HUKUMU YA MUNGU (Sehemu Ya Pili)

hukumu

Nakukaribisha Kwa Jina La Yesu Ili Ujifunze Pamoja Nami Katika Sehemu Ya Pili Ya Somo Hili. Kama Haujaipitia Sehemu Ya Kwanza Ya Somo Hili, Hakikisha Unaipitia.
Somo Hili Linahusiana Na Mambo Gani Ambayo MUNGU Atayashughulikia Kwenye Hukumu. Maana Watu Wote Tunajua Kuwa Kila Mwanadamu Aliyezaliwa Na Mwanamke, Siku Zake Za Kuishi Ni Chache, Na Kuna Siku Ambayo Atamaliza Muda Wa Kuishi Na Atasimama Mbele Za Mungu Kwa Ajili Ya Hukumu. Maana Imeandikwa, ” Kama Vile Wanadamu Walivyoandikiwa Kufa Mara Moja Na Baada Ya Kufa Hukumu” ( Waebrania 9:27).

Kwahiyo Kama Kuna Hukumu Mara Tu Baada Ya Mtu Kufa, Ni Muhimu Pia Kuyajua Maeneo Ambayo Hukumu Ya Mungu Itagusa, Kwa Mujibu Wa Neno La Mungu, Ili Ujipange Na Kuwa Bora Kwa Msaada Wa Roho Mtakatifu Aliye Msaidizi Na Mwezeshaji Wetu Hapa Duniani!
Katika Sehemu Ya Kwanza Ya Somo Hili, Inayopatikana Kwenye Profile Yangu, Nimeyagusa Maeneo Mawili Ambayo Mungu Atayahukumu. Maeneo Hayo Ni Pamoja Na:

1.MANENO YA VINYWA VYETU
Mathayo 12:36-38[..]

2. KAZI;

Na Kazi Zimegawanyika Katika Maeneo Mawili Ambayo Ni, a) KAZI YA KAWAIDA INAYOKULIPA MSHAHARA; Hasa Kwa Walioajiriwa Serikali Au Kwenye Makampuni Binafsi…. Kuna Mambo Mengi Ambayo Mungu ATAYAHUKUMU Siku Ya Mwisho Kuhusiana Na Kazi Ambayo Ni Pamoja Na UAMINIFU, UADILIFU, UWAJIBIKAJI NA ENEO LA UWAKILI, Ambapo Mungu Atamhukumu Mkristo Kwa Kutegemea Jinsi Gani Alimtumikia Mungu Kama Wakili Wa Serikali Ya Ufalme Wa Mungu… Ni Kwa Namna Gani Na Kiasi Gani Alikuwa NURU NA CHUMVI Kwenye Eneo Lake La Kazi Na Kumdhihirisha Yesu Kupitia Kazi Yake!
(Kupata Kwa Undani Kuhusu Maeneo hayo mawili hapo Juu Hakikisha Unasoma HUKUMU YA MUNGU Sehemu Ya Kwanza Ambayo Iko Hapahapa Kwenye Profile Yangu)

3.FAMILIA
Eneo La Tatu Ambalo Hukumu Ya Mungu Itagusa, Ni Eneo La Familia, Na Familia Inajumuisha BABA, MAMA, NA WATOTO Na Kila Mmoja Kwa Nafasi Yake ATASIMAMA MBELE ZA MUNGU KWA AJILI YA HUKUMU.

a)Baba : Baba Wa Familia Atasimama Mbele Za Mungu Kwa Ajili Ya Maeneo Mawili; Kama Mme Na Pia Kama Baba/ Mzazi

KAMA MME:
Mme Atasimama Mbele Za Mungu Kwa Ajili Ya Kueleza Uwajibikaji Wake Kama Mme, Yaani Atasimama Kutoa Hesabu Kuhusu Namna Alivyokaa Na Mkewe Na Uwajibikaji Wake Kwa Mke Wake… Mme Anayo Majukumu Ya Kufanya Kwenye Familia Ambayo Kama Akiyafanya vema, Mungu Atamhesabia Haki, Ila Akichemka Mungu Atamhukumu, Tuyapitie Maandiko Sasa:

“Enyi Waume WAPENDENI WAKE ZENU KAMA KRISTO NAYE ALIVYOLIPENDA KANISA, AKAJITOA KWA AJILI YAKE” (Waefeso 5:25) Mme Atatoa Hesabu Kwenye Eneo La Kumpenda Mkewe… Tena Si Kumpenda Kwa Sababu Ya Mema Tu Hapana, Kumpenda Kwa Aina Ya Upendo Aliokuwa Nao Yesu Kwa Kanisa… Upendo Wa Kuwa Tayari Kufa Kwa Ajili Ya Mkeo… Kumsamehe Hata Ukimkuta Na Kosa Kubwa Kiasi Gani Sawa Na Yesu Alivyolisamehe Kanisa… Hata KAMA UKIMFUMANIA MKEO, FANYA KAMA YESU ALIVYOFANYA KWA KANISA… Kiwango Hiki Cha Upendo Ndicho Atakachohukumiwa Mme.
“VIVYO HIVYO IMEWAPASA WAUME NAO KUWAPENDA WAKE ZAO KAMA MIILI YAO WENYEWE. AMPENDAYE MKEWE HUJIPENDA NAFSI YAKE MWENYEWE.MAANA HAKUNA MTU ANAYEUCHUKIA MWILI WAKE POPOTE; BALI HUULISHA NA KUUTUNZA… LAKINI KILA MTU AMPENDE MKEWE KAMA NAFSI YAKE MWENYEWE…” (Waefeso 5:28-29, 33)… Maana Hakuna Mtu Auchukiaye Mwili Wake popote Bali Huulisha Na Kuutunza… Hili Ni Jukumu La Mme KUMLISHA MKEWE NA KUMTUNZA [Kumvisha, kumtunza na kuhakikisha anaendelea kupendeza].
“NINYI WAUME WAPENDENI WAKE ZENU MSIWE NA UCHUNGU NAO” (Wakolosai 3:19)… Ni Wajibu Wa Mme Kutafuta Mwafaka Na Mkewe Likitokea Lolote Lisilo Jema Kati Yao; Mme Anapaswa Kutatua Jambo Hilo Na Kusamehe Na Kuepusha UCHUNGU KUKAA NDANI YAKE, Kama Akiwa Na Uchungu Na Mkewe, Hiyo Ni Dhambi, Maana Yesu Angekuwa Na Uchungu Dhidi Yetu Kwa Mapungufu Yetu, Hali Ingekuwaje? (Pia soma 1Petro 3:7) KAZI KWENU WAUME!

KAMA BABA:
Kama Baba Wa Familia, Mungu Ana Mategemeo Makubwa Kwa Baba Kuwa Kiungo Muhimu Katika MALEZI YA WATOTO. Lakini Kwa Familia Nyingi Kazi Ya Kulea Wameachiwa Akina Mama, Hii Si Sawa Na Mungu Atawawajibisha Akina Baba Kwa Uharibifu au Mmomonyoko wa Maadili Ya Watoto… “NANYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU; BALI WALEENI KATIKA ADABU NA MAONYO YA BWANA” (Waefeso 6:4)… Kazi Ya Kuwalea Watoto Katika ADABU NA MAONYO YA MUNGU Ni Ya Baba… Kama Baba Utasimama Mbele Za Mungu Kutoa Hesabu Kwa Ajili Ya Malezi Ya Watoto Wako, Mungu Atakuhesabia Haki Au Kukuhukumu Kwa Malezi Yako Utakayotoa Kwa Wanao.

MKE: Kama Mke, Utasimama Mbele Za Mungu Kutoa Hesabu Kuhusiana Na Uwajibikaji Wako Kwa Mmeo. Ubora Wako Utakufanya Uhesabiwe Haki Na Uzembe Wako Utakusababisha Uhukumiwe!
“ENYI WAKE, WATII WAUME ZENU KAMA KUMTII BWANA WETU” (Waefeso 5:22)… Kuna Kiwango Cha Utiifu Cha Juu Sana Ambacho Mke Anapaswa Kukionesha Kwa Mme Wake. Biblia Inasema KAMA KUMTII BWANA WETU… Kwa Lugha Rahisi, “MKE AMTII MMEWE KWA KIWANGO KILE KILE AMBACHO ANAMTII BWANA YESU” Kama Unamchukulia Poa Mmeo, Akiongea Na Wewe Unainua Mdomo Wako Kujibizana Naye, Hauwezi Kujishusha, Na Kutafuta Suluhu Kwa Utiifu, Kuna Siku Utajieleza Mbele Za Mungu Kwa Ajili Ya Hilo… Utatoa Hesabu Kwa Ajili Ya Utiifu Wako… Kama Mke Unahitaji Uwezesho Wa ROHO WA MUNGU Kuweza Kumtii Mke Kama Au Kwa Kiwango Cha Kumtii BWANA WETU… Jitahidi Kwa Maombi, Sala Na Dua, Mungu Akusaidie Uwe Bora!
Pia Mke Anawajibu Wa Kumlinda Mme Wake Kiroho Na Kimwili… Maana Imeandikwa, “MUNGU AMEFANYA JAMBO JIPYA DUNIANI, YA KWAMBA MKE ATAMLINDA MME WAKE” (Yeremia 31:22b)
Unamkumbuka Abigaeli? Alimlinda Mmewe Nabali Asiuawe Na Mfalme Daudi… Wewe Mke Unamlinda Mkeo? Huu Ni Wajibu Mpya Wa Mwanamke Toka Kwa Mungu…LAZIMA UMLINDE MMEO KWA MAOMBI NA KWA VITENDO [Ila Kwa Hekima Na Uongozi Wa Mungu]. (Pia soma 1 Petro 3:1-6)

KAMA MAMA: Mwanamke, Aliye Mzazi, Hatasimama Mbele Za Mungu Kwa Ajili Ya Kutoa Hesabu Kwenye Eneo LA UTII KWA MMEWE KAMA KUMTII BWANA na KUMLINDA MMEWE… Pia Atasimama Mbele Za Mungu Kwenye Eneo La Malezi… Malezi Ya Watoto Katika Njia Ya Bwana Na Maonyo Yake Pia Ni Jukumu Kwa Mama Akishirikiana Na Baba Aliye Mmewe… Aina Ya Malezi Unayotoa Kama Yako Kinyume Na Maonyo Ya Bwana, Itakugharimu Siku Ya Hukumu. Ila Ukiwalea Wanao Katika Njia Ya Bwana, Utahesabiwa Haki Siku Ukisimama Mbele Za Mungu Hukumuni!

WATOTO: Watoto Nao Ni Sehemu Ya Familia, Na Mungu Atawahukumu Pia Kwa Namna Walivyoishi Na Wazazi Wao. Jukumu Kubwa La Watoto Litakalowapelekea Kuhukumiwa Au Kuhesabiwa Haki Hukumuni Ni Namna Ambayo WALIVYOWATII NA KUWAHESHIMU WAZAZI WAO NA PIA NAMNA AMBAVYO WALIWAJIBIKA KUWATUNZA WAZAZI WAO… Kama HAUNA MAHUSIANO MAZURI NA WAZAZI WAKO; HAITAISHIA KUKUZUILIA MAISHA MAREFU YA BARAKA NA YA AMANI DUNIANI BALI PIA ITAKUFANYA USIMAME MBELE ZA MUNGU KUTOA HESABU HUKUMUNI. Kama Una Mzazi Aliye Hai, Hakikisha Unakuwa Na Mahusiano Bora Na Ya Uhakika. Kama Uliwakorofisha Au Kuwakasirisha Wazazi Wako Nenda Katengeneze Nao, Nenda Kawaangukie Na Kuwaomba Msamaha. Nenda Kapatane Nao… Pia Anza Kuawahudumia Na Kuwasaidia Pale Unapoweza. Tunza Sana Mahusiano Yako Na Mungu Kwa Kuwa Vizuri Na Wazazi Wako.
(Mistari Ya Neno La Mungu Kuhusu Watoto Na Wajibu Wao Kwa Wazazi: Waefeso 6:1-3, Wakolosai 3:20, Kutoka 20:12, Kumbukumbu 5:16)

Tukutane Katika Sehemu Ya Tatu Ya Somo Hili,
Mwl. D.C. Kabigumila.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: