TOFAUTI KATI YA MAMBO YA ROHONI NA YALE YA MWILINI

..

Mambo Ya Mwilini Ni Yale Mambo Ambayo Unaweza Kuyapima Na Kuyachunguza Kwa Kwa MILANGO MITANO YA FAHAMU; Mambo Ambayo YANAONEKANA KWA MACHO, YANASHIKIKA NA KUHISIKA, YANAYOWEZA KUONJEKA KWA ULIMI, YANAYONUSIKA KWA PUA NA KUSIKILIZIKA KWA MASIKIO… LAKINI Mambo Ya Rohoni Ni Yale Mambo Yasiyoweza Kupimika Au Kuchunguzika Kwa Kutumia MILANGO MITANO YA FAHAMU; Mambo Ambayo Macho Hayajawahi Kuona, Masikio Kusikia Wala Hayawezi Kuingia Kwenye Moyo Wa Mwanadamu, Mambo Ambayo Mungu Amewaandalia Wale Wampendao; Mambo Ambayo Mungu Anatufunulia Sisi Tulionunuliwa Kwa Damu Yake Kupitia Roho Wake, Maana Anayujua Na Kuyachunguza Mambo Yote, Hata Mafumbo Ya Mungu (1 Wakorintho 2:9-10)! Mambo Ya Rohoni Yanatambuliwa Na Watu Wa Rohoni, Maana Yanajulikana Na Kutafsiriwa Kwa Njia Ya Rohoni, Na Mungu Ametupa Roho Wake Makusudi Tupate Kuyajua Yale TULIYOKIRIMIWA [ Tuliyopewa Na Baba Kwa Ukarimu]… (1 Wakorintho 2:13-15, 12). Mtu Yeyote Ambaye HANA ROHO WA MUNGU, Hawezi Kutambua Mambo Ya Rohoni; Hawezi KUZIJUA AHADI NA HAKI ZAKE KATIKA KRISTO YESU NA PIA HAWEZI KUJUA VIWANGO VYA UFALME WA MUNGU KWENYE MAENEO YA DHAMBI, HAKI NA HUKUMU, MAANA ROHO WA MUNGU ALIYEMO NDANI YETU NDIYE AYAANDIKAYE KWENYE VIBAO VYA MIOYO YETU ( Yohana 16:8, 13-15, Waebrania 8:10-11). Mtu Wa Rohoni Hashangazwi Na Mgonjwa Wa UKIMWI Kuponywa Ama Mgonjwa WA KANSA Kuwekwa Huru, Wala Aliyefungwa Na Ibilisi Kuwekwa Huru, Aliye Tasa Kuzaa, Aliyekufa Kufufuka Na Kuishi Tena, Aliyepooza Kusimama Na Kurudi Kuendelea Na Shughuli Za Ujenzi Wa Taifa Au Aliye Na Matundu Kwenye Moyo Kuziba… Maana Haya Ni Mambo Ya Rohoni, Yanayofanyika Kwa Urahisi Kwa KIDOLE CHA MUNGU ALIYE ROHO (Yohana 4:24)!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “TOFAUTI KATI YA MAMBO YA ROHONI NA YALE YA MWILINI

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: