MATENDO MEMA NI LAZIMA KWA MKRISTO ALIYEOKOKA

..

..NI UDHIHIRISHO KUWA MUNGU MWEMA ANAKAA NDANI YAKO

Kuna Watu Wanashindwa Kuielewa NEEMA… Wanadhani Baada Ya Neema Ya Mungu Kutupa Fursa Ya Kuokolewa Kwa Njia Ya Imani Iliyo Katika Kristo Yesu, Hatuna Kitu Tena Cha Kuonyesha Nje Au Kufanya Kudhihirisha UHALISI WA KILE WOKOVU ULICHOFANYA NDANI YETU… Hawa Wakristo ‘WA NEEMA’ Hawataki KUKUBALI Kuwa WOKOVU UNAAMBATANA NA MABADILIKO KWENYE MAISHA YA MTU; MATENDO YAKE YAKIWA NDICHO KIDHIBITISHO CHA KWANZA NA CHA MUDA WOTE KUHUSU BADILIKO LA KIROHO LILILOTOKEA NDANI YA MWAMINI… Hawa WAKRISTO WA NEEMA, Wanaendesha MAISHA YASIYO MATAKATIFU, WAKIWA NA KAULI MOJA TU, “TUNAOKOLEWA KWA NEEMA SI KWA MATENDO” (Waefeso 2:8-9)
LAKINI Wanayaacha Maneno Ya Msingi Yaliyosemwa Mstari Unaofuata, ” MAANA TU KAZI YAKE, TULIUMBWA KATIKA KRISTO YESU, TUTENDE MATENDO MEMA, AMBAYO TOKEA AWALI MUNGU ALIYATENGENEZA ILI TUENENDE NAYO [Au Tuishi Ndani Ya Hayo]” (Waefeso 2:10).

Mtume Paulo, Mhubiri Mahiri Wa Neema, Hakuwahi Kuifungia Nje Sehemu Muhimu Ya Matendo Mema Katika Maisha Ya Mwamini. Naye Anatufundisha Hivi, ” MAANA TU KAZI YAKE, TULIUMBWA KATIKA KRISTO YESU, TUTENDE MATENDO MEMA, AMBAYO TOKEA AWALI MUNGU ALIYAUMBA/ ALIYATENGENEZA ILI TUENENDE NAYO” (Waefeso 2:10) Lakini Pia Katika Barua Yake, Kwa WAGALATIA, Mtume Paulo Anasisitiza Juu Ya Umuhimu Wa Matendo Mema, ” TENA TUSICHOKE KATIKA KUTENDA MEMA; MAANA TUTAVUNA KWA WAKATI WAKE, TUSIPOZIMIA ROHO. KWA KADRI TUPATAVYO[..] NAFASI NA TUWATENDEE WATU WOTE MEMA; NA HASA JAMAA YA WAAMINIO” (Wagalatia 6:9-10).

Mtume Petro Naye Amezungumzia Umuhimu na Ulazima Wa MATENDO MEMA Kwa Mkristo/ Mwamini, Naye anasema, ” NAYE NI NANI ATAKAYEWADHURU MKIWA NA BIDII KATIKA KUTENDA MEMA” (1 Petro 3:13) na Pia Mahali Kwingine Anasema, “MAANA NI AFADHALI KUTESWA KWA KUTENDA MEMA, IKIWA NDIYO MAPENZI YA MUNGU, KULIKO KWA KUTENDA MABAYA” (1 Petro 3:17).

Mtume Yohana Naye Anatufundisha Sisi Kuhusu Ulazima Na Umuhimu Wa Matendo Mema Kwa Mkristo Hasa Anayedai Ameokoka. Naye Anasema, ” MPENZI, USIUIGE UBAYA, BALI UIGE WEMA. YEYE ATENDAYE MEMA NI WA MUNGU, BALI YEYE ATENDAYE MABAYA HAKUMWONA MUNGU” (3 Yohana 1:11)
Kama Matendo Mema Hayaonekani Ndani Ya Maisha Yako; Wokovu Wako Una Walakini!

Yesu Aliye Mwanzilishi Na Mkamilishi Wa Imani Yetu Hakuacha Kuzungumza Juu Ya Ulazima Na Umuhimu wa Matendo Mema, Naye Anasema, ” MAANA KILA MTU ATENDAYE MABAYA HUICHUKIA NURU, WALA HAJI KWENYE NURU, MATENDO YAKE YASIJE YAKAKEMEWA. BALI YEYE ATENDAYE KWELI HUJA KWENYE NURU, ILI MATENDO YAKE YAONEKANE WAZI YA KUWA YAMETENDWA KATIKA MUNGU” (Yohana 3:20) Pia BWANA YESU Anasema, ” NINYI NI CHUMVI YA DUNIA… NINYI NI NURU YA ULIMWENGU… VIVYO HIVYO NURU YENU IANGAZE MBELE YA WATU, WAPATE KUYAONA MATENDO YENU MEMA, WAMTUKUZE BABA YENU WA MBINGUNI” (Mathayo 5:13-14, 16) Na Pia Anasema, ” JIHADHARINI NA MANABII WA UONGO, WATU WANAOWAJIA WAMEVAA MAVAZI YA KONDOO, WALAKINI KWA NDANI NI MBWA MWITU WAKALI. MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO. JE! WATU HUCHUMA ZABIBU KATIKA MIIBA, AU TINI KATIKA MIBARUTI?. VIVYO HIVYO KILA MTI MWEMA HUZAA MATUNDA MAZURI; NA MTI MWOVU HUZAA MATUNDA MABAYA. MTI MWEMA HAUWEZI KUZAA MATUNDA MABAYA, WALA MTI MWOVU KUZAA MATUNDA MAZURI. KILA MTI USIOZAA TUNDA ZURI HUKATWA NA KUTUPWA MOTONI” (Mathayo 7:15-19).

HAKUNA UKRISTO, WOKOVU BILA KUWA NA MATENDO MEMA, WOKOVU NA MUNGU KUJA NA KUISHI NDANI YAKO, NA UWEPO WAKE UNADHIRISHWA NA MATUNDA YA MKRISTO HUSIKA!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: