MSISITIZO KWENYE MAOMBI ( CONSISTENCY IN PRAYER)

msisitizo wa maombi

Wakristo Wengi Wanadhani Muda Wa Kwenda Mbele Za Mungu (Kuomba) Ni Kipindi Cha Misukosuko Na Magumu. Lakini Hii Si Kweli. Maana Halisi Ya Maombi Ni “MAONGEZI BAINA YA MWANADAMU (Mwenye Vigezo Vya Kumsogelea Mungu) NA MUNGU” Maongezi Haya YANAWEZA KUWA YA AINA YOYOTE Sawa Na Yale Ya Baba Na Mtoto Wake.

Lakini Wengi Wetu Tunadhani MAOMBI Ni Kwenda Mbele Za Mungu Kwa Ajili Ya KUTAKA MSAADA tu… Mtazamo Wa Wengi Umeishia Kutaka tu MSAADA. Na Kama Wana Nyakati Ambazo HAWAPITII MAGUMU, Wengi Wamekuwa Wanakosa Muda Wa KUKAA KWENYE MAOMBI Maana HAWANA WANALOHITAJI/ HAWANA CHANGAMOTO… Lakini Hili Si Jambo Sahihi, MAOMBI Ni Zaidi Ya Kwenda Mbele Za Mungu Kwa Ajili Ya Kuomba MAHITAJI YAKO AU KUOMBA MSAADA KWENYE CHANGAMOTO.

MAOMBI Ni Mawasiliano Ya Wakati Wote Kati Ya Mungu Na Wanae; Ni Mahusiano Ya Kimawasiliano Kati Ya Baba Na Watoto Wake.
MAOMBI Kwa UPANA WAKE Ni Kitendo Cha Kujitenga, Kukaa Pembeni, Mahali Pa Utulivu (Yesu Anapaita CHUMBA CHAKO CHA NDANI), Na KUUMIMINA MOYO WAKO MBELE ZA MUNGU KAMA MAJI (Maombolezo 2:19), Na Kutokea Hapo Mawasiliano Ya NDANI KATI YA BABA NA MTOTO HUANZA… Hapa Ndipo Mtu Anaweza KUFUNGUA KINYWA NA KUTOA MANENO NJE AU KUONGEA NA MUNGU MOYONI PASIPO KUTOA SAUTI NJE.
Unaweza Kwenda FARAGHA NA MUNGU Ukiwa Na Lengo La KUMSIFU, KUMWABUDU Kwa MANENO YA MOYO WAKO… Kumshukuru Kwa Aliyotenda, Anayotenda Na Unayotegemea Atatenda Kwako (Yeremia 29:11)… Inaweza Kuwa Kwa Nia Ya Kwenda Mbele Za Mungu Ili KUJIPUMZISHA KWENYE UWEPO WAKE NA KUUTAFAKARI UZURI WAKE (Zaburi 27:4). Inaweza Kuwa Kwenda Mbele Za Mungu Kwa Nia Ya KUMUULIZA HABARI YA MAMBO YAJAYO KWAKO, FAMILIA, TAIFA, KANISA nk (Isaya 45:11)… Inaweza Kuwa Kwa Ajili Ya Kumuuliza Mungu Kuhusu WAZO LAKE AU MTAZAMO WAKE KUHUSU JAMBO FULANI (Isaya 55:6-9)…Inaweza Kuwa Kwa Ajili Ya KUUNGAMA, KUTUBU AU KUOMBA REHEMA JUU YA JAMBO FULANI (1 Yohana 1:8-10)… Inaweza Kuwa Kwa Ajili Ya KWENDA KUOMBA MSAADA/ UWEZESHO (Isaya 41:10, Waebrania 13:6, Wafilipi 4:13)… Inaweza Kuwa Kwa Ajili Ya Kutaka USHAURI Au MWONGOZO (Isaya 9:6, Yohana 16:13, Warumi 8:14).

Kwa hiyo, Lengo La MAOMBI Si Kupeleka Mahitaji Yetu Kwa Bwana tu… Ni Zaidi Ya Hayo, Ni Kujenga Mahusiano Ya Kina Na Bwana, Ni Kujenga Ushirika Wa Kina Na Roho Wa Mungu, Ni Kuyatafakari Maneno Yake Uweponi Mwake NA Kupokea Nuru Na Ufunuo Toka Kwake Moja Kwa Moja, Ni Kuufurahia Uwepo Wake, Nguvu, Utukufu Na Pendo Lake… Ni Zaidi Ya Kumuuliza Ule Nini, Uvae Nini, Na Yafananayo Na Hayo… Ni Kukaa Uweponi Mwake, Miguuni Pake Na Wakati Mwingine Kifuani Mwake… Ni Kupata Uzoefu Wa Mbinguni Duniani… Ni Kushiriki Tabia Ya Uungu!

Unapokuwa Mtu Wa Maisha Ya Maombi (Consistent In Prayer) Unajikuta Unaanza Kutoa Matokeo Kama Yake; Hauwezi Kuwa Na Muda Na MUNGU MWENYE HEKIMA Halafu Wewe Usiwe Na Matokeo Yaliyojaa Hekima Itokayo Juu… “Enenda Na Wenye Hekima, Nawe Utakuwa Na Hekima” Pia Kumbuka, “Chuma Hunoa Chuma” … Watu Wote WALIOTEMBEA NA MUNGU (WATU WA MAOMBI) Wameacha ALAMA Kwenye VIZAZI VYAO NA DUNIA YAO, Ni Watu Walio Kwenye Historia Leo!

Watu Kama Andrew Murray, Charles Huddon Spurgeon, Charles G Lake, Charles Finney, Terry Moody, A.A. Allen, Kathrin Kuhluman, Mariah Woodworth Etter, Kenneth Haggin, Smith Wigglesworth, Benson Idahosa Nk Ni Watu Ambao Wamefanya Mambo Makubwa Kwenye Dunia Ya Karibuni (Karne Ya 19 na 20) Na Siri Yao Kubwa Ilikuwa Ni MAOMBI… Ushirika Na Mungu Kupitia Maombi. Na Wameacha Historia Kubwa Sana Ambayo Haiwezi Kufutwa Na Mwanadamu; Dunia Inaendelea Kufurahia Uwepo Wao, Lakini Siri Yao Kubwa NI CONSISTENCY IN PRAYER!

Jizoeze Kuomba; Anza Kwa Robo Saa, Nusu Saa, Saa 1, 2,3…6, 12 na Kuendelea. Hata Kama Una Uvivu Au Uzembe, Wewe Anza tu, Mwombe Mungu Akupe Nguvu Ya Kuendelea, Na Utapata Mpenyo (Breakthrough) Kwenye Shule Ya Maombi.

Kama Ndugu Zangu WAISLAMU Wanaweza Kwenda Mbele Za “Mungu Wao Anayesikiliza Toka Upande Mmoja” Mara 5 Kwa Siku, Itakuwaje Kwako Mkristo Ambaye Mungu Wako Yuko Kila Mahali, Hana Mipaka, Yu Karibu Na Wala Si Mbali, Anasikiliza, Anajibu Na Kuongea… Nadhani Umefika Wakati Mwafaka Wa Kuwa Waombaji Wa Kina Kama Tunataka Kuwa Na Maisha Yenye Ufanisi!

“KAMA UKITUMIA MASAA NA MUNGU, UTATUMIA DAKIKA KADHAA AU SEKUNDE KADHAA KUTATUA MASWALA YA MAISHA… ILA UKITUMIA DAKIKA NA MUNGU, UTATUMIA MASAA KUTATUA MASWALA YAKO YA MAISHA”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: