Na Radha Ya Baraka, Matumaini, Kutia Moyo, Kufariji, Kujenga) Ili Yawafae Wayasikiao”
Aina Ya Maneno Unayoongea, Ni Matokeo Ya Taarifa Ulizoyalisha Masikio Na Macho Yako; Kile Ulichoona Na Kile Ulichosikia Ndicho Utakachoongea, Kile Ulichoweka Kwenye Moyo Wako Ndicho Utakachoongea Nje, “Maana Kinywa Cha Mtu Huyanena Yaujazayo Moyo Wake; Mtu Mwema Katika Hazina Yake Njema Hutoa Maneno Mema, Na Mtu Mbaya Katika Hazina Yake Mbaya Hutoa Mabaya” (Mathayo 12:34-35)
Unachoweka Katika HAZINA YAKO- MOYO WAKO Ndicho Utakachotoa Nje, Ndicho Utakachoongea!
Kuwa Makini Na Unachoingiza Moyoni Mwako, Jiepushe Na SHAURI LA WASIO HAKI, BARAZA LA WENYE MIZAHA NA NJIA YA WAKOSAJI (Zaburi 1:1-2), Hakikisha UNAULINDA MOYO WAKO KULIKO YOTE ULINDAYO (Mithali 4:23)

2.KAZI

Eneo Jingine Ambalo Mungu Atahukumu Siku Ya Mwisho, Pale Mtu Atakapomaliza Muda Wake Hapa Duniani Ni Eneo La Kazi Alizofanya Hapa Duniani; Mungu Atahukumu Aina Mbili Za Kazi; KAZI ZA KAWAIDA KWENYE MAISHA NA KAZI YA MUNGU MAISHANI MWA MTU.

a) KAZI YA KAWAIDA KWENYE MAISHA
Kila Mmoja Wetu Kuna Kazi Ambayo Anaifanya Kwa Sasa, Aidha Ni Yake Mwenyewe Au Ya Kuajiriwa… Wale Mlioajiriwa; Mungu Atawahukumu Kwenye Eneo La Uaminifu: Kama Haukuwa Mwaminifu Kwenye Kitu Cha Mwenzako, Mungu Hatakuamini Kwa Ajili Ya Chako, Kama Haukuwa Mwaminifu Katika Madogo, Mungu Hatakwamini Katika Makubwa… Unakumbuka Mfano wa TALANTA? Mungu Alitaka TUJIFUNZE UMUHIMU WA KUTUMIA VILE MUNGU ALIVYOWEKA MAISHANI MWETU… KWA KILA KIPAWA, KARAMA, ZAWADI, KIPAJI ULICHOPEWA, MUNGU ANATEGEMEA UZALISHE, UWE NA TIJA. Kwa Wale Mlioajiriwa, Mungu Atalitazama Pia Eneo La UWAKILI: Mungu Amekupa Nafasi Mahali Ulipoajiriwa, Unapofanya Kazi Ili Uwe WAKILI/ MWAKILISHI WAKE MAHALI PALE, Uioneshe NURU NA CHUMVI Mahala Pale, Ili Kila Atakayekuona Pale, Akiri Kwamba Wewe Ni Mtu Wa Mungu. Kila Atakayeona Matendo Yenu, Amtukuze Baba Yenu Wa Mbinguni (Mathayo 5:13-16)… Usiwe Kiongozi Wa MIGOMO Kwenye Maeneo Ya Kazi, Bali Hakikisha Kama Unaiona Kasoro Au Tatizo Mahali Pa Kazi, Mwombe Mungu HEKIMA, Chukua Masuluhisho Na Majibu Ya Kurekebisha Au Kuondoa Ile SHIDA/ KERO Na Uziwasilishe Kwa Uongozi Wa Juu… Uwe Mtu Wa Kutatua MATATIZO Kwenye Eneo LAKO LA KAZI Na Si Kiongozi Wa Migomo… Mtu Anayegoma Maana Yake Hana Suluhisho/ Majibu Na Anataka Hao ALIOWAGOMEA Wamsaidie Kutatua Kero/ Tatizo Lake… Pia Kwenye Eneo Lako La Kazi: UWE KIELELEZO KWA MWENENDO, TABIA NA USEMI… Kila Mtu Pale Ofisini Amwone YESU Kupitia Wewe… UWE INJILI WAZI MAHALI PAKO PA KAZI!

b) KAZI YA MUNGU MAISHANI MWAKO
Japo Nimetenganisha Kazi Yako Ya OFISI Na Utumishi Wa Huduma, Lakini Ukweli Ni Kwamba Zote Mbili Ni Ofisi Za Mungu, Ni Madhabahu Za Mungu Maishani Mwako. Kazini Kwako Ni Mahali Pa KUMWINUA NA KUMTUKUZA MUNGU KWA UTENDAJI WAKO, NI MAHALI PA UWAKILI WAKO KAMA RAIA WA MBINGUNI… UBORA WAKO UTAKUPA CREDDIT/ ALAMA KWENYE KITABU CHA MATENDO MBINGUNI.
Kuhusu Kazi Ya Mungu; Kuna Vipawa, Karama, Huduma Mungu Ameweka Ndani Yako Kwa Ajili Ya KUUJENGA MWILI WAKE… Unaweza Kumtumikia Mungu Kwenye Eneo Unakosali, Hata Kama Si Mwalimu Kama MIMI Au MHUDUMU WA MADHABAHUNI… Unaweza Usiwe Mwinjilisti, Mchungaji, Mtume, Nabii, Mwanakwaya, Mzee Wa Kanisa, Shemasi nk Lakini Bado Unaweza Kumtumikia Mungu na KUINGIZA CREDIT MBINGUNI; Unaweza Kujituma Katika Maeneo Ya KUTEGEMEZA NYUMBA YA MCHUNGAJI, Kifedha, Mavazi, Chakula, Kusomesha Watoto wake, Kwenda NYUMBANI KWAKE Kufanya shughuli ndogo ndogo kama Kufua Nguo zake, watoto wake, Kuzipiga Pasi nk Pia Unaweza Kujituma Kufanya Shughuli Kama Vile Kufanya USAFI WA KANISA NA MAZINGIRA YAKE, VIWANJA, VYOO, OFISI, KUFUTA VITI nk Pia Hata Kwa Kununua Vitu Kanisani Kwako Vile Ambavyo Ni Vya Muhimu Na Unadhani Viko Ndani Ya Uwezo Wako Kifedha… KUMTUMIKIA MUNGU KUNAHITAJI MAAMUZI YANAYOHUSISHA NGUVU, AKILI NA MALI YAKO.
“AMELAANIWA AIFANYAYE KAZI YA MUNGU KWA ULEGEVU”
“UNAWAZA NINI KWA AJILI (JUU ) YA BWANA?” (Nahumu 2:9)… Nini Unaweza Kufanya Kwa AJILI YA MUNGU NA KAZI YAKE? FIKIRIA VEMA NA UANZE KUTENDA.
Kumbuka: “KILA KAZI YA MTU ITAPIMWA; ALIYEJENGA KWA NYASI ATAPOTEZA, ALIYEJENGA KWA DHAHABU ATANG’ARA”
Kazi Ni Kwako Mwana Wa Mungu!

Tukutane Katika Sehemu Ya Pili Ya Somo Hili, Mwl D.C.Kabigumila!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “HUKUMU YA MUNGU (sehemu ya kwanza)…
  1. Yeremia kitila says:

    Ubarikiwe mtumishi kwa ujumbe

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: